Kiwango cha Elimu na kipawa cha uongozi wapi na wapi

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
918
1,401
Juzi nimemsikia spika was Binge la JMT ndugu Job Ndugai akitoa tathmini ya viwango vya Elimu za Wabunge , na mwishoni mwa tathmini yake akajisifia kuwa CCM Ina idadi kubwa ya wabunge wenye PhD hili ni kweli, lakini mbona kwa idadi hiyo bado haiendani na uwezo wao wa kiutendaji, wamekuwa ni dhaifu kwenye kujenga hoja za msingi ambazo zingaliweza kulikwamua taifa letu kwenye mikwamo mingi hasa inayo husu utata wa mikataba mbali mbali ambayo imeleta taharuki kubwa na mingine imesababisha serikali kushtakiwa na hatma yake imekuwa ni kushindwa na kupelekea hata Mali za serikali kuwekwa rehani.

Swali ni hili hivi Ndugai anapo jivunia wingi huo mbona kwa upande mwingine hauendani na uhalisia wa kiutendaji ? Hawa anao waita wasomi ndio wamekuwa dhaifu kabisa katika kujenga hoja mbali mbali bungeni hadi kupelekea serikali kupiga marufuku uonyeshaji wa bunge live au Job anadhani wananchi ni maamuma kwa kiwango hicho, ni wasomi wanaojali matumbo yao kuliko maslahi ya Taifa letu , wamebaki kuwa watu wa ndiiyo ndiyo , na zaidi wamebaki kudhalilisha Elimu waliyo nayo mbele ya jamii ya kitanzania.

Si dhani kuwa kama uwiano wa kiwango chao cha Elimu kinaendana na ushauri wao kwa naslahi ya nchi yetu. Tumeshuhudia teuzi za wasomi wenye viwango vya Doctors ,na professor's lkn utendaji wao umekuewa wa kiwango kisicho ridhisha kabisa, nadhani kuwa unaweza kuwa na kiwango cha Elimu ya kawaida na bado ukawa na mawazo chanya na yenye tija kwa maslahi ya nchi yako.

Humo ndani ya bunge wanao ongoza kwa kutoa michango iliyo mizuri na yenye maslahi ni hao wenye Elimu ya kati, sasa sijui kuwa huenda wabunge wasomi huwa wamejaa uwoga wa nini kama si kudhalilisha Elimu waliyo nayo.

Lakini pia bado ukifanya mahesabu vizuri bado utaona kuwa vyama upinzani wana uwiano mzuri wa wasomi na idadi yao ndani ya bunge.

Niliwahi kuhudhuria kampeni za uchaguzi wa mbunge Fulani ambaye kiwango chake cha Elimu kilikuwa ni darasa la saba , aliulizwa swali kuwa , ndugu unaomba na fasi ya ubunge mbona kiwango chako cha Elimu hakiendani na uzito wa kazi yenyewe ?

Jibu lake lilikuwa kuwa hao unao waona kuwa ni wasomi ndio niliyo waajiri kwenye kampuni yangu, hivyo sio kweli kwamba pale pana takiwa Elimu kubwa Ila kikubwa ni hekima. Jibu hill japo lilikaa zaidi kisiasa .

Swali ni hivi kweli kiwango cha Elimu kinaendana na kipawa cha uongozi ?
 
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tonny Blair aliiongoza vyema Uingereza, hakuwa na elimu ya kutisha!, Barack Obama ni Msc.holder, ameikwamua USA kwenye janga la mdororo wa uchumi 2008- 2012.

Mh, Augustine Mrema, Hayati Sokoine, Mh Lowassa n.k unaweza ku eye mark walichofanya wakiwa watendaji wateule.
Lakini, kwa upande wa pili, ili nchi iendelee,elimu ni chaguo la msingi.

Kwa maoni yangu Uongozi bora unahitaji vitu vitatu ; Kipawa + Elimu + Hekima; ukikosa kimojawapo, ni kazi bure.
 
Back
Top Bottom