Kizazi Cha 1946-1956 Wametuletea Umasikini Mkubwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizazi Cha 1946-1956 Wametuletea Umasikini Mkubwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Oct 26, 2011.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Jamani hiki ni kizazi cha Tanzania ambacho hakuna cha kujivunia!!. Hiki ni kizazi cha watoto wa Nyerere na mababa zetu. Kizazi cha kwanza kuja baada ya Mkoloni wamesomeshwa bure wengi mpaka masters, walikuwa hawana shida ya kutafuta kazi kuanzia ualimu mpaka jeshini. Kwa mara ya Kwanza hiki kizazi kililetwa mijini kutoka vijijini. Zaidi ya kuwa waongeaji na kutukuza sisi tofauti na wao wengi wa kizazi hiki wametuibia nchi sana. Hawaja Invest kabisa na hakuna ubunifu uliobadilisha nchi kutoka kizazi hiki. Hatuna Steve forbes au Bill Gates Tanzania, Hospitali ziko China wakati Chuo kikuu cha Dar kina miaka 50, Shule zimekuwa mbaya kuliko zamani ingawa sasa watu wengi wanalipa na wanategemea tution, pesa za maendeleo nyingi zimeishia mifukoni. Mimi nachosema ni kwamba kuna wengine lakini hawa ndiyo viongozi wetu mpaka sasa kwenye idara mbalimbali. Mimi naamini Tatizo kubwa Tanzania ni Kizazi
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,608
  Likes Received: 3,910
  Trophy Points: 280
  Vizazi vyote ni vinaweza kuwa 'wasted generation' mpaka CCM iondoke madarakani. kizazi cha 1960 mpaka 1986 kimefanya nini na kinafanya nini? if you do no have a solution you are part of problem.

  Please lets not point fingers to others until we have done something!
   
 3. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa 3 years ago niliweka bandiko langu hawa jamaa wakalitungungua lakini mie nikasema poa. This tiome sijui kama wataweka hii. Ni kweli hawa jamaa walilishwa maziwa na shayiri ambalo lilikuwa lagawanywa mashuleni. Sas nikilink na hili usemalo naona kama ilikuwa mfumo wa kisayansi kuwa-brainwash hawa jamaa. We fikiri hadi aliyesaini katiba ya nchi fisadi. Naomba kuwakilisha.
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Mimi siamini kama sisi na hawa wa zee ni sawa wengi wetu tumeshafanya mengi kuliko hawa wazee na hata hatuna madaraka mfano Kizazi chetu mawazo ya kwenda nje kutafuta elimu na maisha hajaletwa na serikali bali mwamko wa vijana na sasa tunasaidia ndugu, nchi kwa kutuma pesa na wengine tumejisomesha wenyewe vyuooni na kufanya kazi na kujitegemea kuanzia miaka 22. Hawa wazee wamesomeshwa, wamepewa kazi na uongozi na wameiba. Wegi wetu hatujawahi kuchukua rushwa kwenye maisha yetu hata senti moja! na tunaishi.Vijana wengi wanafungua biashara ingawa hawa wazee wameruhusu bank zinazoiba pesa na hazitoi mikopo. Hakuna hata umeme wa uhakika Tanzania kwasababu ya mikataba mibovu. Hawa wazee wameishia kuitana waheshimiwa na ku kiss up lakini zaidi ya kuwa wazazi wametuharibia nchi sana
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Waberoya, let us accept and direct blame where it fits best!! Mimi ni kizazi hicho huyu bwana anachokilaumu na nikweli kizazi changu hakuna kitu cha kujivunia bali ni aibu tu. Nashawishika kusema kuwa naona aibu zaidi nikitambua kuwa huyu rais wetu ni co-hort yangu lakini hana la maana alilofanya kwa nchi yetu hata baada ya kupata overwhelming support ya wananchi . the best he has done is to divide the country on religious grounds as a means of his political survival at the same time being insensitive to the problems afflicting the majority of the population; his insensitivity to the chronic national problems is exemplified by his frequent travels to foreign countries even when it is unnecesary for him to do so!!
   
