Kizazi hiki cha wanasiasa kinaweza kukataa ukoloni mamboleo na ubeberu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizazi hiki cha wanasiasa kinaweza kukataa ukoloni mamboleo na ubeberu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bagamoyo, Jul 15, 2011.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Kizazi cha cha wanasiasa kama Nyerere, Karume na wenzao wengi waliweza kuhamashisha umma wa watanzania hasa vijana wa shule kuanzia waliokuwa ktk ngazi ya shule za msingi/ sekondari na vyuo vya elimu ya juu umuhimu wa uhuru wa kisiasa na kupambana na ukoloni mamboleo na ubeberu wa mataifa makubwa. Tujiulize ni vipi kipindi hiki sasa, wanasiasa wanaona wale wanaoeneza ukoloni mamboleo na ubeberu kuwa watatukomboa kiuchumi, kijamii na kisiasa? kwa kufungua milango ya 'uwekezaji' toka nje bila mipaka ya kizalendo!

  Nyerere na wenzie walihakikisha nyimbo nyingi za kimapinduzi kama wimbo wa 'Bara La Afrika' wenye maneno ':
  ''Bara la Afrika lahitaji ukombozi,
  Ukoloni ni mbaya na Ubaguzi wa rangi
  Mataifa haya ya Ulaya ndiyo Afrika kuivamia
  Wahenga wetu wa zamani walikataa ubeberu,
  Walikataa ukoloni........

  Hebu tusikilize wimbo huu wa vijana wa kutoka Bagamoyo walivyoguswa na nyimbo hizo za kimapinduzi za enzi hizo kuwa bara la Afrika lahitaji ukombozi na kuamua kuzipakua ktk youtube kama historia ya kuwa ubeberu upo hai ktk wimbo maarufu 'Bara la Afrika ( African Nation) :

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. kingfish

  kingfish JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli wimbo huu ni mzuri
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  I like this line: Nyerere alipambana, kwa nini sisi tushindwe? Ni wajibu wetu kukumbuka, ubeberu upo hai.
   
 4. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kizazi cha sasa kinapingana na maudhui ya wimbo huu. chanzo cha yote ni vyama vya siasa ndio vinara wa kuendeleza mapingo ya wimbo huu.mfano kama cdm iko na CDU au kama cdm iko na Republican eti ccm iko na Democratic. hakika hili ni tatizo kubwa. waafrica tutaendelea kuwa madaraja.
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Utunzi mzuri, melody safi. Yaan kuna mistari ikitumika kwenye maandamano, watu wanaweza wakapandisha munkari mpaka ukashindwa kuwacontrol. Ok hayo tuyaache. Viongozi wetu wa leo hawawezi kuukataa ukoloni mambo leo kabisa. Sual la kujitegemea limewekwa kando na kuombaomba ndio kunapewa kipaumbele. hebu fikiria mkuu wa kaya kwenda kuomba net ya sh. 3500. Hii inatia aibu, ina maana hata hiyo nayo hatuwezi. Bora hata angeomba technology na ujuzi wa kuzitengeneza ili tuje tutengeneze wenyewe.

  Na hii mentality ya kila kitu kuomba omba kwa wahisani imeanza kuwa na athari kubwa sana kwenye kizazi hiki, sasa kama mkuu wa kaya anakwenda kuomba kila siku, unategemea watoto watajifunza nini? Akili ya haraka itawaambia kuomba ndio solution. Kesho yake asubuhi wataingia mjini na vibakuli. The aid-givers know how to do things in their own way but do they know how to assist self help among the poor, uneducated, country based? They know how to do few big things in big town, but do they know how to do thousands of small things in rural areas?
   
Loading...