Kizazi cha wapinzani kinakwisha kwa kasi, kimebaki kizazi cha wapingaji. Case study: Upinzani wa Awamu ya Tano

Haya yanayayofanywa na upinzani katika awamu hii ya Dkt. Magufuli ni dhahiri kuwa Tanzania kadiri muda unavyokwenda tunapoteza kizazi cha wapinzani wenye sifa ya upinzani na matokeo yake wapinzani wenye sifa ya upingaji ndio wanaibuka. Tunashuhudia kuzaliwa kwa upinzani shibe tuliza njaa, upinzani ambao hakika hatuwezi kusema ni mbadala wa CCM. Upinzani wa sasa ni wa kulinda maslahi yao binafsi na si ya Tanzania yetu.

Wakati wa kampeni, tumekuwa tukisikia sera zao ambazo kwa hakika zinavutia na watu kufikiri sasa umepatikana mbadala wa CCM lakini kile wanachohubiri kabla ya uchaguzi wakati wa kampeni majukwaani sicho wanachofikri kufanya baada ya kuchaguliwa. Kadhia na tabia hii imedhihirika kwa uwazi awamu hii ya tano. Utendaji wa serikali ya awamu ya tano chini ya jemedari Rais Magufuli umeufichua uhalisia wa upinzani.

Tunasikia wakipaza sauti zao pande zote wakihubiri wasiyoyaamini na wameshikwa na kiwewe kuona anayeweza kutekeleza wanayohubiri kafanikiwa. Kwa miaka mingi walihubiri juu ya mafisadi na wala rushwa na hakika hao ndio walikuwa ni wapinzani lakini sasa kizazi cha kuhubiri hivyo kimepotea kimebaki kizazi cha kupinga waliokuwa wanahubiri. Sisi watanzania tunapatwa na mashaka na kujiuliza, ni upande upi upinzani unasimama kwa maslahi mapana ya taifa hili?

Kilio cha muda mrefu cha matatizo na changamoto sugu ya mtanzania kimepata mfutaji machozi. Mwalimu Nyerere aliwahi kutuasa juu ya kuchagua viongozi wasio na sifa kwa sababu kwa kufanya hivyo tutalia kilio kisicho na mfutaji machozi. Hiyo ilikuwa ni tahadhari ya baba wa taifa hili ambapo hadhari hiyo imenijia kuwakumbusha watanzania wenzangu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ni jukumu letu kutafakari pamoja na kuja na jawabu la pamoja, ni nini hatima ya Tanzania yetu kwa kuchagua wapinzani baada ya wapinzania kuwa wapingaji? Ninaamini mwalimu angekuwepo hadi leo maneno yake aliyosema “kiongozi bora atatoka CCM” asingebadili hata herufi moja. Miaka 20 bila Mwalimu CCM imethubutu, imeweza na inasonga mbele kuwa kinara wa kulinda na kuandaa viongozi bora wa nchi hii. Hakika CCM ni jabali la wanasiasa na viongozi, twende nayo pamoja uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tatizo kubwa watu wanafikiri upinzani ni kiongozi. Wapinzani wengi Tanzania hawajali vyama ni kazi, biashara, na maendeleo yao. Kazi bado ni tatizo na wengi wanakasirishwa na kubanwa kwa uhuru. Ukiwasema au kupiga madongo hubasilishi fikra za watu za ndani.
 
KARIBU MKUU! NAONA HUJAKATA TAMAA UNATAKA TEUZI KWA THREAD ZAKO MAGUMASHI!!!

KUNA lemutuz yupo kitambo sana kwenye game bado anasugua GAGA!

Kifupi sijawahi kuona uzi wa maana toka kwako daima unakuja na U.H.A.R.O TU.
Bado anaendelea!
 
Back
Top Bottom