 6. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  I have a story to share of a boy within the age range you have picked who slept on mkeka and teremka tukaze, used a pit latrine, lived in hatched house and went to school barefoot now owns a bungalow in Oystebay. Once he saw the life in town when he first arrived the only achievement he thought he could have was to be where he is right now. The down side of this story is that firstly he never thought that "oyster bay" could be built every where in his Tanganyika in places like Mbambabay..Secondly he could have more than the colonial government innovation. With these " thick heads" on helms of our leadership ladder would you wonder of our fate?ooooh the dollar today goes at 1800sh.
   
 7. T

  Tata JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Nimebahatika kufanya kazi na watu wa kizazi hicho na kwa kweli mpaka leo sijafanikiwa kuelewa mindset yao. Moja ya sifa yao kubwa ni kukwepa kufanya maamuzi magumu hasa pale wanapohisi kuwa yanaweza kuwaathiri wao na familia zao. Kama kuna mkakati ulikuwepo wa kuandaa watu wa aina hii basi aliyeuandaa alifanikiwa sana.
   
 8. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sasa ni jukumu la kizazi cha 1957-1985 kuleta mabadiliko chanya ili kizazi cha 1986------ kisije kutulaumu. wahenga wa kidhungu walisema better late than never.
   
 9. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Steve Jobs not Steve Forbes!
   
 10. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Nyie mtaitwa kizazi cha kulalamika. Majawabu (solutions) mlizonazo ni zipi? Rika mnalolilalamikia ndilo limejenga vyote unavyoviona ingawa vingi vimeishapokonywa katika 'ubinafsishaji'. Kama unatamani kusoma bure hilo liliwezekana enzi hizo na ndiyo Ujamaa wenyewe mnaouchukia sasa. Huwezi kuchukia mti ukatamani matunda yake. Kama mnafuatilia zilipoingia sera za ubinafsishaji kulikuwa na mshirika ya umma zaidi ya 400 vikiwemo viwanda. Vyote vilijengwa na rika hilo linalolaumiwa. Labda nikupe mifano kidogo. Tuanze na viwanda vya simenti. Twiga (Dar), Simba (Tanga) na Tembo (Mbeya) vilianzishwa chini ya Nyerere. Tuje Viwanda vya Nguo: Urafiki (Dar), Ubungo Spinning (Dar), Mwatex (Mwanza), Mutex (Musoma), Mbeya Textile (Mbeya), Moro Canvas (Moro), etc.. Twende Mahotel: Kunduchi Beach (Dar), Kilimanjaro Hotel (Dar), New Africa (Dar), Mafia Island Lodge (Mafia), Mikumi Wildlife Lodge (Moro), Ngorogoro Crater Lodge (zamani Arusha), Lake Manyara Hotel (Arusha), Lobo Wildlife Lodge (Arusha), Mount Meru Hotel (Arusha) na nyingnezo. Haya twende viwanda vya sukari: TPC (Kilimanjaro), Kagera Sugar (Kagera), Kilombero I & II (Moro), Mtwiba Sugar (Moro). Orodha ni ndefu. Siyo tu viwanda vilijengwa bali jitihada ilifanywa kuvisambaza nchi nzima. Ni sera zenu 'nzuri' za WB, IMF, na mabepari wa dunia mnazozihusudu ndizo zilishinikiza vyote viuzwe (vibinafsishwe) au vifilisiwe ndizo zimetufikisha hapa tulipo. Labda wengine kwa udogo wenu hamjui historia hii. Acheni kulalamika. You can't have your cake and eat Sharobaro meeeeeeeeen.
   
 11. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  2sije pata lana bure kwa hawa wazee hebu fikiria nape na mwigulu je? wapo kwenye hiyo time flame maana story zao hazina tofauti na hao wazee kabla ha2jawalalamikia hawa wazee 2tafakari nape, ngeleja, adam malima wanafanya nini tofauti na wazee hao? Muda mwingine naona bora ya hao wazee kwani mpaka leo bado 2na2mia miundombinu yao ya umeme, maji, wali2letea uhuru wa bendera etc
   
 12. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wait until you see the 1956 to 66 kizazi - the Ngelejas; Jairos; Chamis; Mwakyembes, Masha etc I believe so far they have very little to show. The only one who seems to have some vision is the CDM Chaiperson Mbowe - but time will tell. The 1966 to 76 kizazi is just naively too ambitious - the Nape; January Makamba; Millya; Nchimbi,etc They should spend the next decade getting useful experience rather than aspiring for high political posts.
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa nadhani umekurupuka hukufanya kautafiti japo kadogo tu. Hayati Nyerere alizaliwa mwaka 1922 na kamwe hawezi kuangukia kwenye rika la 1946-1956. Hivyo vitu ulivyoviorodheshwa havikujengwa bali viliuzwa na kizazi cha 1946-56. Naomba ukafanye kautafiti kengine utuorodheshee vitu walivyojenga rika hili tunaloliongelea. Kwa kukurahisishia kazi naanza na shule za kata.
   
