Kiwanja changu kimekaa kama sambusa, ninapanga kumega eneo la jirani kiwe square. Sheria inasemaje kuhusu hili?

Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,373
6,756
Kwa kweli siridhiki kuona kiwanja changu kimekaa kama sambusa.. Natamani kiwe square kama kiwanja cha mpira.

Sasa ili 'kuboresha mipango miji' ninapanga kumega kama mita moja kutoka kwa jirani ili kikae sawa.

Hapa ninakusanya nguvu ya tofali elfu mbili.. Nikija kuibuka naibuka na ukuta mmoja mrefu wa maana.

Mpaka jirani aje kushtuka atakuta kuna ukuta mzito kama ule wa kuzuia bahari wa Ocean road.
Je, kuna mwenye wazo tofauti?
 
I HOPE HUJACHUKUA CHA MKURYA
SI KILA MTU ANATUMIA SHERIA KUDAI CHAKE

MWENYEWE UTATOROKA UKIANZA KUKIMBIZWA NA MAPANGA NA MISHALE WEWE NDIO UTATAFUTA SHERIA ILIKO NA KITUO CHA POLISI KILIKO BAADA YA KUWA UNAVUJA DAMU KILA ENEO KWA KUKATWA MAPANGA NA KUCHOMWA MISHALE
 
Ukutane na jirani kauzu kama mimi wallah nabomoa kuna mwenzio alileta ujinga kama wako nilibomoa.
 
Ulibomoa kwa gharama za nani? wewe una huruma mbona
Mimi mwenyewe nilikodi vijana wakabomoa na kuna mwengine namuona anajipendekeza upande mwingine sijui kwa nini baadhi walidhiki na ukubwa wa viwanja vyao mtu ukinunua unajua hiki kitanifaa kwa matumizi ama la
 
jiandae kabisa kwenda kwa sangamo, huyo jirani yako hata kuacha kama ulivyo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
huwa kuna majirani wanapendana kama ni uswahilini anahama.

kuna jirani mmoja alichukua kiwanja cha mwenzie maeneo yasiyopimwa .Yule aliyeporwa kiwanja akawaambia majirani .Majirani wakasema haina shida .USiku kaenda na gari zake mbili alikuwa na dala dala na ya kutembelea akapaki.

usiku sehemu ya barabara ya kuingilia majirani wakafunga kwa kujenga ukuta wakiunganisha nyumba zao ili asiwe na pa kutokea.Asubuhi anatoka getini akajikuta kazungukwa na kuta kama yuko magereza.Watoto hawawezi kwenda shule wala yeye kutoka.

IKabidi aruke ukuta aulize kulikoni.Wakasema ile barabara ni eneo lao waliachiana tu nafasi kama majirani sio barabara ya serikali wamekubaliana wameamua kujenga ukuta vibaka wanawasumbua.AENDE KOKOTE.kWENDA SERIKALI YA Mtaa kule akaambiwa hilo eneo ni lao wana haki kufanya nalo chochote.

Ilibidi aongee nao wamuuzie wakagoma wakasema hawahitaji pesa

Ilibidi ahame na aliuza eneo kwa hasara kwa msikiti ,msikiti wakaongea na majirani wale majirani wakavunja kuta kwa gharama zao akatoa magari yake na vitu vyake akahama moja kwa moja

mambo ya ukorofi wa ardhi sio mazuri
 
Umeeleza tabia za walio wengi, sijui wakati unakinunua hukuona kiko kama sambusa!!
 
Kwa kweli siridhiki kuona kiwanja changu kimekaa kama sambusa.. Natamani kiwe square kama kiwanja cha mpira.

Sasa ili 'kuboresha mipango miji' ninapanga kumega kama mita moja kutoka kwa jirani ili kikae sawa.

Hapa ninakusanya nguvu ya tofali elfu mbili.. Nikija kuibuka naibuka na ukuta mmoja mrefu wa maana.

Mpaka jirani aje kushtuka atakuta kuna ukuta mzito kama ule wa kuzuia bahari wa Ocean road.
Je, kuna mwenye wazo tofauti?
watu km nyie tukiwakabidhi madaraka kuongoza nchi mnakuaga wezi kupindukia hamridhikagi.
 
Back
Top Bottom