Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Imekuwa kama vile serikali ya Kikwete ni serikali yenye mikosi vile, kwa maana kila jambo wanalojaribu kulifanya hawaachi kukosea.wakitaka kuboresha Elimu ya juu wanakosea,wakitaka kuboresha michezo wanakosea,yaani wao kazi yao ni kukosea tuu kila siku!
jana wakati akiongea na wafanyakazi wa TBC yaani shirika linalojaribu kuwa la habari Tanzania, kwa sababu mpaka sasa ni kama vile ni shirika la habari la CCM, Waziri wa Habari George Mkuchika alisema mambo mawili yaliyonichanganya hadi kutaka kutafiti kwa wana JF.
kwanza alisema kuwa CNN ni shirikal la habari linalomilikiwa na serikali ya Marekani kitu ambacho najua si sahihi. Sasa kama kuna mtu ana ushahidi kwamba CNN ni shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya Marekani anitoe tongotongo!
Pili mkuchika anadai kuwa Mao Tse Tung aliwahi kusema kuwa "No investigation No right to speak" mimi nadhani mao alisema "No research No right to Speak. Sasa kama kuna mtu atatuthibitishia kwamba haya maneno mawili yaani "Research" na "Investigation" yana maana moja nitashukuru sana.
Mkuchika alikuwa anatetea dhana ya serikali kuendelea kumiliki vyombo vya habari dhidi ya hoja za wadau wengine wanaotaka serikali iviachie vyombo hivyo viwe huru na kumilikiwa na Umma.