 14. Capital

  Capital JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,036
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa napita tu ila baada ya kuona comments zako ikabidi nisimame nisome kidogo. Nikagunduwa kauli yako eti "tutaitwa kizazi cha kulalamika" haifurahishi na inalenga kufisha kwa maksudi ukweli. Kwanza ifahamike kuwa watu wote waliohusika katika ubinafsishaji sio kizazi cha sasa, ni kizazi hicho cha 1946-1956. kizazi hiki ni hopeless, nakifananisha na chief Mangungo wa Msowero alivyolaghahiwa na matapeli wa kizungu akauza nchi yake. Kizazi tajwa nahisi hakikuwa na elimu au falsafa stahiki kuweza kutujengea utajiri. Hakika hawa ni watu walikuwa wameleweshwa ujinga wa kuamini kuwa wazunu ni bora, wana akili kuliko sisi na ushauri wao ni wa msingi. Ndo maana nchi hii iliendelea kuingizwa kichakani kuanzia SAP (structural adjustment programs) na market-led economy, wasijuwe kuwa hii ilikuwa mbinu chafu dhidi ya mtu mweusi-Mtanzania. Hawa wazee continued to cling onto old and worn out dogmas while the world was changing very fast. Badala ya kukaa na kufikiri kwa kina kuandaa positive and far-reaching REFORMS, walikaa na kuimba nyimbo za ajabu eti zidumu fikra za mwenyekiti na ujinga mwingi tuuuuu kama mwenge! shameless.

  kitu kingine hawa wazee hatutawasamehe ni kufikiria kuwa wazungu can give you free money! wakasahau kuwa wealth is created by sweat, perseverance and not otherwise. Ona sasa Tz haiwezi kutengeneza hata tooth-pick, 50 years down the road after independence.

  Kizazi chetu sasa, 1970-1985, tuna kazi kubwa. kazi hiyo ni NEW INDEPENDENCE. Warning, this independence can come only through sacrifice. Ni PM niwape maujanja. Else, tuendelee kunywa ndovu na wine za South Africa, kula kuku wa Brazil wakati tunaweza kufuga, kuvaa nguo za kichina wakati tunalima pamba, kutumia sukari ya India wakati ardhi, viwanda tunavyo, watoto wetu watatupiga mawe. Trust me.
   
 15. NAIPENDA TANZAN

  NAIPENDA TANZAN Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependezwa sana na orodhayako fupi ya mafanikio uliyoyataja, lakini nadhani umesahau kitu kimoja, Mwenye mada ameongelea kizazi cha 1946-1956, naamini kuwa mafanikio yote uliyoyataja yalifanywa na wengine nje ya kizazi hicho, yaani akina MWL NYERERE, hawa sio wa kizazi cha 1946- 1956. Hawa wako kwenye kizazi cha 1920 - 1945.
  Aliye anzisha hii mada amejaribu kulinganisha baina ya hizo generations, hii ya 1946 hadi 1956 ndio wanaoendelea kuuza viwanda vyote na maliasili zote za watanzania. Na ni hao hao tulionao katika ngazi nyingi za kutengeneza sera na ngazi za maamuzi.
  Kizazi hiki ulichokiita cha kulalamika kimeyaona haya na kimeanza kuchukua hatua, kwa taarifa yako, hiki kizazi kiko kwenye hatua muhimu ya kuleta mageuzi kwenye thinktank ya Tanzania. Hatua yoyote ya kuleta mageuzi inaanza na awareness creation, katika hatua hii kizazi hiki kinajaribu kuwainua wale wenye ubongo uliolala au wenye fikra mgando, hawa wakisha amka hawatalala tena bali nao watawainua wengine.
  Pia ni vizuri nikufahamishe kuwa KULALAMIKA ni hatua ya kwanza ya kuonyesha kutoridhishwa na jambo/ mambo fulani.
  Naamini wewe sio sehemu ya tatizo hili la kizazi cha 1946 - 1956, kwa msingi huo ninashauri uwaunge mkono hawa WALALAMIKAJI na kutoa ushahidi wa yote mabaya yaliyofanywa na wanayoendelea kufanywa na kizazi cha 1946-1956 ili hatua zaidi za KIUKOMBOZI zichukuliwe.

