KKKT kuadhimisha miaka 500 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Ni katika maadhimisho ya miaka 500 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri. Waumini wote wa kanisa hili katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani(DMP),watakusanyika kufanya ibada ya pamoja pale uwanja wa Taifa kuanzia saa 2 asubuhi.

Itakuwa ni ibada ya kipekee ambapo maelfu ya watu wanatarajiwa kuhudhuria ibada hiyo ambayo itahudhuriwa pia na askofu wa DMP Dr. Malasusa.

Tutashuhudia kwaya zenye mamia ya watu wakiimba kwa pamoja kutoka katika kila jimbo.

Wote tukaribie.
Ina maana wakristo wa miaka kabla ya KKKT kuanzishwa hawatakwenda mbinguni?
 
Taifa la watu walionyimwa elimu, magazeti yao yanawaandikia pumba, na wenyewe hawajui wanalishwa upupu.

KKKT halijafikisha miaka 500.

KKKT halijaanzishwa na Martin Luther.

KKKT halifiki nje ya Tanzania kwa hiyo huwezi kusema KKKT linaungana na waumini wengine wa kanisa hilo duniani. WALUTHERI WA VIETNAM SIO WAUMINI WA KKKT.

Taarifa hii ingefaa kama ingehusu Kanisa Katoliki kwa sababu wakatoliki wote duniani ni kanisa moja chini ya figurehead mmoja, kwa sasa PAPA FRANSISCO!

MWANANCHI COMMUNICATIONS tangazeni kazi ya CHIEF MANAGING EDITOR nije niwasaidie, sio kila tamko la Askofu mnalimeza zima zima mnakuja kulitapika kama lilivyo! Aaaaah!

===========

Naona JF wamefuta taarifa ya MWANANCHI. Good job. That's a tremendous editorial work.

Watu ambao wanafanya kazi bure, mods wa JF, wanaandika edits kwa usahihi kuliko upupu wa ma professionals wa magazetini.
Namsikitikia atakayepiteza muda kubishana na wewe.
Kiufupi ni wazi kuwa wewe jamaa dish limeyumba.
 
Ina maana wakristo wa miaka kabla ya KKKT kuanzishwa hawatakwenda mbinguni?

1. Kabla ya KKKT, most likely hapakuwa na Wakristo Tanganyika.

2. Sina hakika kama KKKT ina umri wa miaka 500. Pengine tunamaanisha miaka 500 ya Lutheran Church, yaani ni miaka 500 iliyopita Martin Luther aliandika ile thesis yake kuasi Kanisa Catholic.

3. Historia inaonesha kanisa la kwanza kujengwa Mainland East Africa ni kanisa Catholic liko pale Bagamoyo. Na nafikiri lilijengwa in 1800s. Hivyo, Kanisa la Lutheran Tanzania haliwezi kuwa na umri wa miaka 500.
 
Ngoja wanaojua zaidi watujuze...
 
Basi iwe miaka 500 ya Ulutheri duniani
 
52f799d31f7893369e4fdf3b4fa4fb96.jpg
 
1. Kabla ya KKKT, most likely hapakuwa na Wakristo Tanganyika.

2. Sina hakika kama KKKT ina umri wa miaka 500. Pengine tunamaanisha miaka 500 ya Lutheran Church, yaani ni miaka 500 iliyopita Martin Luther aliandika ile thesis yake kuasi Kanisa Catholic.

3. Historia inaonesha kanisa la kwanza kujengwa Mainland East Africa ni kanisa Catholic liko pale Bagamoyo. Na nafikiri lilijengwa in 1800s. Hivyo, Kanisa la Lutheran Tanzania haliwezi kuwa na umri wa miaka 500.
Haya ni maadhimisho ya miaka 500 ya kuzaliwa kwa dhehebu au kanisa la Kilutheri duniani. Maadhimisho haya yamefanywa mwaka huu duniani kote ambako Lutheran ina nguvu kama vile Ujerumani kwenyewe, Denmark,Finland,Sweden n.k. Hapa Tanzania KKKT kama kanisa liliadhimisha mwezi uliopita ila Dayosisi ya Mashariki na Pwani imeadhimisha leo tukio linaloenda na Kipaimira kwa vijana wote wa Dayosisi nzima.

miaka 500 inatokana na hoja 95 za aliyekuwa Kasisi wa Kanis Katoliki kwenye kinachoitwa Reformation au Matengenezo ya Kanisa. Kw sababu hiyo Lutheran imetimiza miaka 500 kuanzia 1517 hadi 2017
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), linaungana na waumini wengine wa kanisa la Kilutheri duniani kuadhimisha miaka 500 tangu kufanyika kwa matengenezo ya kanisa hilo yaliyofanyika mwaka 1517 na Martin Luther nchini Ujerumani.

Maadhimisho hayo yanafanyika leo Jumapili Novemba 5,2017 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yakiambatana na ibada maalumu itakayoongozwa na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa.

Maandamano ya kuingia uwanjani yanaongozwa na kwaya ya matarumbeta.

Pamoja na waumini wengine, katika maandamano hayo wamo wanafunzi wa kipaimara 3,369 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Akizungumzia maadhimisho hayo hivi karibuni, Msaidizi wa Askofu, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza alisema ibada hiyo itakuwa ni kumbukumbu ya matengenezo ya kanisa ambayo ndiyo yanayoliongoza sasa.

Mchungaji Lwiza amesema ibada itashirikisha sharika 83 na mitaa 243 ikiwa ni maalumu ya kumshukuru Mungu kwa umri mrefu wa kanisa hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Tafuteni suluhu ya migogoro mbalimbali inayotokana na tamaa ya madaraka katika Kanisa,
 
Namsikitikia atakayepiteza muda kubishana na wewe.
Kiufupi ni wazi kuwa wewe jamaa dish limeyumba.

Unawa lecture watu wasibishane wakati we ndo kwanza kuja kubisha.

Daah, hili dunderhead sijui la wapi hili.
 
Kwanza Ladha ya KKKT imekufa kabisa..

Sermons na Homilies za Wachungaji wa KKKT hazina tofauti na Walokole
Kutoka vyombo vya kimataifa, Kanisa ambalo Martin alibandika ujumbe wake, lilikuwa na waumini wapatao sabini siku ambayo sherehe za kumbukumbu hiyo zilipofanyika Ujerumani. Na katika hali ya kushangaza karibu wote walikuwa wazee. Katika wakati tulio nao sasa vijana wako busy na matamasha ya miziki, matembezi mitandaoni, kubeti na mambo mengine kama hayo. Hakika hizi ni nyakati za majaribu sana, tumwombe Mungu awaoneshe njia ya kuongoka na kuachana na raha na starehe za kidunia.
 
...hivi kesi ya malasusa na yule mchungaji mke wa mtu iliishia wapi??

....Na kesi ya Askofu mkuu mstaafu dr. Erasto Kweka wa kkkt kaskazini na Taifa aliyekatakata Shamba la ndizi la mjane kule siha...

...Na deni aliloacha askofu laizer Kule Kkkt Arusha..kiasi cha waumini kuchangishwa michango tele....huyu Laizer pia alibariki kikombe cha Maji taka cha babu wa loliondo kilichopelekea maelfu ya wagonjwa kuacha dawa zao mahospitalini na kwenda kunywa uchafu ule na wengine hata kufa...

..nikipata majibu haya nitaanza kuingia kwenye makongamano yao kuwasikiliza...

...
 
Back
Top Bottom