Kizimbani kwa kujifanya wake wa Waziri wa Elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizimbani kwa kujifanya wake wa Waziri wa Elimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Kizimbani kwa kujifanya wake wa Waziri wa Elimu


  Saturday, April 18, 2009 10:06 AM
  WANAWAKE wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la udanganyifu kwa kujifanya ni wake wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe
  Washitakiwa hao ni Hanifa Kassim Kawambwa [30] mkazi wa Temeke Mikoroshini na Hawa Aladita Sharif [30] mkazi wa Mbagala Chemchem.

  Wanawake hao walifikishwa Mahakamani hapo jana kujibu mashitaka yanayowakabili wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  Walisomewa mashitaka yao na Mwendesha Mashitaka Inspekta Msaidizi wa Polisi Denis Mujumba mbele ya Hakimu Janeth Kinyage wa Mahakama hiyo.

  Mujumba alidai kuwa katika shitaka la kwanza, washitakiwa wote kwa pamoja mapema mwaka huu, walikula njama ya kujipatia kiasi cha shilingi 6,600,000 kutoka kwa Kiramuu Petro Mbowe.

  Katika shitaka la pili imedaiwa kuwa Machi 27, mwaka huu, katika Benki ya Access iliyopo Temeke washitakiwa hao walijipatia Sh. 3,000,000 kutoka kwa Kiramuu Petro Mbowe kupitia akaunti iliyokuwa na namba 0221100609319.

  Washitakiwa hao waliweza kujipatia fedha hizo baada ya kujitambulisha kuwa wao ni wake wa Waziri wa Elimu wa Tanzania Prof. Maghembe.

  Washitakiwa walikana mashitaka hayo na kudai kuwa si kweli na waliweza kuwa nje kwa dhamana,.

  Hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi hapo Mei 21, mwaka huu, itakapotajwa tena Mahakamani hapo.


  Na Chondoma Shabani, Dar es salaam

  Mtumie Rafiki Yako
   
Loading...