Kiwanda hiki kinakwepa kodi.

KATATA

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
478
500
Wasalamu wana JF. Pamoja na sikukuu, ni vema nikatoa taarifa ya kile nilichokipata Arusha. Eneo la Njiro, Arusha karibu na yalipo majengo ya General Tyre, kuna kiwanda kinaitwa Fibre. Hiki kiwanda kilikuwa mali ya serikali na kikauzwa kwa ndugu wawili raia wa India. Tangu kuuzwa kwa kiwanda hiki, mamlaka ya mapato huwa haipati mapato sitahiki kutoka kwa wezi hawa. Wafanyakazi wengi ni Wahindi; jambo la kushangaza ni kuwa hata walinzi wamechukuliwa kutoka India kuja kulinda Tanzania, walinzi hao hawajui Kiswahili wala Kiingereza, wanajua Kiindi tu. Mbaya zaidi hata Ofisi ya Afisa uajiri ambaye ni Mtanzania iko getini ambako kwa kawaida inakuwa ofisi ya walinzi. Afisa uajiri yuko kama bendera tu na wala hausishwi kwa lolote. Hii habari nimeiandika kutokana na yale niliyoyashuhudia ndani ya Ofisi hiyo na ushuhuda wa wafanya kazi wawili. Hawa watu wamekuwa na urafiki wa karibu na Kikwete tangu akiwa waziri wa mambo ya nje.
Naomba kuwasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom