Kiwanda cha spirit kifaru kuuangamiza mlima kilimanjaro

matubara

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
226
88
Wapendwa Watanzania, hivi karibuni kimefunguliwa kiwanda cha kutengeneza spiriti katika eneo la Kifaru,Mwanga Kilimanjaro.Kwa wanaopita na mabasi kutoka Dar kwenda Arusha nadhani mnakumbuka harufu kali inayotoka kiwandani hapo. Mojawapo ya nishati wanayotumia kwenye ma boiler yao ni magogo mabichi! Wananunua kwa bei nzuri sana ili mradi magogo hayo yawe mabichi na hasa yale yanayotoa utomvu! Hivi sasa wafanyabiashara wenye malori maeneo mbalimbali mkoani hapa hasa wilayani Rombo na Moshi Vijijini wanaouzunguka Mlima wanasaka magogo mabichi kwa hali na mali na kwenda kuyauza kiwandani hapo!
 
Halafu unakuta ni kiwanda ya waziri wa maliasili na utalii!

Huyu MUNGU tunayemlilia kila leo iko siku atajibu maombi yetu!
 
Ndio tatizo la kutokufanya environmental impacts assessment. Ni lazima mwenye kiwanda aweke bayana source ya raw materials, na sustainability ya supply.
You can post this kwenye website ya nemc ili waweze kuingilia kati.
 
Kile kiwanda ni mali ya watengenezaji wa konyagi tunajua wamiliki ni pamoja na serikali.
 
Dunia yote inaona JF. Hapa nadhani NEMC wameshaona tusubiri.
 
Kile kiwanda ni mali ya watengenezaji wa konyagi tunajua wamiliki ni pamoja na serikali.
Ach kulalamika wewe Kilimanjaro Biochem LTD sio ya Serikali inamilikiwa na Banco Products ya India na wanatengenza Ethanol na vile vile wanatoa ajira kibao kwa hiyo kama una utalaamu wa Chemistry na mambo ya Microbiology kachukue kazi,kuna mshikaji kachukua kazi kama Mwanakemia atakuwa anakula $ 8000kwa mwezi!
 
Huu mlima ndio tunaambiwa tuupigia kura za maajabu ya dunia?

Hali ya hewa kuzunguka Mlima Kilimanjaro imebadilika sana, kama kiwanda kinatumia magogo - tena mabichi basi hapo ndio mwisho wa huo mlima.
 
Itakuwa kichekesho sana kama walipewa leseni baada ya environment impact assessment wakati wamesema boilers zao zitatumia wood badala ya HFO au waste za viwanda vya miwa kuzalishia nishati inayohitajika kwa ajiri ya matumizi ya hicho kiwanda.
 
Leo nimekatiza.....hii kitu inatiririsha maji meusi sana kwenye vijito ambavyo vinatokea upande wa juu yake kutoka milimani,sijui kama maji haya meusi ni salama,maana hivi vijito vyote vinakusanyika na kukutana mbeleni upande wa chini na kupeleka maji mpaka bwawa la Nyumba ya Mungu........
 
nemc watatuma ujumbe, pia waziri wa mazingira , pamoja na waziri wa bia na viwanda Alhaji Dr Kigoda, kwani Alah hapendi uharibifu
 
Ach kulalamika wewe Kilimanjaro Biochem LTD sio ya Serikali inamilikiwa na Banco Products ya India na wanatengenza Ethanol na vile vile wanatoa ajira kibao kwa hiyo kama una utalaamu wa Chemistry na mambo ya Microbiology kachukue kazi,kuna mshikaji kachukua kazi kama Mwanakemia atakuwa anakula $ 8000kwa mwezi!

Ishu sio kutoa Ajira, wewe ni wawapi? Kwahiyo waharibu Mazingira kisa wanatoa ajira? Halafu kwenye mshahara hapo unatudanganya
 
Dunia yote inaona JF. Hapa nadhani NEMC wameshaona tusubiri.
Mmoja wa wakuu wa NEMC ana hisa ya asilimia 28 kiwandani hapo. So sijui kama atakubali lala na njaa kwa kelele zetu...!!
Nawasilisha.....
 
Ach kulalamika wewe Kilimanjaro Biochem LTD sio ya Serikali inamilikiwa na Banco Products ya India na wanatengenza Ethanol na vile vile wanatoa ajira kibao kwa hiyo kama una utalaamu wa Chemistry na mambo ya Microbiology kachukue kazi,kuna mshikaji kachukua kazi kama Mwanakemia atakuwa anakula $ 8000kwa mwezi!
mhh, mhindi akulipe zaidi ya mill 12 kwa mwezi????

atakuwa sio mhindi huyu au umekosea ulimaanisha mia 8 labda
 
Ach kulalamika wewe Kilimanjaro Biochem LTD sio ya Serikali inamilikiwa na Banco Products ya India na wanatengenza Ethanol na vile vile wanatoa ajira kibao kwa hiyo kama una utalaamu wa Chemistry na mambo ya Microbiology kachukue kazi,kuna mshikaji kachukua kazi kama Mwanakemia atakuwa anakula $ 8000kwa mwezi!
Nafikiri somo la mazingara hulijui sana unachojua ni ajira:Kumbuka ndg kuwa mazingira hainunulia bali hutunzwa nayo ikutunze Watu wengi wanaharibu mazingira kwa kilio cha riziki ya kila siku matokeo yake sasa njaa kila kunapokucha au mafuriko kwa wanaokaa bondeni au mlimani usiseme tambarare:
 
Back
Top Bottom