KKKT haya mahubiri ya Upendo Tv kuhusu siasa ni msimamo wa kanisa au wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani?

Kimaro ni muhubiri mzuri...nimeshamsikiliza mara kadhaa...kama atapitia bandiko hili ninamshauri na kumuomba....apunguze kwenye mahubiri yake kutaja mambo ya makabila, na siasa...itamsaidia sana kuboresha mahubiri yake....kuna waumimi wake tukimsikiliza akianza kutamba kuhusu ...sijui kabila fulani au
sijui mwanasiasa fulani masikio yanawasha...Afuate mfano wa Mwakasege.....ikitokea akagusia siasa katika mahubiri yake haoneshi upande...anasimama katika neno..(rejea mahubiri yake ya neneo:ili ufanikiwe maombi pekee hayatoshi)...akigusia makabila hataji jina la kabila...au kusema anatoka wapi....
Mungu azidi kumpa hekima mchungaji Eliona Kimaro...
Huwa namshangaa sana huyu jamaa hata katika mahubiri yake utakuta unaongea kirugha(kichaga).

Kimaro ni mzuri sana ila tabia yake ya kuabudu ukabila ina kera sana.
 
KKKT lazima ijue kuwa serikali zina nguvu kubwa na mbinu nyingi, ikitaka kuingia katika taasisi yeyote iliyo huru na yenye nguvu wanatumia watu wa ndani ya taasisi hiyohiyo.
Nilipoona majuzi mahubiri ya Mchungaji wa Kijitonyama yanapewa Airtime ya kutosha na page ya Msigwa wa Ikulu nilijua tayari KKKT imeingiliwa.
Nadhani KKKT ni zaidi ya hapo, watachukua hatua haraka isipotezwe na wachache wanaotumika.
Nenda kashtaki kwa Askofu Shoo!

Alafu msiwe mazwazwa, hivi Munga zile Makala zake nazo huwa mnazitolea maoni kama haya?

Pendeni kusikia hata msiyo penda kusikia
 
Siku hizi kuna ujinga wa kulitafsiri neno la Mungu. Watu wanatumia biblia ili kukamilisha matakwa yao ya kishetani.

Wanatenda uovu, wakikosolewa wanasema Mungu amesema, 'tiini mamlaka'. Upumbavu mkubwa wa uelewa wa neno la Mungu.

Mamlaka ikiua, ni sawa. Ikionea watu ni sawa. Ukiwanyima watu haki ni sawa. Kama ni hivyo, kwa nini tuliwaondoa wakoloni? Serikali ya wakoloni haikuwa mamlaka? Kwa nini hatukuitii?

Na wale manabii lukuku waliowashambulia wafalme waovu kwa kauli kali, walienda kinyume cha neno la Mungu? Au ni ujinga wa kutofahamu tofauti ya kutii na kukosoa? Kutii na kuonya?

Someni biblia vizuri na kuelewa content badala ya kusoma kamstari kamoja na kusimamia hapo.

Wale wakunga waliamriwa na Farao kuua watoto wa kiume wa kiyahudi, neno linasema, walimwogopa Mungu, wakaigomea mamlaka, na Mungu akawabariki.

Shedrack na wenzake walimgomea mfalme Nabukaneza. Na Mungu akawabariki, na kuwaokoa na kifo.

Daniel alimgomea mfalme Darius. Mungu akamlinda Daniel dhidi ya uaji uliopangwa na Darius.

Katika Agano Jipya (Mdo4:19), Petro na Yohana waliigomea mamlaka. Na tena walinena mbele ya mamlaka kuwa, 'inatupasa kumsikiliza Mungu kuliko kitu kingine chochote'

Mktadha wa Paulo juu ya Submission to Authority ni pale mamlaka hiyo inapotenda haki, inapoendana na mafundisho ya Mungu. Lakini siyo inapokwenda kinyime cha maagizo ya Mungu.

Mungu amesema, usiue, mamlaka inasema ua. Ni lazima usimame na kusema hapana. Kwa sababu inanipasa kumtii Mungu zaidi aliyesema siruhusiwi kuua kuliko mwanadamu.

Kabla hujatii mamlaka, ujiulize kama mamlaka hiyo imetoka kwa Mungu. Alama ya mamlaka iliyotoka kwa Mungu ni matendo yanayofanywa na hiyo mamlaka kuendana na maagizo ya Mungu. Kinyume chake ni kwamba mamlaka hiyo imetoka kwa shetani. Hatutakiwi kumtii au kumkubalia shetani. Tuliapa kumkataa. Kutii mamlaka ya shetani ni kukubali kuwa sisi wote ni wafuasi wa shetani.

Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Umemaliza Mkuu
 
Yamemdhalilisha Kimaro sio Kkkt Mimi ni mkkkt ila sikubaliani na huo ujinga
Mkuu SI ametumia jukwaa laKKKT,wasipokanusha kuwa huo sio msimamo wa Kanisa hatutawaelewa!
Na Hali ilivyo nchini sidhani Kama Hilo limetokea bahati mbaya!
muda utaongea!
 
Huwa namshangaa sana huyu jamaa hata katika mahubiri yake utakuta unaongea kirugha(kichaga).

Kimaro ni mzuri sana ila tabia yake ya kuabudu ukabila ina kera sana.
Sawa mkuu...ila tumuombe sasa...aachane na hayo mapungufu....ajue ana wafuasi wengi na uwezo wa kuhubiri i ni mzuri....sina shaka na ila...ila baba mchungaji achana na kuzungumza ukabila na siasa kwenye mahubiri yako..Kumbuka: Mtu anayekupenda daima atakwambia ukweli hata kama ni mchungu
 
Huwa namshangaa sana huyu jamaa hata katika mahubiri yake utakuta unaongea kirugha(kichaga).

Kimaro ni mzuri sana ila tabia yake ya kuabudu ukabila ina kera sana.
Labda wachaga ndo wanatoa sadaka nono nono, ngoja na sisi wakara tutafute mchungaji wetu atusifie kuvua samaki, twende kazi...
 
Askofu wake siyule aliyeongoza kwa awamu mbili kwenye hiyo dayosisi akarudi tena kugombea kipindi kingine?malasusa ni askofu ambae sikuwahi kuvutiwa nae kabisa katika uongozi wake nimamluki wa ccm
niliacha kuangalia Upendo TV zamani sana kwa sababu ya "uduli" wa Kimaro na kujikombakomba kwake kwa wenye mamlaka.

in fact, Dayosisi ya Mashariki & Pwani watumishi wake majority ni wachumia tumbo (kuanzia kule chini hadi pale juu).
 
Mkuu SI ametumia jukwaa laKKKT,wasipokanusha kuwa huo sio msimamo wa Kanisa hatutawaelewa!
Na Hali ilivyo nchini sidhani Kama Hilo limetokea bahati mbaya!
muda utaongea!
Tatizo la Dayosisi hii mkuu kabisa yuko kwapani mwa dab
 
Askofu wa kweli alikuwa SENDORO tu!
Askofu wake siyule aliyeongoza kwa awamu mbili kwenye hiyo dayosisi akarudi tena kugombea kipindi kingine?malasusa ni askofu ambae sikuwahi kuvutiwa nae kabisa katika uongozi wake nimamluki wa ccm
 
Sina budi kumshukuru Mungu kwa kile kidogo ulichochangishana, leo Tuna TV ya kanisa inayomhubiri Kristo ktk maeneo mengi ya Tz na Duniani!

Bila kuwa mnafiki nimeshtushwa na mienendo ya mahubiri yanayorushwa live pale yanapogusia SIASA!

Iliianza Jumapili iliyopita Mch.Masai alipowalaani wote, aliwaita wachache wanaompinga Rais Magufuli.

Leo ibada ya jioni Mch wa Kijitonyama ameliambia Taifa, kuwa Kuna kabila moja tu lenye roho ya maendeleo nalo ni wachaga!...na kwa kuwa Rais Magufuli analeta maendeleo Basi yeye ni damudamu na Wachaga...na ile minong’ono kuwa JPManawsbagua Wachaga SI kweli!

Ameendelea kubainisha kuwa Wachaga hawapendi SIASA na ukiona Mchaga yupo kwenye Siasa huyo anazuga!?

Jana asubuhi ktk mahubiri yake alisema kuwa Kanisa lilifunga ili Tz ipate Rais mpenda haki na Mungu alijibu maombi ya Kanisa!

Akahitimisha kuwa wanaolia maisha magumu ni wale waliokuws wanaishi kwa wizi!

Nimejiuluza maswali mengi Sana:
Je, Kama KKKT wanajua ibada hizo zinaonekana nchi nzima, wamekubali pia maudhui ya Hawa wachungaji yaenee nchi nzima?!

Je, huu ni MSIMAMO wa Kanisa, DAYOSISI ya MASHARIKI au ni mawazo yao Hawa ndugu!

Kama Kanisa mnawaweka fungu gani waumini wenu?

