Kizimbani kwa kumwagia mtoto maji moto

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Dar es Salaam. Mkazi wa Kigamboni, Prisca Msame (34) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na shitaka la kujeruhi kwa kumwagia maji moto mtoto wa miaka 16.

Msame anadaiwa kumjeruhi mtoto wa miaka 16 kwa kumwagia maji ya moto sehemu ya mgongoni na hivyo kumsababishia majeraha.

Mwanamke huyo alifikishwa katika mahakama hiyo na kusomewa shtaka linalomkabili.

Akisoma hati ya Mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Wilberforce Luhwago, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Erick Shija alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 6, 2017 eneo la feri wilaya ya Ilala.

Shija alidai siku hiyo ya tukio katika eneo la Feri, mshtakiwa alimwangia maji ya moto mlalamikaji Alfonce Maiko mwenye umri wa miaka 16 sehemu ya mgongoni na kumsababishia maumivu.

Chanzo: Mwananchi
 
Hizi roho tulizo nazo binadamu wakati mwingine ni zaidi ya tunavyo zijua kwa matendo ya kinyama,

Pole dogo
 
Back
Top Bottom