Kiwanda chatozwa faini na NEMC

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Serikali kupitia Baraza laTataifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC imekitoza faini ya shilingi milioni kumi, kiwanda cha kutengeneza sabuni cha Royal Soap industry cha Mabibo jijini Dar es Saal kwa kosa la kutiririsha maji machafu na yenye sumu sambamba na vumbi la sabuni lenye kusambaa katika makazi wa watu na mazingira ya mto kibangu.

Uchafuzi huo wa mazingira umekuwa ni wa muda mrefu katika makazi ya mtaa wa mabibo kisimani na kupelekea afya za wakazi wa eneo hilo kuwa hatarini, kutokana na maji machafu yenye kemikali na vumbi la sabuni, na kupelekea wananchi wa mtaa huo wa kibangu kupeleka malalamiko yao katika Ofisi ya Makamu wa Rais, na ndipo Naibu Waziri wa Ofisi Hiyo anaeshunghuliakia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina, kuinuka ofisini na kwenda kujionea adha wanayoipata wakazi hao.

Naibu Waziri Mpina alilielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuatilia vipimo vya vumbi na maji ya sabuni yanayotiririka katika mazingira na mto kibangu, kama ni rafiki kwa mazingira na viumbe hai na kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku kumi na nne sanjari na kukitoza faini ya shilingi milioni kumi kiwanda hicho na kukitaka kilipe kwa muda huo wa wiki mbili, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zaake ya mwaka 2004.

Naibu Waziri Mpina, yupo kwenye ziara ya ukaguzi wa mazingira na kufuatiliaji na uzingatiaji wa sheria ya mazingira na kanuni zake kwa wawekezaji wenye viwanda nchini. Amewashukuru wananchi kwa kuripoti moja kwa moja kwa serikali juu ya waharibifu wa mazingira, na kuonyesha kuwa malalamiko ya wananchi yanafanyiwa kazi, Naibu Waziri Mpina anafanya Ziara nyingi za kushtukiza katika viwanda.
 

tereweni

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
597
500
Safi sana Mpina....
Kuna vingine vingi fanya uvitembeleage utakutana na hali kama iyo ya BIBO
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,729
2,000
Hao NEMC kwanini wanaviogopa vile viwanda vya Morogoro ambavyo navyo vinatiririsha maji yenye kemikali kwenye mto ambao maji yake yanatumiwa na binadamu na mifugo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom