Kiwanda cha pombe Kali cha Mbundi mbundi Arusha chawatimua wafanyakazi 180 kwa mkupuo

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
547
1,000
Wafanyakazi zaidi ya 180 wa kiwanda cha kutengeneza kinywaji aina ya Mbundi mbundi kilichopo eneo la Unga limited jijini hapa,wamejikusanya mbele ya lango la kiwanda hicho wakimlalamikia mwajiri wako kwa hatua ya kuwaachisha kazi bila kufuata utaratibu na kukataa kuwalipa stahiki zao.

Wakiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya wenzao wafanyakazi hao,wamedai hawakutendewa haki na mwajiri wao kwani wengi wao wanazaidi ya miaka kumi wanafanyakazi bila kuwa na mikataba ya uhakika jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Aidha wamedai kunyanyaswa na afisa mwajiri wa kiwanda hicho,Juma Athumani ambaye amekuwa akiwatolea lugha chafu na kuwaambia wananuka jasho pindi wanapokuwa wakidai haki zao za msingi ikiwemo mikataba ya kazi.

Wamedai kuwa tarehe moja ,mwezi huu waliamua kujikusanya na kumfuata mwajiri wao kwa lengo la kutaka wapatiwe mikataba hata hivyo mwajiri huyo alikuwa akiwaporomoshea matusi makubwa jambo lililowalazimu kupeleka kilio chao ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,na kuonana na afisa tarafa ambaye aliwaamuru warejee kazini wakati ofisi yake ikilishughulikia suala lao.

Naye mkurugenzi wa kiwanda hicho,Dominick Nyabige alisema kuwa yeye kama mkurugenzi wa kampuni hiyo amefuata taratibu zote za kuwaachisha kazi ikiwemo kupeleka nakala ya barua, shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa viwandani( TUIKO)tawi la Arusha .

Wafanyakazi hao wanadai kuachoshwa kwa ujumbe wa simu za mkononi leo majira ya saa nne asububi na kwamba waliamua kujikusanya katika lango la kiwanda hicho wakitaka haki itendeke na wamemwomba,mkuu wa mkoa waa Arusha Mrisho,Gambo waziri wa viwanda .
IMG_20190211_163932.jpeg
IMG_20190211_180312.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
3,384
2,000
Huyo anayesema warudi kazini, ana uhakika watalipwa mishahara mwisho wa mwezi ukifika?
 
Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,882
2,000
Wafanyakazi zaidi ya 180 wa kiwanda cha kutengeneza kinywaji aina ya Mbundi mbundi kilichopo eneo la Unga limited jijini hapa,wamejikusanya mbele ya lango la kiwanda hicho wakimlalamikia mwajiri wako kwa hatua ya kuwaachisha kazi bila kufuata utaratibu na kukataa kuwalipa stahiki zao.

Wakiongea na vyombo vya habari kwa niaba ya wenzao wafanyakazi hao,wamedai hawakutendewa haki na mwajiri wao kwani wengi wao wanazaidi ya miaka kumi wanafanyakazi bila kuwa na mikataba ya uhakika jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Aidha wamedai kunyanyaswa na afisa mwajiri wa kiwanda hicho,Juma Athumani ambaye amekuwa akiwatolea lugha chafu na kuwaambia wananuka jasho pindi wanapokuwa wakidai haki zao za msingi ikiwemo mikataba ya kazi.

Wamedai kuwa tarehe moja ,mwezi huu waliamua kujikusanya na kumfuata mwajiri wao kwa lengo la kutaka wapatiwe mikataba hata hivyo mwajiri huyo alikuwa akiwaporomoshea matusi makubwa jambo lililowalazimu kupeleka kilio chao ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,na kuonana na afisa tarafa ambaye aliwaamuru warejee kazini wakati ofisi yake ikilishughulikia suala lao.

Naye mkurugenzi wa kiwanda hicho,Dominick Nyabige alisema kuwa yeye kama mkurugenzi wa kampuni hiyo amefuata taratibu zote za kuwaachisha kazi ikiwemo kupeleka nakala ya barua, shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa viwandani( TUIKO)tawi la Arusha .

Wafanyakazi hao wanadai kuachoshwa kwa ujumbe wa simu za mkononi leo majira ya saa nne asububi na kwamba waliamua kujikusanya katika lango la kiwanda hicho wakitaka haki itendeke na wamemwomba,mkuu wa mkoa waa Arusha Mrisho,Gambo waziri wa viwanda .
View attachment 1019924 View attachment 1019926

Sent using Jamii Forums mobile app
Poleni dada zangu. Mbona hao akina dada wasafi nadhifu na smart halaf unawatukana wananuka jasho.

Dah bongo survival for the fittest
 
Baba Heri

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
1,111
2,000
Mleta mada Hicho kiwanda kinaitwa Bhunu Mbundi na hakizalishi pombe kali kinazalisha aina ya pombe kama banana.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom