Kizimbani kwa kosa la kuhujumu uchumi

Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
563
433
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Benhadard Tito na wenzake wawili wamepadishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo wawili wa RAHCO na mfanyabiashara wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kusababisha hasara ya dola za Marekani 527,540.

Mbali na Tito, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria wa RAHCO, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.
 
Aisee nchi ilikuwa imeoza, haya ndiyo mambo tunategemea Serikali ya viwanda iyafanye sio kushinda mahakamani kila siku kupambana na wakosoaji au wapinzani na kuishia kupigwa Kata funua na Lissu
 
Nilisoma mahala hizi tuhuma pia kwenye hili swala

*Majipu Rahco*

Katika hatua nyingine, PPRA imebaini madudu katika zabuni ya kuboresha Reli ya Kati iliyofanywa na kampuni ya Rahco, ambayo haikuwa katika mpango wa manunuzi kwa mwaka 2014/2015.
Mamlaka hiyo inadai mkurugenzi mkuu wa Rahco alijitwalia madaraka yote ya kuwa mamlaka ya uidhinishaji wa bajeti na yale ya bodi ya zabuni na kuidhinisha matumizi ya fedha. Meneja mkuu wa manunuzi wa Rahco, alitoa ushauri sahihi kwa mkurugenzi huyo mwendeshaji lakini ushauri wake haukuzingatiwa na matokeo yake alibanwa na mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bodi ya zabuni ya Rahco haikushirikishwa kabisa katika mchakato huo wa zabuni ambapo kampuni ya CRCC and Integreted Communication zilipewa zabuni.

Jukumu la kuita wazabuni na kuwapa zabuni hiyo lilifanywa na mkurugenzi mwendeshaji wa Rahco pekee bila kushirikisha bodi ya zabuni, taarifa hiyo inabainisha.
PPRA imeeleza katika taarifa hiyo kuwa hakuna ushahidi wowote wa nyaraka kuonyesha ni kwanini mkurugenzi huyo aliivunja bodi ya zabuni iliyokuwepo na kuteua nyingine kabla ya muda wake kwisha.

Mamlaka hiyo imependekeza mkurugenzi huyo, Benhadard Tito afike mbele ya Bodi ya wakurugenzi ya Rahco kujieleza ni kwanini alikiuka kwa makusudi sheria ya manunuzi ya umma. Vilevile mamlaka hiyo inaagiza bodi ya wakurugenzi kumchukulia hatua mkurugenzi huyo huku ikipendekeza suala hilo lipelekwe Takukuru ili kuchunguza uwepo wa mazingira ya rushwa. Mamlaka hiyo ilipendekeza Rahco ijulishwe kuwa zabuni kati yake na makampuni hayo ni batili na ianzishe mchakato upya na pia kulipeleka suala hilo kwa mkurugenzi wa upelelezi (DCI) kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo, Tito na mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya RothChild Proprietary Ltd ya Afrika Kusini, Kanji Mwinyijuma wameshtakiwa kwa makosa tofauti na hilo la PPRA. Tito ameshtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kula njama na kuisababishia Serikali hasara ya Dola 527,540 za Marekani.
 
Wako sero hadi leo, hakuna dhamana ila hili la Tito lina mkono wa jamaa mwenyewe baada ya Tito "kumjibu" nanihii.... kiufupi huenda hii kesi ikawa na ugumu na visa, ngoja tuone
 
Wako sero hadi leo, hakuna dhamana ila hili la Tito lina mkono wa jamaa mwenyewe baada ya Tito "kumjibu" nanihii.... kiufupi huenda hii kesi ikawa na ugumu na visa, ngoja tuone

Alimjibu nini Mkuu?
 
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Benhadard Tito na wenzake wawili wamepadishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo wawili wa RAHCO na mfanyabiashara wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kusababisha hasara ya dola za Marekani 527,540.

Mbali na Tito, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria wa RAHCO, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.
Vipi wauza viroba?
 
Back
Top Bottom