Kizazi cha wanasiasa vijana na wenye nguvu zaidi Tanzania

Dr Shekilango

Senior Member
Dec 30, 2013
192
117
Wakati tunaelekea kwenye Utawala wa kidikteta wa Rais Magufuli naona kuelekea miaka ya huko mbeleni kipo kizazi cha wanasiasa vijana ambao watakuwa msaada mkubwa kwa Taifa letu.

Rais Magufuli atatawala kwa mkono wa chuma na anaweza kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi, hizo Dalili zipo wazi. Sasa lazima kutakuwa na Wanasiasa jeuri na viburi dhidi yake na mfumo kadamizi ambao atauendeleza akiwa madarakani.

Kule Uganda yuko Bobi Wine wakati ambao Museveni ni mtawala mbabe kabisa katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Magufuli ni miongoni mwa madikteta chipukizi hivyo lazima wawepo vijana jeuri na viburi dhidi yake nao ni:

Mdude Nyangari, CHADEMA: Huyu ni jeuri na kiburi sana na mfuasi wa siasa za kati, sio kijana goigoi huyu ni moja wa vijana wanaoweza kupambana na Magufuli kwa kufa na kupona siyo mwoga kabisa.

Mdude Nyangali huyu kama akiendelea hivi atakuwa faida kwa Taifa.

Nicolas J Clinton, NCCR - MAGEUZI: Huyu naye ni miongoni mwa vijana jeuri kutoka chama kisichokuwa na ushawishi sana hapa nchini, Mwanadiplomasia ni kijana chipukizi anayeamini katika siasa za kushoto na mpigania demokrasia na uhuru.

Sio muoga anakosa tu jukwaa muhimu kumjenga ili kumleta karibu sana na Taifa.

Mwalimu John Pambalu, CHADEMA: Mfuasi wa siasa za kati pia, kijana msomi na mwenye moyo wa kupambana dhidi ya tawala kamdamizi kama zama hizi za Magufuli.

John Heche, CHADEMA: Naye ni mfuasi wa siasa za kati, kijana mkubwa zaidi lakini jeuri na kiburi sana ni muhimu vijana hawa kuwaangalia kwa ukaribu na kuwagroom vyema ili waje kuwa Vijana wa matumaini kwa Taifa letu.

Wapo vijana wengine wazuri pia ila kwa hawa nina matumaini nao kama viongozi wa Taifa letu hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom