Kizimbani kwa kutishia kuua kwa njia ya Ujumbe wa Barua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizimbani kwa kutishia kuua kwa njia ya Ujumbe wa Barua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  KIJANA Seifu Nassoro [24] mkazi wa Mikocheni amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za kutishia kuua kwa njia ya ujumbe wa barua. Mshitakiwa huyo amefikishwa Mahakamani hapo mbele ya hakimu Lina Msanga wakati upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka Nassoro Sisiwaya wa Mahakama hiyo.

  Sisiwaya alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo la kutishia kuua Agosti 26 mwaka huu, huko akiwa maeneo ya Mikocheni ‘A’ jijini Dar es Salaam.

  Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitishia kumuua mlalamikaji Mohamed Nassoro kwa njia ya kuandika ujumbe wa barua wa vitisho.

  Sisiwaya alidai kuwa maneno yaliyokuwa katika barua hiyo ya vitisho juu ya mlalamikaji yalikuwa ni
  “ Ukae tayari kwa mashumbilizi ya hali ya juu ambayo yanaweza yakakusababishia upoteze maisha yako na kupoteza mali zako unazoringia kama hiyo nyumba yako na magari”.

  Hatahivyo mshitakiwa alipotakiwa kujibu tuhuma hizo alikana kuhusika kwa namna moja wala nyingine kushiriki kuandika ujumbe huo dhidi ya mlalamikaji.

  Alitakiwa kutojielezea zaidi mahakamani hapo hadi hapo siku ya kusikiliza kesi hiyo itakapofika.

  Hakimu alitaka ushahidi wa ujumbe huo uletwe mahakamani na upepelezi wa kina bado unaendelea dhidi ya tuhuma hizo kwa mshitakiwa.

  Mshitakiwa alipewa dhamana na kesi hiyo iliahirishwa hadi hapo Septemba 15, mwaka huu itakapotajwa tena.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3022142&&Cat=1
   
Loading...