Kizazi cha JKT kimeharibu nchi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,798
maudhi yanayoendelea hapa nchini kwa kiasi kikubwa yanafanywa au yamefanywa na wazee wetu ambao walipitia JKT.inashangaza kuona hawa wazee wenzangu wakilaumu vijana ati hawajapita jkt.walioko madarakani,watendaji serikalini na wapiga kura wazee ni mifano ya kizazi cha jkt.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,447
2,999
Nami huwa nashangaa hawawazee wakulaumu kizazi cha .com eti kitapeleka nchi pabaya kwa sababu hawajapita jkt na hivyo hatuna uzalendo. Kwa kiasi kikubwa hawa wazee wanaojidai wazalendo kwa kupita jkt ndo wametufikisha hapa tulipo
 
mujungu

Senior Member
Nov 1, 2010
143
55
Hii ni kweli pasi na shaka, kwani wao ndo waliokiandaa kizazi cha dotcom. sungura awezi kuzaa TEMBO.
 
ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,975
1,639
Na sehemu kubwa ya viongozi wanaoshikilia nyadhifa nyingi ni kizazi ambacho kimepitia JKT, na ulkilinganisha na hali tuliyonayo ya matatizo na jinsi wanavyoyashughulikia, ni wazi kuwa JKT haikuwa suluhu ya kuiletea nchi hii maendeleo.
 
August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,502
3,041
wazee waliotufikisha hapa sijui kama walipitie jkt au lilikuwepo wakati huo, Pius Mkara, Anna Abdullah , Kingunge CCM,hawa ndio wanafiki wakubwa ndani ya nchi hii, huku wanahubiri ujamaa na kupingana na Rushwa , huku upande wapili ndio wala rushwa wakubwa kwa upendeleo wao, kuagiza madawa ya majaribio kwa commission , angalia suala la ngorongoro, vodacom na uspika na uenyekiti wa bodi wa supika, kingunge yeye ni kulainisha wananchi kwa sera za ccm , huku kwingine vijana wana mpelekea pororo. kwenye masting.

Sasa hawa wengine akina mwanduli ndio walipitie jkt, wakajua ili wafanikiwe lazima wapeleke pororo kwa maafande wao ili vikao vya chama viwapitishe au kuwalinda.

Lakini kwa sisi wengine tulikwenda jkt, lilikuwa zuri tu, tatizo halikutumika kujenga nchi, bali kujenga ni dhamu ya woga na undumila kuwili. lakini concept yake ilikuwa nzuri, na uzalishaji ulikuwa mzuri, sema wazee wa chama wakipita lazima wapewe pororo, mwenye kuchukua gunia moja,mbili nk awe wa chama au mjeshi.

Bsi chain inakuwa hivyo hivyo mpaka kwa recruit, wenyewe walikuwa wana sema kuruta.
 
Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,614
Tupe list ya Upinzani ambao hawakupitia JKT.
..Nyie ambao hamkwenda JKT ndio hata kupiga kura hamtaki neno Uzalendo kwenu ni utamaduni ulopitwa na wakati.
 
lutamyo

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
641
158
Mkandara huyu naamin ndiye Bwanyenye aliyepo UDSM kwa sasa. Ambaye kabla hajapewa cheo alichonacho kwa asante nilidhan anafanana na akina prof Shivji lakin mmmh! Sijui huo uzalendo ni upi alionao... Angalien 2 historia itawahukumu
Tupe list ya Upinzani ambao hawakupitia JKT.
..Nyie ambao hamkwenda JKT ndio hata kupiga kura hamtaki neno Uzalendo kwenu ni utamaduni ulopitwa na wakati.
 
lutamyo

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
641
158
Hivi wazee hawa waliopitia jkt wana uzalendo upi wanaoweza kujisifu nao ktk Tanganyika hii wao ndio waliofikisha nchi hii katika lindi hili la umasikini wanazani kushangilia na kuvaa nguo za kijan ndo uzalendo. Ila kuiba, kujilimbikizia mali, kuuza nchi na kufanya maovu mengine kedekede ndo uzalendo.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,798
Tupe list ya Upinzani ambao hawakupitia JKT.
..Nyie ambao hamkwenda JKT ndio hata kupiga kura hamtaki neno Uzalendo kwenu ni utamaduni ulopitwa na wakati.
ndugu mkandara au sijui nikuite prof mkandara tatizo langu sio ccm wala upinzani bali tatizo ni system nzima iliyopo kuanzia serikalini mpaka uraiani naamini wengi wa hawa walipita JKT lakini angalia walipoifikisha nchi,leo hii tuna mpango wa kurudisha JKT tukiamini vijana wetu watajifunza nidhamu,maadili na uzalendo kitu ambacho si kweli kwani baba na babu zao wamekosa uzalendo,nidhamu na maadili pamoja na kupitia JKT.
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
maudhi yanayoendelea hapa nchini kwa kiasi kikubwa yanafanywa au yamefanywa na wazee wetu ambao walipitia JKT.inashangaza kuona hawa wazee wenzangu wakilaumu vijana ati hawajapita jkt.walioko madarakani,watendaji serikalini na wapiga kura wazee ni mifano ya kizazi cha jkt.

ati kupita jkt kunajenga uzalendo. hivi...hii mijizi ilioko ccm ni wazalendo?
 
matawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
2,053
241
Na sehemu kubwa ya viongozi wanaoshikilia nyadhifa nyingi ni kizazi ambacho kimepitia JKT, na ulkilinganisha na hali tuliyonayo ya matatizo na jinsi wanavyoyashughulikia, ni wazi kuwa JKT haikuwa suluhu ya kuiletea nchi hii maendeleo.

Naona kuna mix ya ajabu hapa. Tatizo lililopo halihusiani na jkt au kutokuwa na jeshi. Tatizo tulilo nalo ni ukosefu wa usimamiaji wa sheria maana zikiwepo sheria na wasimamiaji wakaamua kusimamia nchi isingefika hapa ilipo. Hata wachezaji kama messi na ronaldo wanacheza na kufanikiwa huku sheria zikisimamiwa
 
tz1

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
2,124
523
Naamini kama kungekuwa na jkt mpaka leo,tungeweza kukomboa nchi yetu.
Jkt ilikuwa inafundisha ujasiri,na vijana wa leo hawana ujasiri.
iIli tuweze kuwa na mabaliko lazima tuende front,vijana wataweza?
ukiwaambie tuingie front watasema "hiyo ni kazi kubwa man au nita chafuka man.
Itawzekana vipi uingie front na suruali inaninginia kwenye magoti?
 
CLEMENCY

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
211
116
Kuna mtu kama wewe aliwahi fanya research ya watu waliokuwa wanaendesha magari kisha yakapata ajali. Aliwauliza kama walipata breakfast au la. Conclusion yake ikawa wengi wa waliopata ajali walikuwa wamekula mikate. Akarecommend kuwa ili kupunguza ajali, watu wale viazi badala ya mikate.
Conclusion yako haina tofauti na mtafiti wa ajali na mikate!
 
NnyaMbwate

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,681
1,202
wengi tuliopita JKT sio wezi wala mafisadi kama baadhi mnavyotaka kuaminisha watu hapa jamvini! je huyo riz1 na wengine wanaofanana naye wamepitia JKT? WENGI WA HAO MAFISI-HADI WAKO MADARAKANI NA WAMETUMIA NAFASI ZAO SI KWA SABABU WAMEPITIA JKT! Ni PEPO tu limewakalia kichwani!
 
Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,774
1,853
Siamini kama JKT iinawajibika kusimamia tabia ya mtu baada kutoka kambini na kwenda ku-lead maisha yake mwenyewe.Kule unafundishwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu hasa kwa wanaokuzidi vyeo.So siku na wewe ukipata cheo hutarajii wa chini yako kuanza kuhoji unayoyafanya.Hiko ndicho kitokeacho sasa.Hakuna anyefikiri kuwa apaswa kuhojiwa kwa kuwa wote walifundishwa 'nidhamu ya hali ya juu'
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,736
27,798
Naamini kama kungekuwa na jkt mpaka leo,tungeweza kukomboa nchi yetu.
Jkt ilikuwa inafundisha ujasiri,na vijana wa leo hawana ujasiri.
iIli tuweze kuwa na mabaliko lazima tuende front,vijana wataweza?
ukiwaambie tuingie front watasema "hiyo ni kazi kubwa man au nita chafuka man.
Itawzekana vipi uingie front na suruali inaninginia kwenye magoti?
kama kweli JKT ilifundisha ujasiri iweje leo hii watu kama kina rostam et al wanayumbisha nchi?naamini vijana wa leo ni majasiri kwani wanaweza kuipinga serikali waziwazi,wanaweza kuandamana pamoja na vitisho vya polisi nina uhakika huko tunapoelekea wataanza kujitoa muhanga.wanaotuangusha ni hawa wa wazee wenzangu wa JKT ambao wanakosa ujasiri wa kusema kodi ya madini iwe 50%
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom