KKKT Mbezi Beach msilazimishe waumini kuabudu kwa Kiingereza

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,280
2,000
Wakati Taifa lina lengo la kuimarisha matumizi ya lugha yetu kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na elimu wapinzani wa taifa kujikomboa kwenye ukoloni wa lugha na utamaduni wa kigeni wanajibu mapigo kupitia makanisa.

Kama muomini wa KKKT Mbezi Beach sioni mahitaji na ungezeko la ibada na mafunzo ya sunday school kwa Kiingereza.

Ilianza kidogo kwa misa chache sasa kila Jumapili na kwa sikukuu ya chrismas na mwaka mpya. Naona kuna wazee wa usharika wamejaa kasumba ya Kiulaya, binafsi sipendelei jambo hili.

Nina hakika mahitaji ya misa kwa Kiingereza ni madogo sana au hakuna kwa hiyo viongozi wasitulazishe kukosa misa ya pili saa 4.00 asubuhi kwa Kiswahili eti inageuzwa ya Kiingereza.
Ingekua jambo la maana kanisa kuanzisha darasa la lugha ya kiswahili kwa hao waomini wachache badala ya kuwawekea ibada muda muafaka kwa waomini wengi.

Kama ndio usomi mwenyewe ni msomi ngazi ya uzamili ila sipendi kulimbukia utamaduni wa watu wengine.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,863
2,000
Kama ibada ya Kiingereza inakukwaza, hudhuria za Kiswahili acha kulalamika. Baadhi ya makanisha ya kikatoliki walikuwa na utaratibu wa ibada za Kilatini siku za nyuma sina hakika siku hizi kuna makanisa bado yanazo.

Pia baadhi ya makanisa hususan ya mijini yana utaratibu wa baadhi ya ibada kuendeshwa kwa Kiingereza ili ku-accommodate wale wasiojua Kiswahili ni kawaida sana.

Huku kwetu masaini, KKKT huendesha baadhi ya ibada kwa Kimasai ili ku-accommodate wale wasiojua Kiswahili nayo ni kawaida sana tuache kulalamika.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,924
2,000
Sasa makabwela watasali Wapi!
Kuna misa ya kiswahili na kiingereza. Muumini unachagua inayokufaa. Na tukumbuke kuwa Tanzania hatuishi watanzania peke yetu, tuna wageni ambao wangependelea zaidi misa ya Kiingereza.

Na kwa vile makanisa yako mengi, mtu akiona anakwazika kwa sababu muda walioamua kuwa na misa ya kiingereza ndio muda ambao angependa kusali basi anaweza kuhamia kanisa lingine la dhehebu hilo hilo ambalo halina misa za kiingereza.

Naamini viongozi wa kanisa hili wameona kuna waumini ambao wangependa kuabudu kwa lugha hiyo. Nao kama wachungaji wa Bwana hawawezi kuachia kondoo wao wapotee kwa kitu ambacho ambacho kiko ndani ya uwezo wao.

Amandla...
 

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,334
2,000
Nikuulize wanao wapo st kayumba au shule zinafundisha kiingilishi,

Kama ni zinazofundisha kiinglishi basi huna hoja!! Endelea kuabudu au hama kanisa!
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,924
2,000
... kama ibada ya Kiingereza inakukwaza, hudhuria za Kiswahili acha kulalamika. Baadhi ya makanisha ya kikatoliki walikuwa na utaratibu wa ibada za Kilatini siku za nyuma sina hakika siku hizi kuna makanisa bado yanazo...
Umejibu vizuri sana. Naongezea tu kuwa Kiingereza ni lugha ya taifa kama kiswahili. Ndio maana sheria zinaandikwa kwa lugha zote mbili.

Amandla...
 

The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,580
2,000
Dini ni utapeli kama utapeli mwingine.

Unajiuliza kwani ukiomba kwa kingereza ndio Mungu anaelewa zaidi kuliko ukiomba kwa kiswahili ama kisukuma?

Kwamba Mungu anaelewa zaidi kingereza ama kiarabu kuliko lugha nyingine yoyote hivyo maombi kwa kingereza ama kiarabu ndio yanamfikia mungu haraka ama anayaelewa kwa haraka kuliko ukiomba kinyambo?

Dini ni taasisi za kitapeli.
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,280
2,000
... kama ibada ya Kiingereza inakukwaza, hudhuria za Kiswahili acha kulalamika. Baadhi ya makanisha ya kikatoliki walikuwa na utaratibu wa ibada za Kilatini siku za nyuma sina hakika siku hizi kuna makanisa bado yanazo. Pia baadhi ya makanisa hususan ya mijini yana utaratibu wa baadhi ya ibada kuendeshwa kwa Kiingereza ili ku-accommodate wale wasiojua Kiswahili ni kawaida sana.

Huku kwetu masaini, KKKT huendesha baadhi ya ibada kwa Kimasai ili ku-accommodate wale wasiojua Kiswahili nayo ni kawaida sana tuache kulala
Tatizo wahitaji wa huduma hiyo ni wachache kwa hivyo wasilete usumbufu kwa kuipanga saa 4.00 muda kwa waomini wengi kwenda kuabudu siku ya jumapili.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,791
2,000
Wakati taifa lina lengo la kuimarisha matumizi ya lugha yetu kwenye nyanja zote ikiwa ni pamoja na elimu wapinzani wa taifa kujikomboa kwenye ukoloni wa lugha na utamaduni wa kigeni wanajibu mapigo kupitia makanisa...
Bwashee sali misa ya kwanza.

Binafsi naona wamechelewa sana kuanzisha hii misa ya kiinglishi.

Kanisani kwetu pale Anglican St Alban Huduma kwa lugha ya malkia ina zaidi ya miaka 100 sasa.........Ni misa ya pili.

Ya kwanza na ya tatu ni za kiswahili!
 

Joh Doe

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
395
1,000
Hahahaa hii ibada ipo Azania front na mimi ni mmoja wapo nasali hapo ila kuna mchungaji wetu alihamishiwa huko kutoka huku nafikiri labda ndiye aliyeenda kupeleka huko huu utaratibu. Kusudi kuu la hii ibada ni kuwapa nafasi waumini wa kigeni kushiriki ibada.

Kwa mf. waumini wengi wa Azania front ni wakazi wa Upanga, Oyster Bay, Masaki na Kinondoni maeneo haya kwa sehemu kubwa pia hukaliwa na wageni sana ambao kiswahili sio lugha wanayoimudu nahisi pia labda hata huko Mbezi walifanya ombi la kuwekwa hiyo ibada pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom