KKKT Mashariki na Pwani kuhakiki vyeti vya watumishi wake

Cicadulina

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
961
2,345
Malasusa_statement.jpg

SAKATA la vyeti feki, limetinga ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Akizungumza katika mkutano wa pamoja na watumishi wote, Kurasini jijini Dar es Salaam, Mchungaji Kadiva amesema, “uhakiki wa vyeti umelenga kulisafisha kanisa.”

Taarifa zinasema, tangazo hilo lililotolewa na naibu katibu mkuu wa dayosisi hiyo, liliwaudhi baadhi ya watumishi kwa madai kuwa limewalenga baadhi ya watu.

Hata hivyo, mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, suala la vyeti feki laweza kumkumba hadi mkuu wa dayosisi hiyo, Askofu Dk. Alex Malasusa.

“Hata mkuu wetu hawezi kubaki salama katika sakata hili. Naye

ni mmoja wa watuhumiwa wakuu katika sakata hili la vyeti feki. Anatuhumiwa hata kujipachika shahada ambazo hakuwahi kuzisomea,” anaeleza.

Amesema, “sisi huyu jamaa tunamjua tangu utoto wake. Alimaliza kidato cha nne na kushindwa mtihani, lakini hivi sasa anadai ana shahada ya pili (masters) kutoka chuo kikuu kimoja nchini Kenya.”

Alipoulizwa katibu mkuu wa Askofu Malasusa, Godfrey Nkini aligoma kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa ni mgeni katika nafasi hiyo na “silijui undani wake.”

Mtoa habari amesema, “huko nyuma mkuu wetu alitaka kutumia kigezo cha vyeti feki kuwafukuza wabaya wake, lakini sasa naye anatuhumiwa.”

“Kuna wachungaji walisimamishwa, wengine walizuiwa kuendelea na masomo na hata wengine kuacha kazi kwa kudaiwa walitumia vyeti feki kuingia katika uchungaji,” ameeleza mtoa taarifa.

Baadhi ya wachungaji waliosimamishwa na baadaye kurejeshwa kazini ni Paulo Lusambi, Leona Kimaro, Nkya, Mchome, Mbaga na Mgaya.

Aidha, imeelezwa kuwa yuko mwanamke mmoja aliyeruhusiwa na Askofu kwenda masomoni akiwa na cheti feki na kumaliza chuo, lakini Askofu aligoma kumbariki kwa kudai ana cheti feki.

Mtoa habari anasema, sababu ya cheti ilitumika kufunika sababu halisi ya Askofu kukataa kumbariki mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mwinjilisti mmoja kutoka Jimbo la Kusini ndani ya dayosisi hiyo alisimama na kufoka kuwa “wako wachungaji wengi waliobarikiwa na wana vyeti feki.”

Akahoji, “kwa nini sisi wainjilisti na parish workers tunaonewa na kuachwa wengine.”

Mwaka mmoja uliyopita, Askofu Malasusa aliitisha vyeti vya wachungaji kadhaa kwa madai kuwa vilikuwa vimeghushiwa.

Baada ya mjadala, baadhi waliomba radhi na kusamehewa lakini ilibainika wakati huo kuwa hata yeye alikuwa anatumia cheti bandia cha kidato cha nne na pia kujaza katika wasifu wake (CV) yake habari za uwongo kuwa alisoma Chuo Kikuu Katoliki nchini Kenya.

Hivi karibuni Askofu Malasusa amepeleka kundi la watu 40 kusomea uchungaji huko Mwika-Moshi, lakini Naibu Katibu Mkuu Mchg Bon Kombo alipolekeka vyeti baraza la mitihani, aliambiwa asilimia 80 ya vyeti hivyo ni feki na walitakiwa kurudishwa.

“Askofu Malasusa alimua wabaki huko na wasome programu maalum na kuwa atawabariki wakimaliza.”

Wachungunzi wa mambo katika dayosisi hiyo wanadai Askofu Malasusa baada ya kukabiliwa na tuhuma mbaya za maadili anaandaa jeshi la kumlinda kwa kupeleka watu wenye vyeti feki katika kazi ya uchungaji.

Taarifa zinasema, tuhuma pia kuwa ameanzisha vita na watu wanaotoka Kaskazini huku akiingiza watu wengi kutoka Mbeya katika mkakati wa kujilinda.

Chanzo: Mwananchi
 
Tatizo watumishi wa Mungu nao wamekuwa kama wanasiasa wa kutaka kumupendeza mh Magufuli badala ya Mungu.

Kazi ya kumtumikia Mungu ni wito siyo vyeti,kwa hiyo askofu amekuwa zaidi ya Mungu kama ana weza kumuzuia na kumufukuza mtumishi wa Mungu aliyeitwa kumutumikia Mungu kwa sababu ya makaratasi yaliyobuniwa na binadamu?.
 
