KKKT Konde msimushambulie Mkuu wa Kanisa Dkt. Shoo

Tardy

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
1,287
1,604
Taarifa zinazosambaa mitandaoni kupitia Mwananchi digital zikionyesha baadhi ya wachungaji kumlaumu Mkuu wa Kanisa kushauri kiti cha uaskofu kurudi Tukuyu.

1. Enyi wachungaji mnajua maana ya KITI CHA UASKOFU?
2. Mnajua hicho kiti kilisimikwa wapi?
3. Mnaijua Katiba yenu?
4. Mnajua na kuelewa mamlaka na mipaka ya Mkuu wa kanisa?
5. Mnajua nakuelewa kati ya;
Mkuu wa kanisa na Askofu mkuu?

Wachungaji mnaomlaumu Mkuu wa kanisa mnamkosea sana. Ametimiza wajibu kama mkuu wa kanisa kwa Katiba ya Dayosisi ya Konde na Katiba ya KKKT.

Ushauri
1. Someni katiba zote mbili kwa umakini

2. Mkuu wa kanisa amewasaidia kuthibitisha kuwa kiti kilihamishwa kiimla

3. Mwenye mamlaka ya kumuondoa Mwaikali ni Katiba yenu na siyo mkuu wa kanisa

4.Wajumbe wa vikao vya maamuzi vya dayosisi ndivyo havijui wajibu wao. Wachungaji mnatakiwa kuwaondoa hao kwanza.

NB:
Malumbano hayatawasaidia

Utawala na Jiografia ya Dayosisi hiyo inahitaji kumegwa

Wachungaji mliokaa kumlaumu mkuu wa kanisa mmuombe radhi.

Umoja wakurudisha head office Tukuyu hampaswi kumbeza. Mmbeze aliyelazimisha kuhamisha usajili Kikanisa na kiserikali.
 
Kweli kitu kama hakikuhusu huwezi kukielewa, hapa nimetoka kapa kabisa.
Michungaji mizima inalichafua kanisa bila kujua katiba zao.Wanamlaum shahidi aliyesema ukweli wakuwalinda wao.Angekuwa ni Askofu mkuu alikuwa na mamlaka kupeleka hoja kwenye baraza la maaskofu ili Mwaikali ajadiliwe kukalia kiti au laa.
Kiti cha Askofu
Askofu ni vitu viwili tofauti.
Kiti ni mamlaka ya kitume
Askofu ni mtu.

Kilichotokea Konde Mtu aliamka akawatangazia wajumbe tunahamia Mbeya mjini.
Kiti cha Askofu kuhama ni
Kubadili mfumo wa katiba kwa kuridhia vikao halali,baraka kwa Mkuu wa kanisa ndipo kwa msajili serikalini.
K.K.K.T ndiye anayetambulika Nchini.
Mwaikali hakwenda moja kwa moja serikalini kuwaambia ninajipatia kiti cha uaskofu.
 
Itabidi kanisa katoliki tuandae semina ya jinsi ya kujiendesha kwa haya madhehebu uchwara,naona jinsi tutakavyopiga pesa hapa
 
Itabidi kanisa katoliki tuandae semina ya jinsi ya kujiendesha kwa haya madhehebu uchwara,naona jinsi tutakavyopiga pesa hapa
Ni ngumu sana.
Katoliki na Lutherani kiti cha uaskofu mamlaka yake ni tofauti.
Romani kiti cha Askofu kipo mikononi mwa Papa.
Lutherani kiti cha uaskofu kipo mikononi mwa wakristo chini ya uangalizi wa mkuu wa kanisa.

Semina hiyo haiwezi kukidhi.
Papa anamteua Ask na kumpanga.
Lutheran wanamchagua Ask kukalia kiti cha Dayosisi husika.Kiti cha wakristo makao makuu ya uaskofuni,akiondoka kiti kinabaki aje mwingine.
Kwanini migogoro ya Roman huisikii ni wakristo hawana mamlaka na Askofu
 
waache wafu wazike wafu wao sasahivi dini imekua sehemu ya kutafutia ulaji na umaarufu tu , ile ya imani na kupendana kuheshimiana na kusameheana hakuna ni pesa na madaraka kwa kwenda mbele, wapigane tu maana wana matumbo wala sio utashi na kuhudumia wananchi na waumini pia
 
Taarifa zinazosambaa mitandaoni kupitia Mwananchi digital zikionyesha baadhi ya wachungaji kumlaumu Mkuu wa Kanisa kushauri kiti cha uaskofu kurudi Tukuyu.

1. Enyi wachungaji mnajua maana ya KITI CHA UASKOFU?
2. Mnajua hicho kiti kilisimikwa wapi?
3. Mnaijua Katiba yenu?
4. Mnajua na kuelewa mamlaka na mipaka ya Mkuu wa kanisa?
5. Mnajua nakuelewa kati ya;
Mkuu wa kanisa na Askofu mkuu?

Wachungaji mnaomlaumu Mkuu wa kanisa mnamkosea sana. Ametimiza wajibu kama mkuu wa kanisa kwa Katiba ya Dayosisi ya Konde na Katiba ya KKKT.

Ushauri
1. Someni katiba zote mbili kwa umakini

2. Mkuu wa kanisa amewasaidia kuthibitisha kuwa kiti kilihamishwa kiimla

3. Mwenye mamlaka ya kumuondoa Mwaikali ni Katiba yenu na siyo mkuu wa kanisa

4.Wajumbe wa vikao vya maamuzi vya dayosisi ndivyo havijui wajibu wao. Wachungaji mnatakiwa kuwaondoa hao kwanza.

NB:
Malumbano hayatawasaidia

Utawala na Jiografia ya Dayosisi hiyo inahitaji kumegwa

Wachungaji mliokaa kumlaumu mkuu wa kanisa mmuombe radhi.

Umoja wakurudisha head office Tukuyu hampaswi kumbeza. Mmbeze aliyelazimisha kuhamisha usajili Kikanisa na kiserikali.
Ifike wakati sasa Dayosisi ya Konde wajitambue, why wao tu kila siku na migogoro
Tunajua hao maaskofu hawako hapo kwa ajili ya roho za watu, wako hapo kwa ajili ya matumbo yao tu
 
Umeongea kiroho na kiakili/kisheria.

Mwenye masikio na asikie.

KATIBA IHESHIMIWE.
 
Itabidi kanisa katoliki tuandae semina ya jinsi ya kujiendesha kwa haya madhehebu uchwara,naona jinsi tutakavyopiga pesa hapa
Unazungumzia hao wapadiri wanaosema hawaoi ila wanalawiti watoto!?? Au wapi!??
 
Back
Top Bottom