   
 16. NAIPENDA TANZAN

  NAIPENDA TANZAN Member

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependezwa sana na orodhayako fupi ya mafanikio uliyoyataja, lakini nadhani umesahau kitu kimoja, Mwenye mada ameongelea kizazi cha 1946-1956, naamini kuwa mafanikio yote uliyoyataja yalifanywa na wengine nje ya kizazi hicho, yaani akina MWL NYERERE, hawa sio wa kizazi cha 1946- 1956. Hawa wako kwenye kizazi cha 1920 - 1945.
  Aliye anzisha hii mada amejaribu kulinganisha baina ya hizo generations, hii ya 1946 hadi 1956 ndio wanaoendelea kuuza viwanda vyote na maliasili zote za watanzania. Na ni hao hao tulionao katika ngazi nyingi za kutengeneza sera na ngazi za maamuzi.
  Kizazi hiki ulichokiita cha kulalamika kimeyaona haya na kimeanza kuchukua hatua, kwa taarifa yako, hiki kizazi kiko kwenye hatua muhimu ya kuleta mageuzi kwenye thinktank ya Tanzania. Hatua yoyote ya kuleta mageuzi inaanza na awareness creation, katika hatua hii kizazi hiki kinajaribu kuwainua wale wenye ubongo uliolala au wenye fikra mgando, hawa wakisha amka hawatalala tena bali nao watawainua wengine.
  Pia ni vizuri nikufahamishe kuwa KULALAMIKA ni hatua ya kwanza ya kuonyesha kutoridhishwa na jambo/ mambo fulani.
  Naamini wewe sio sehemu ya tatizo hili la kizazi cha 1946 - 1956, kwa msingi huo ninashauri uwaunge mkono hawa WALALAMIKAJI na kutoa ushahidi wa yote mabaya yaliyofanywa na wanayoendelea kufanywa na kizazi cha 1946-1956 ili hatua zaidi za KIUKOMBOZI zichukuliwe
   
 17. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  mfululizo wa vizazi na maendeleo yao baada ya uhuru 1961-1970 maendeleo ya kati, na watiifu kwa serikali, 1971-1982 hawana kazi wengi matapeli wana uchu wa madaraka na wapenda sifa , wanavijisenti sana kwa kuwani kizazi cha mzee ruksa walifanya sana biashara hewa 1983-2010 hawa ni bongo fleva, wapenda kutunzwa na mijimama, madawa kwa sana, mziki na maigizo ndio waona njia kuu ya kipato wana ndoa za kuoana leo kesho wakamwagana ni watu wa skendo za ngono na ulevi, sasa tuwaokoe wa 2011 -2020 watupeleke mwezini
   
 18. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Mimi naona haya malalamiko ni ya Msingi.

  Jamani tuangalieni Chuo kikuu cha Muhimbili kilikuwa kwa miaka mingapi?? Hawa wazee hawajaendeleza hivi vyuo kwasababu hawajaangalia mbali na tatizo haikuwa pesa. Sasa wamezeeka na kuanza kuumwa wanataka tuwapeleke India kutibiwa!! je tutapeleka watu wangapi India?. Je hao madoctor wote kwa miaka yote hiyo wako wapi na wanafanya nini??. Sasa vyuo kama Dodoma vinajengwa na pesa za vijana za michango ya NSSF na siyo serikali!. Nyumba za polisi kwa miaka yote zimemalizika juzi na NSSF, Umeme NSSF, Barabara USA, Japan. Meneja wa zamani wa Urafiki alijenga ghorofa Kariakoo wakati kiwanda kilivyokuwa kinakufa 1995-1996. Hata railway hatujajenga. Lazima tukubali kizazi chetu ndicho kitabadilisha hii nchi na hatuwezi kuacha nchi kwa watoto wetu kama hawa wazee walivyotufanyia.
   
Loading...