Kanisa nalo lipeleke mambo kama siasa?hakuna MUNGU humo kwa staili hyo
 
impongo njoo huku uone hawa wenzako huku.....teteteteteeee hiyo inaitwa Pombe effect a.k.a Alcohol effect
 
Kanisa langu. TAASISI zimekuwa Sana. Watu wanabeza ETI wanadhani watumishi ni WA kwenye ibada tu.. TUMIA akili ndogo tu kwamba makanisa hasa hili ya kiluteri na Roman Catholic na Anglicans wanamiliki huduma nyingi shule magari wanayo. Kwa hio watumishi NAFASI kama hizo zinahitajika wenye Elimu pia. Kwa hiyo wale WA Ujanja yaani hewa hawakosekani. . Hata misikitini Kuna ipo inamiliki computer Sasa si lazima awe na CHETI.. Sioni tatizo labda Kwa Hao watumishi WA kiroho ambao nao wanahitaji kuwa na wito kuliko Elimu kubwa Sana
 
Kama kweli wanamtumikia Mungu huku wanavyeti feki ni hatari, maanake ni waongo mbele za Mungu. Uhakiki ufanyike tena haraka sana.
 
Watumishi wa Mungu wanatakiwa kuwa wasafi muda wote, kanisa linataratibu na kanuni zake. Wasiokizi vigezo waondoke tu.
 
Mimi najua uchungaji ni wito usipoingia kwa wito utapata shida
 
Malasusa_statement.jpg

SAKATA la vyeti feki, limetinga ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Akizungumza katika mkutano wa pamoja na watumishi wote, Kurasini jijini Dar es Salaam, Mchungaji Kadiva amesema, “uhakiki wa vyeti umelenga kulisafisha kanisa.”

Taarifa zinasema, tangazo hilo lililotolewa na naibu katibu mkuu wa dayosisi hiyo, liliwaudhi baadhi ya watumishi kwa madai kuwa limewalenga baadhi ya watu.

Hata hivyo, mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, suala la vyeti feki laweza kumkumba hadi mkuu wa dayosisi hiyo, Askofu Dk. Alex Malasusa.

“Hata mkuu wetu hawezi kubaki salama katika sakata hili. Naye

ni mmoja wa watuhumiwa wakuu katika sakata hili la vyeti feki. Anatuhumiwa hata kujipachika shahada ambazo hakuwahi kuzisomea,” anaeleza.

Amesema, “sisi huyu jamaa tunamjua tangu utoto wake. Alimaliza kidato cha nne na kushindwa mtihani, lakini hivi sasa anadai ana shahada ya pili (masters) kutoka chuo kikuu kimoja nchini Kenya.”

Alipoulizwa katibu mkuu wa Askofu Malasusa, Godfrey Nkini aligoma kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa ni mgeni katika nafasi hiyo na “silijui undani wake.”

Mtoa habari amesema, “huko nyuma mkuu wetu alitaka kutumia kigezo cha vyeti feki kuwafukuza wabaya wake, lakini sasa naye anatuhumiwa.”

“Kuna wachungaji walisimamishwa, wengine walizuiwa kuendelea na masomo na hata wengine kuacha kazi kwa kudaiwa walitumia vyeti feki kuingia katika uchungaji,” ameeleza mtoa taarifa.

Baadhi ya wachungaji waliosimamishwa na baadaye kurejeshwa kazini ni Paulo Lusambi, Leona Kimaro, Nkya, Mchome, Mbaga na Mgaya.

Aidha, imeelezwa kuwa yuko mwanamke mmoja aliyeruhusiwa na Askofu kwenda masomoni akiwa na cheti feki na kumaliza chuo, lakini Askofu aligoma kumbariki kwa kudai ana cheti feki.

Mtoa habari anasema, sababu ya cheti ilitumika kufunika sababu halisi ya Askofu kukataa kumbariki mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Mwinjilisti mmoja kutoka Jimbo la Kusini ndani ya dayosisi hiyo alisimama na kufoka kuwa “wako wachungaji wengi waliobarikiwa na wana vyeti feki.”

Akahoji, “kwa nini sisi wainjilisti na parish workers tunaonewa na kuachwa wengine.”

Mwaka mmoja uliyopita, Askofu Malasusa aliitisha vyeti vya wachungaji kadhaa kwa madai kuwa vilikuwa vimeghushiwa.

Baada ya mjadala, baadhi waliomba radhi na kusamehewa lakini ilibainika wakati huo kuwa hata yeye alikuwa anatumia cheti bandia cha kidato cha nne na pia kujaza katika wasifu wake (CV) yake habari za uwongo kuwa alisoma Chuo Kikuu Katoliki nchini Kenya.

