Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 13,806
- 15,787
Kwa vile nimekuwa mtu wa mitini mara nyingi, inawezekana kuwa jambo hili limekisha ongelewa hapa kijiweni. Najua kuwa mwaka jana tuliwahi kuwa na thread ya kutathmini utendaji wa serikali ya Mwungwana Kikwete lakini sikumbuki tuliishia wapi, na nilipojaribu kuitafuta sikufanikiwa kuipata.
Kumbukukumbu yangu kuhusu muundo wa serikali zetu tangu tupate uhuru siyo nzuri sana na nitashukuru sana kama kuna mtu atakayeweza kunikumbusha. Ninataka kuongelea swala la kazi na ajira. Mwanzoni baada ya uhuru kulikuwa na Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii; baadaye ikaja Wizara ya Mawasiliano, Kazi na Ujenzi; na nadhani mwishoni kulikuwa na Wizara ya Kazi na Utumishi ingawa sina uhakika kuwa Mkapa alikuwa na wizara ya namna ipi kuhusu kazi. Wizara ya kazi ilikuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa waajiriwa wote wanatendewa haki na matajiri wao.
Rasi Kikwete alipoingia madarakanai aliunda Wizara iliyokuwa na neno ajira na hilo ndilo jambo ninalotaka tulichambue. Wakati ule nilisema kuwa Col. Kikwete alikuwa anawadanganya walala hoi wanaohangaika kutafuta ajira; nikasema kuwa uingizaji wa msamiati "ajira" katika jina la mojawapo ya wizara zake ilikuwa ni namna ya kujikosha kuwa serikali yake itawashughulikia vijana kupata ajira, lakini hakukuwa na lolote bali danganya toto tu.
Sasa jana jioni nikiwa hapa Crystal City Marriott nilipata nafasi ya kusikiliza wimbo wa Nakaaya unaosema Mr. Politician na kilichonikuna ni pale dada huyu alipoongelea ile ahadi ya "ajira nje nje." Nikasema nikurudi kijiweni nitawaomba rafiki zangu tuliongelee tena,
Swali langu ni, je ni nini majukumu ya Wizara hii, na je unemployment rate ya Tanzania ikoje leo hiiu ukilinganisha na mwishoni mwa mwaka 2005? Uanajua kuwa nemployment ndilo tatizo la kwanza linaleta mabadiliko ya kisiasa katuka nyingi hapa duniani. Nadhani kuwa wazee wenzangu mnalikumbuka sana tatizo la unemployment pale Uingereza baada ya vita ya Forkalnds ambalo ndilo lilipekea kuundwa kwa bendi ya reggae ya UB-40 (yaani unemployment benefit form number 40) pamoja na mambo mengine. Wakai huo uzalendo ulisaida kulinda utawala wa Mama Chacha.
Je Wizara hiyo ya kazi na ajira inatoa huduma gani kwa watanzania wasiokuwa na ajira? je, inawalipa social security allowance au unemployment benefit yoyote ile, je inasimamia kuhakikisha kuwa ajira hazitolewi kwa watu nje wakati kuna atanzania wanazihitaji? Nimwahi kuruka na ATCL kutoka Dar kwenda Mwana wakati mhudumu mle ndani alikuwa m-South Africa, na sikuelewa kabisa kama kweli dada zetu hawajui kuhudumia ndani ya ndege zinazofanya domestic flights.