Kizungumkuti cha mtu akifa anaenda wapi? Maoni ya watu na imani mbalimbali duniani

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Kifo fumbo ambalo ni kutokuwa na majibu ya haraka sahihi na kwa sababu hawa jamaa hawarudi na hata kama wakirudi hatuwaamini.

1:Wahindu (hinduism)
Hakuna cha mbingu wala jehanam, Mtu akifa anarudi kwenye maisha haya kama kitu au kiumbe kingine.

2:Uislam
Quran 45:26. Sema: Mwenyezi Mungu anakuhuisheni, kisha anakufisheni, kisha anakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.
hapa inaonekena Hata ufeje, mwili utakusanywa na kutakiwa kusimama mbele ya hukumu. wataalam wanaweza kutupa maarifa zaidi.

3:Wabudha
Hawa wanaamini Ukifa mwili utaoza lkn akili/mind itaendelea kuwepo. Na pia kuna kuzaliwa upya baada ya kifo.

4:Wayahudi/Judaism
Nafsi inaishi milele, mwili ni kama kasha ambalo limeazimwa roho likifa linaoza roho inaendelea kula maisha.pamoja na hili wanamaelezo ya ziada.

5:Wakristo
Hapa wamegawanyika makundi mawili.
wale wanaoamini Mtu akifa roho yake haifi, inaenda kula raha mbinguni, au kama ni ovu inateswa motoni. Pia wapo wanaoamini na mimi nikiwemo mtu akifa ni kaubirini analala usingizi mzuri wa mauti kusubiri hukumu ya haki siku ya kiyama. haendi popote.

6:Mababu zetu na Wababe wakiafrika wanasemaje.
Kifo sio mwisho wa maisha, bali ni mwendelezo wa maisha kwa mfumo tofauti ambao hauna mwili. Kwa baadhi ya mila Kifo ni sherehe maana jamaa anakuwa amehamishiwa katika maisha mengine ambayo ni bora zaidi.

8:Wanasayansi na wasiamini Mungu na Miungu
Hapa nao wanamaoni mengi, ila athiest na mwanasayansi nguli aliyefariki majuzi Stephen Hawking anasema Ubongo ni kama Kompyuta kuna wakati Unachoka unaacha kufanya kazi na kufa. Hakuna chochote mtu akifa, zaidi hakuna cha mbingu wala kiyama wala moto. Hizo ni hadithi za watu Wanaoogopa giza.



vipi wewe unaamini lipi.
 
Hapa ni kila mmoja kuamini na kuenenda kadri ya anayoona inafaa na imani yake inavyomuongoza.

Kati ya hayo yote uliyoyataja hapo juu, hauwezi kusema kipi ni sahihi na kipi sio sahihi, inategemea na mhusika uko upande gani.

Kwa upande wangu, sijui mwili au roho kupi kitabaki au kuelekea wapi, ila jambo moja nna imani nalo na nna hakika nalo, ntawajibika kwa maisha niliyoishi hapa duniani, iwe kwa uovu au kwa wema.
 
binafsi naamini na kuunga mkono hoja ya bwana hawking sambamba na dawkins(athists pia).ubongo pekee ndio huweza kufa mtu huwa hafi na ndio maana kuna tofauti kati ya kufa na kufariki.kwani ukisoma vitabu vinatuelekeza yakuwa ubongo unaratibu matendo na matukio yote ya mwili either ya hiari au ya lazima.kwa hiyo mimi kama implicity ethists namuunga mkono comrade hawkings hasa katika "a brief history of time from bing bang to dark holes"
salute!
 
Hata sasa injili inahubiriwa kwa mataifa yote.

Siku ya kutisha inakuja ambayo watu wote watasimama kutoa hesabu ya matendo yao, ikiwa yalikuwa mema wataingia rahani kwa Mungu na kuurithi ufalme wa Mungu, ikiwa ni maovu watatupwa katika jehanamu ya moto na kiberiti.

Toka kuumbwa kwa ulimwengu watu wote waliowahi kufa wako katika sehemu ya mangojeo wakisubiri siku ya hukumu. Kama ni mwema yuko paradiso anangojea hukumu (refer Lazaro), kama alikuwa mwovu yuko kuzimu anasubiri hukumu (refer tajiri akimuomba maji Lazaro).

Uamuzi ni wako ndugu, mwamini YESU UOKOKE na utende mema, ukiingojea siku ya mwisho. Kama itatokea umekufa haijaja sio mbaya maana utaungana na either ya hayo makundi mawili hapo juu.

Be blessed, Yesu ndio njia kweli na Uzima.
 
Hapa ni kila mmoja kuamini na kuenenda kadri ya anayoona inafaa na imani yake inavyomuongoza.

Kati ya hayo yote uliyoyataja hapo juu, hauwezi kusema kipi ni sahihi na kipi sio sahihi, inategemea na mhusika uko upande gani.

Kwa upande wangu, sijui mwili au roho kupi kitabaki au kuelekea wapi, ila jambo moja nna imani nalo na nna hakika nalo, ntawajibika kwa maisha niliyoishi hapa duniani, iwe kwa uovu au kwa wema.
Namna pekee ya kuwajibika kulingana na maisha yako ni legacy utakayoiacha. Basi
 
Angalao ninamuunga mkono Stephen Hawking. Mtu akifa, haendi popote.