Hivi karibuni Askofu Malasusa amepeleka kundi la watu 40 kusomea uchungaji huko Mwika-Moshi, lakini Naibu Katibu Mkuu Mchg Bon Kombo alipolekeka vyeti baraza la mitihani, aliambiwa asilimia 80 ya vyeti hivyo ni feki na walitakiwa kurudishwa.

“Askofu Malasusa alimua wabaki huko na wasome programu maalum na kuwa atawabariki wakimaliza.”

Wachungunzi wa mambo katika dayosisi hiyo wanadai Askofu Malasusa baada ya kukabiliwa na tuhuma mbaya za maadili anaandaa jeshi la kumlinda kwa kupeleka watu wenye vyeti feki katika kazi ya uchungaji.

Taarifa zinasema, tuhuma pia kuwa ameanzisha vita na watu wanaotoka Kaskazini huku akiingiza watu wengi kutoka Mbeya katika mkakati wa kujilinda.

Chanzo: Mwananchi
mtoa post hongera kwa kutuhabarisha inawezekana nawe umo kwenye kundi,ila naamini zamani shughuli za kanisa ilikua wito sio km nyinyi mnavyoweza kufanya,kuna maeneo kuna wachungaji waliishia darasa la nne na washarika wana amani na umoja na wengine wakati tunakua tulidhani uchungaji halipwi mshahara ila ni posho ya kumuwezesha kuchunga kondoo.
unapotaka kujenga mifumo lazima kuna wengine wataumia,km ww ni rais uliingia kwa mapinduzi ungependa wote waingie kwa mapinduzi ?km una ufahamu uongozi na una mitazamo imara utaandaa watu wenye uwezo.
dayosisi ya mashariki na pwani ni ya wote si ya watu wa kaskazin wala wa kusini,kihistoria tunapotaka kujua aliyeanzisha shughuli za iliyokuwa sinodi ya mashariki na pwani walianzia uzaramoni si kaskazini wala nyanda za juu,leo hii wa nyanda za juu na kaskazin mnapigana vikumbo hamuoni kuwa ni rahana hiyo?
unakumbuka mgogoro enzi za askofu jery mngwamba? kwa nini mnaturudisha tulipotoka?
shime wewe na baba askofu na wenzenu tumieni busara,mbona mzee sendoro aliwaongoza vema?je hamna vikao vya halmashauri na jimbo?hamuoni wenzenu waroma wanavyofanya mambo yao?mimi nimeona kijana mmoja katimuliwa mafunzo ya upadre miezi sita kabla ya kubarikiwa upadre akiwa na mastaz degree and he was the best student in his class just alilewa sifa na kuto heshim mamlaka!

kuna mambo ya msingi km kanisa kufanya
-mfano kwa nini miradi yenu hasa elimu na afya vinayumba?
-kuongeza miradi na vitega uchumi
-kuongeza mashauriano na mashirikiano na watu wa madhehebu na dini nyingine.
kuanzisha mashirika ya miito nk
-kuwa na watumishi wataalamu wa fani mbali mbali ili kudhibiti ubora wa huduma

yaani walutheran kadri wasomi wanavyoongezeka katika kanisa ndo migogoro inaanza kuongezeka

inawezekana askofu kaamua ila sio malasusa,askofu ni taasisi si mtu,unajua kwa nini kambariki huyu kamwacha yule dada?ulienda kuumuuliza ?je uliwasiliana na halmashauri ya kanisa?
askofu malasusa anaweza nae akawa na mapungufu yake km kibinadamu au kitaasisi kutokana na mianya iliyo kwenye katiba zao za kanisa,personal nilimfahamu akiwa ana shahada ya kwanza ya uchungaji km mika ishirini iliyopita alikua mtu ambaye hawezi kuchukua maamuzi kwa jambo ambalo hana uhakika na alikua mtu wa utaratibu na si msemaji mno na kwa wakati ule alikua mtu wa hekima.
kwa sasa anawezekana akawa mlevi mwizi nk maana binadamu wanabadilika but mnaopeleka watoto wenu uchungaji na huduma nyingiene km hizo alfu hawana wito au vigezo kwa kua hakuna ukaguzi na walafi wa madaraka wallah kanisa mtalibomoa na mtaanza kulaumiana .
hongereni waroma waamin na viongozi wa kiidini kwa kulea watu wenu kwa maadili, maaskofu wa kkkt inabidi muombe semina elekezi kwa wenzenu wa roma ili muanze kujenga kanisa upya muwaite akina berlin III na wengineo

samahani kam nimewakwaza
wasalaam
 
Waacheni viongozi wetu wa dini. Elimu yao sio ya DUNIA, inatoka juu. Jambo usilolijua litakusumbua bure. Katubu umrudie Bwana aliyewaweka katika viti hivyo !!

Back
Top Bottom