Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,655
- 729,724
Kwa wale wapenzi na walioko kwenye mahusiano na ndoa migogoro ni kitu cha kawaida na sehemu kubwa ikisababishwa na wivu...lakini pia kuna hali ya kuzoeana na kuchokana Kwa kiasi fulani
Tukiachana na haya matamanio ya kawaida ya kimwili ambayo macho huona na kuvutika, kuna hisia za ndani kabisa ambazo ndio hubeba mapenzi ya kweli! Hizi hisia hazionekani machoni bali huzihisi gizani
Migogoro mingi imetatuliwa na hizi hisia za ndani kabisa muwapo kitandani pekeyenu gizani, mmenuniana siku kadha lakini mara kila mmoja Kwa wakati wake hukumbuka nyakati za furaha na mapenzi motomoto...mara kila mmoja wenu huhisi uwepo wa mwenziwe na upweke hapo hapo na kujikuta hisia za kumbatio kuja Kwa kasi ya ajabu na kusahau mapungufu yote ya mwenzio na migogoro....kifuatacho baada ya hapo ni jambo la kumbukumbu nzuri
Kuna wakati mwanaume inabidi kumchukulia mwanamke kama mpenzi lakini pia kama
-mama yake
-rafiki
-mdogo wake
-mtu wake wa karibu
-kiongozi wake nk
Na wanawake hivyo hivyo kwa wanaume
Ishu ya kutatua migogoro gizani inahusu kipengele cha mapenzi tuu