Gari (mashine) linapofanya kazi vizuri, huo ndio uhai wake. Linaposhindwa kufanya kazi milele, linakuwa limekosa uhai. Halifanyi tena kazi iliyokusudiwa. Linatumika kama skrepa hadi linaisha kabisa. Hali ya gari kufanya kazi (roho) itakuwa imeenda wapi?

Roho za wanyama wengine na viumbe hai wengine ukiondoa binadamu zinaenda wapi? Viumbe hawa wana "destination" gani baada ya kufa? Angalao maandiko yanasemaje kuhusu viumbe hawa wasio wanadamu? Mwenye majibu, tafadhali anisaidie.

Je, tunaweza kufanisha kifo cha "gari" na mwisho wake na kifo cha binadamu na mwisho wake?.

Kwa maoni yangu, kifo ni hali ya kiumbe hai kushindwa kuendelea kujimudu milele. Kujimudu kwa maana ya kwamba mifumo ya mwili inafanya kazi kwa ushirikiano na kwa utimamu. Huu ndio uhai.

Kwa hiyo, kuna hali mbili. Kuwepo na kutokuwepo.

Kuwepo ni mchakato. Kuanzia kutungwa kwa mimba hadi kuzaliwa na kuendelea kuishi.

Kutokuwepo nao ni mchakato ambao unaanza na kiumbe kushindwa kujimudu milele. Hii unaweza kusema ni hali ya kiumbe kupoteza uhai. Kinachofuata ni kumalizika kwa kuwepo ambapo mwili unaoza na kuisha kabisa.

Kwa hiyo, kwa maelezo hapo juu, mwili na roho havitenganishwi. Kwanza hakuna kitu roho. Kuna hali ya kiumbe hai kujimudu. Gani kujiendesha kiutimamu kwa kadiri ya mifumo ya kiumbe hai inavyofanya kazi. Kufanya kasi kiutimamu "in a coordinated fashion" ndiko huko kunakotafsiriwa kama roho. Ila, kimsingi, hakuna kitu roho.

Utimamu wa utendaji wa mifumo ya kiumbe (hai-mfumo wa damu, chakula, n.k pamoja na ogani zoye, viumbe visivyo hai-gari-injini kufanya kazi vizuri, jiwe kuendelea kuwa jiwe, mbao kuendelea kuwa mbao n.k) ndiko kunakosabisha kuwepo kwa hiki tunachokiitaa mwili.

Kukosekana milele kwa utendaji timamu wa mifumo, ndicho kifo. Madhara ya ukosefu wa utimamu wa utendaji hupelekea mwili kuharibika na kisha kupotea kabisa.

Hii inamaanisha kuwa so rahisi kutenganisha hicho kinachoitwa roho na mwili. Hakuna kitu roho wala mwili, bali kuna kuishi au kutokuishi. Kuwepo au kutokuwepo.

Tunachokiona kama mwili ni mchakato wa kutokuwepo tu. Haimaanishi kuwepo kwa kitu mwili bado kuna uwepo.

Kwa hiyo, hakuna kinachoenda popote. Upon au haupo. Basi kama jinsi ambavyo ambaye hayupo, hajawahi kuwepo na hatokaa awepo had I atakapokuwepo.

Unakumbuka uzi wa "Usipokuwepo, hakuna Kilichopo"?. Yani, wewe ndio mwanzo na mwisho wa kila kitu. Hats Mungu hawezi kuwepo bila ya kuwepo wako.

Hata kifo, hakipo bila wewe kuwepo. Usipokuwepo (ukifa au hujazaliwa), hakuna ambacho kipo, na hakuna ambacho kitakaa kuwepo.

Lazima kuwepo kwanza ili kila kitu kingine kuwepo.

Kwenda mbinguni, Motoni, peponi n.k ni hadithi zinazofifisha uwezo wa binadamu. Ni utumwa mkubwa sana.
 
binafsi naamini na kuunga mkono hoja ya bwana hawking sambamba na dawkins(athists pia).ubongo pekee ndio huweza kufa mtu huwa hafi na ndio maana kuna tofauti kati ya kufa na kufariki.kwani ukisoma vitabu vinatuelekeza yakuwa ubongo unaratibu matendo na matukio yote ya mwili either ya hiari au ya lazima.kwa hiyo mimi kama implicity ethists namuunga mkono comrade hawkings hasa katika "a brief history of time from bing bang to dark holes"
salute!
Umetaja majina mawili na vitabu.

Unaweza kutoa nukuu za moja kwa moja kuonesha kuelimisha zaidi na kuonesha kwamba watu hao walisema hivyo, na si wewe tu uliyekosea kuwaelewa?

Hao ni waandishi wawili ninaowafuatilia sana, "A Brief History of Time" cha Hawkings nimekisoma kama miaka 25 iliyopita na nakirudia sana. "The God Delusion" cha Dawkins nimekisoma miaka 12 iliyopita.

Katika maandishi, documentaries, commentaries etc za kuhusiana na habari za Hawking na Dawkins nilizopitia - ni nyingi sana- sijawahi kusikia wanahusishwa na habari za wao kusema ubongo pekee ndio unakufa, mtu hafi.

Mtu bila ubongo ni nini? Unaweza kutoa nukuu za moja kwa moja?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom