mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,753
- 7,075
- Thread starter
- #21
Mangi kama unampenda, mpe mawazo haya.Acheni kumuaribia Mangi
1. Yeye anamiliki mtaji atafute wataalum wenye uwezo wa kuendesha kiwanda kitaasisi sio kifamily.
2. Awe na HR. Na CEO,
3.Apunguze jaziba kunatokea sitomfahamu ili ajue vyanzo vya matatizo.
4. Aondoe kabisa janja ya kuwafanya wafanyakazi wote vibarua wengine akiwaahidi kuwaajiri baada ya test miezi kadhaa alafu anawafukuza.
5. Kila mtu asimamie anachokijua, sio mlinzi ndiye anakuwa makenika kwenye vifaa vya electronic.
6. Aeshimu haki za wafanyakazi wake kwani wakati mwingine akiwafukuza wakaduwaa anawatolea bastola.
7. Athamini uwezo wa wafanyakazi kazi wake sio kila mtu anaona analingana na mtu mwingine hadi kutumwa vitu visivyositahili kulingana na elimu.
8. Atambue kuwa mali na vitu vingine vyote kapewa na Mungu hivyo tunaishi kwa kutegemeana si kuwa na hela tu inatosha.