muzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2016
- 1,038
- 1,448
Siku zote MWANAMKE hawezi kumpata Mwanaume aliye mkamilifu maana tupo aina tofauti tofauti.
- Ukimpata Handsome_Kichwa chake ni empty.
- Ukimpata Genius_Yuko serious masaa 24 na wengi huwa hawako romantic, hawajipendi kihiivyo, wako rafu mno.
- Ukimpata Tajiri_ Hawezi kukuheshimu full madharau, utamwambia nini wakati hela anayo bana.
- Ukimpata Mfanyakazi hodari_ Hana muda wa kuwa karibu na wewe, muda wote anawaza kazi na kutafuta maisha/pesa.
- Ukimpata mnyenyekevu_ Mfukoni huwa ni 0% au salio halisomi
- Ukimpata anayekupenda kwa dhati_ Anakuwa siyo type yako, yaani hana sifa unazozitaka, au hana muonekano ule unaoutaka wewe.
- Ukimpata msomi_ Hasikilizi ushauri wako anakuona boya tu, huna point za maana mbele yake.
- Ukimpata yule Smart_ Ni muongo kupita kiasi na play boy.