Mch Kimaro anaposema tukiwaona Wachaga kwenye Siasa tujue wanazuga, wanazuga ili iweje? Wanatafuta Nini kwenye hayo aliyoita MAIGIZO!!?

USHAURI WA BURE:
KKKT KUWENI MAKINI NA MASUALA HAYA MNAYOONANI MADOGO.

..KAMA MCH. KIMARO NA MATSAI NDIO MNAONA WANAIBRAND KIROHO KKKT, BASI WAFUNGENI GAVANA YA KIBURI

...HIVI NI LAZIMA KUWAPA AIRTIME KIJITONYAMA PEKEE KWENYE MAHUBIRI, MBONA KUNA WACHUNGAJI WENGI WANAOJUA KUHIBIRI NA KUFUNDISHA?

...JITAHIDINI MSITENGENEZE MANABII NA MITUME NDANI YA KKKT MTAJUTA!
KWA TAARIFA YENU

...TULIOCHANGIA UPENDOTV.
...Ndio sisi ndugu na jamaa wa akina Tundu Lissu, Ben Saanane na wengine!

..ni sisi watumishi wa serikali ambao hatujapandishiwa mishahara kwa miaka minne,

...NI sisi ambao tunamkosoa Rais tunapoona anatenda ndivyo sio '!

...Sisi mliotufundisha haki huinua Taifa.

SAMAHANI KWA UANDISHI, NINA JAKA MOYO LA KIROHO!
ASANTE SANA NDUGU, BARIKIWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA DAUDI, siku hizi makanisani mengi ni biashara tu, hakuna kuhubiri yesu kristo,lakini mwisho wao waja, je inawezekana mtu aliye na akili kamili au timamu awe mkristo, muislam au hata awe hana dini anayeweza kumusifu magufuli? angalia ile unyama na ukatili na kuharibu taifa huyu raisi wa wanyonge ametenda, siwezi ombea binadamu wenzangu mabaya lakini huyu jiwe mungu MUONDOE TOKA MADARAKANI, na mungu saidia watumishi wako wanaohubili neno lako bila uoga
 
Sasa hivi ni sawa ukimsifia Magufuli na ccm yake hata kama unaenda nje ya maadili ya kazi yako. Kosa ni pale utakapowasifia wapinzani na kuipa changamoto ccm na serikali.
Hawa wanaoitwa wachungaji ukifuatilia wengi wao utagundua ni makanjakanja wa kiroho.
 
ASANTE SANA NDUGU, BARIKIWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA DAUDI, siku hizi makanisani mengi ni biashara tu, hakuna kuhubiri yesu kristo,lakini mwisho wao waja, je inawezekana mtu aliye na akili kamili au timamu awe mkristo, muislam au hata awe hana dini anayeweza kumusifu magufuli? angalia ile unyama na ukatili na kuharibu taifa huyu raisi wa wanyonge ametenda, siwezi ombea binadamu wenzangu mabaya lakini huyu jiwe mungu MUONDOE TOKA MADARAKANI, na mungu saidia watumishi wako wanaohubili neno lako bila uoga
AMEN, SALA YAKO IMEFIKA.
WAMEKULA RAMBIRAMBI HUKO KAGERA, WAMEKULA HEL ZA MAFAO NSSSF, WAMEVUNJA NYUMBA KIMARA BILA FIDIA ILA MWANZA KASEMA WALIPWE NA WAMELIPWA,
WAlio vamia maeneo kuona ni wasukuma yale mapori kasema watu waishi humo, ila ingekuwa mchaga wangepata kipigo cha mbwa koko kama muruto asemavyo
 
Kimaro ni muhubiri mzuri...nimeshamsikiliza mara kadhaa...kama atapitia bandiko hili ninamshauri na kumuomba....apunguze kwenye mahubiri yake kutaja mambo ya makabila, na siasa...itamsaidia sana kuboresha mahubiri yake....kuna waumimi wake tukimsikiliza akianza kutamba kuhusu ...sijui kabila fulani au
sijui mwanasiasa fulani masikio yanawasha...Afuate mfano wa Mwakasege.....ikitokea akagusia siasa katika mahubiri yake haoneshi upande...anasimama katika neno..(rejea mahubiri yake ya neneo:ili ufanikiwe maombi pekee hayatoshi)...akigusia makabila hataji jina la kabila...au kusema anatoka wapi....
Mungu azidi kumpa hekima mchungaji Eliona Kimaro...
Kimaro msanii tu kama wengine.
 
Back
Top Bottom