Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,430
Habari zenu wapendwa. Natumai mu wazima na poleni na mihangaiko ya siku ya leo.
Naomba mawazo yenu au msaada wenu kwenye jambo hili dogo au kubwa ambalo nimelifikiria sana kwa muda mrefu katika maisha yangu na kwenye mahusiano niliyokuwa nayo mwanzoni mpaka leo hii.
Binadamu tumetofautiana namna ya kuvumilia jambo au tabia fulani kutoka kwa wenza wetu. Kuna mtu hata mpenzi wake akimsaliti lakini bado ataendelea kuwa naye lakini kuna mwingine inakuwa ndio mwisho wa mahusiano. Hivyo hivyo kwa baadhi ya tabia, kuna baadhi ya tabia watu fulani wanaweza kuzivumilia lakini kuna wengine hawawezi kuzivumilia. Hii ni kutokana na mitazamo tofauti ya kimaisha.
Je kiwango cha uvumilivu kwenye mahusiano kinatakiwa kiwepo mpaka kwenye nafasi ipi? Namaanisha ni kwa kiwango gani au muda gani umvumilie mwezi wako katika mambo anayoyafanya mpaka pale itakapofika useme sasa basi nimeshindwa kila mtu afanye yake. Pia kwenye mahusiano kwa ujumla ni mambo gani ni ya kuvumilika na yapi sio ya kuvumilika?
Nawasilisha
Matusi tafadhali yasiwepo mjadala usonge kwa amani