Kiwanda cha Nyama Shinyanga, ni usanii au deal imegoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiwanda cha Nyama Shinyanga, ni usanii au deal imegoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mgoyangi, May 28, 2008.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  May 28, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni zaidi ya Miezi 10 sasa hakuna kinachofanyika katika kiwanda cha Nyama tangu apatikane mwekezaji, kupitia ubia wa mwekezaji huyo na Mbunge wa Meatu, Salum Khamis, maarufu kama Salum Mbuzi miongoni mwa wapiga kura wake.

  Wafanyakazi waliorithiwa kutoka Tanganyika Parkers, mmiliki wa awali wa kiwanda hicho kupitia mfilisi, sasa wanapiga miayo kwa kuwa hakuna wanacholipwa na wanadai heri enzi hizo kuliko kuwa chini ya mwekezaji huyu.

  Kiwanda kina balaa, sababu hakijawahi kufanya kazi tangu kianze kujengwa miaka ya sabini mwishoni, kisa ufisadi, kwani, Mkandarasi alizidiwa kete, badala ya kuagiza yeye vifaa kama mkataba unavyodai, maafisa wa serikali waliagiza wao na kula cha juu, mkandarasi akachukia na kuamua kuondoka kabla ya kukamilisha ujenzi.

  Tangu wakati huo kiwanda kikawa hifadhi ya popo na nyoka, baadaye amekuja anayedaiwa kuwa mwekezaji ambaye hajafanya kazi yoyote hadi leo, na mambo yamekuwa mabaya zaidi, pengine kutokana na kukatwa mirija, ya kufyonza pesa kwa kisingizio cha uwekzaji, maana hata huyo mwekezaji ni mbongo mburushi kama alivyo partner wake Salum Mbuzi.

  Kilichokuwa kimetegwa hapa ni deal, sasa siyo wakati wake watanzania wameamka, na katika hili hakuna tena kinachoendelea. RIP Kiwanda cha Nyama Shinyanga.
   
 2. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  kwani kina salumu mbuzi wana uchungu na nchi yetu?hawa wao wanaangalia pesa tu!sasa wameshindwa kuendeleza kiwanda!fikiria pesa iliyotumika kujenga hicho kiwanda then kiwanda hakifanyi kazi!
  mimi nashangaa kwa nini hata tunawapa ubunge hawa waburushi?
   
 3. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wakiambiwa waje wazungu kuwekeza sisi hao hao na akina Mbuzi tunaanza kupiga kelele. Ndio tatizo letu hilo wabongo.
   
 4. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Projects kama hizi zilibatizwa jina la "Elephant Projects". Watu wanaanzisha miradi mikubwa wasiyoweza kumudu kuiendesha. Kwa kifupi, huu ni usanii tu.
   
 5. U

  Ufunuo wa Yohana JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 35
  Mirija baba ya kufyonzea pesa imekatwa...wafanyakazi watapiga miayo mpaka basi.....ndo wahindi hao wakina RA, Patel, Jeetu, wamekinga bakuli lao BOT likijazwa tu wanaita kampuni nyingine kutoka nje yenye uwezo wa kufanya hiyo kazi wanaipa 60% ya lile bakuli na wao wanatambaa na ile 40% canada.
   
 6. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hao hawarudi tena kwani wameshachota mipesa yao BOT na sasa wanazungusha kwenye miradi yao mingine. toka lini mburushi mnunuzi wa ngozi za Meatu aje auze Nyama nchi za nje? better call it WHITE ELEPHANT BISSNESS
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  May 28, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  ..mitambo haikununuliwa.

  ..mkandarasi hakukamilisha ujenzi.

  ..eneo likawa hifadhi ya nyoka na popo.

  ..hapakuwahi kufanyika uzalishaji wa aina yoyote.

  ..HAO WAFANYAKAZI WANATOKA WAPI, NA KWANINI WASTAHILI MALIPO?

  ..KWANINI TUNAITA ENEO HILO KIWANDA?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 28, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  labda wanahitaji watanzania kutoka nje ya nchi kwenda kuwaambia jinsi ya kufanya!
   
 9. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi najitolea kuwa mshauri wao lakini nitakuwa natoa ushauri nikiwa huku... free of charge (ili watu wakose 10%).
   
 10. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #10
  May 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kiwanda Hicho Kilijengwa Kwa Ushirikiano Na Kampuni Moja Inayoitwa Interconsult Ya Jijini Dar Es Salaam , Interconsult Pia Ilishirikiana Na G7 Kujenga Bot Dsm Na Znz

  Kazi Ipo
   
 11. A

  August JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli na Hili tunasubiri mpaka wahisani? au World Bank, IMF nk .
  Hivi Wabunge wa Shinyanga mkiachana na Hiyo Serikali Yenu Hamuwezi kufanya Kitu kwa Ajili ya Wananchi Wenu?
  Maana Pake Shirecu mlikuwa mnayachezeaga mapesa mengi tu? haya sasa mnapataga kama mrahaba nacho hamuwe kudundunduliza mkawekeza kwenye Chiwanda cha Nyama? Au mnasubiri Chifu Mkwaia aseme ? Au mpaka Pasco, Julius aka Nyani Ngabo? na wengineo wa JF walalamike?


  Date::12/17/2008
  Uhai wa kiwanda cha nyama Shinyanga bado mashakani[​IMG]Na Julius Sazia, Shinyanga
  Â
  MATUMAINI ya kufufuka na kuanza kwa uzalishaji kwa kiwanda cha nyama cha Old Shinyanga cha mkoani hapa yameanza kutoweka baada ya mwekezaji aliyekichukua kiwanda hicho, kutoonekana.
  Â
  Kiwanda hicho, kilichojengwa mwaka 1975 chini ya Tanganyika Packers, hakijawahi kuzalisha hata mara moja licha ya mitambo yake kuwepo na kuwa katika hali nzuri.
  Â
  Â Hayo yalibainishwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa, RCC, kilichofanyika mjini Shinyanga jana.
  Â
   Alisema mwekezaji huyo, Tripple S, kutoka Texas nchini Marekani, alifuata utaratibu wote wa kisheria wa kukichukua kiwanda hicho na kusaini mkataba na alitarajiwa kuanza uzalishaji kabla ya mwisho wa mwaka huu, lakini hadi sasa hajaonekana na hakuna mawasiliano naye.
  Â
  ''Matumaini ya kiwanda kuanza uzalishaji yamepotea... nilifuatilia Wizara ya Mifugo na wao wakasema hawajawasiliana naye na hapa Shinyanga hatumuoni na baadhi ya vifaa vimeanza kuibiwa," alisema.
  Â
  Â Katika hatua nyingine mbunge wa Bariadi Mashariki, John Momose Cheyo ameilaumu serikali kwa kuwanyasanya wafugaji wanaosafiri na makundi ya mifugo wakitafuta malisho.

  Â Alisema wafugaji hao hawapendi kufanya hivyo bali ni kutokana na hali ya malisho kuwa haba kwenye maeneo wanayotoka na kushauri kuwa serikali ingechukua jukumu la kufanya uchunguzi wa sababu zinazowafanya wahame na kuzitatua badala ya kutumia njia za ubabe kuwazuia.
  Â
   ''Tumejenga chuki dhidi ya mifugo, hali hii siyo nzuri, wafugaji wasibughudhiwe wanaposafirisha mifugo yao, wananyanyaswa mno njiani kwa rushwa katika kila kituo wanapopita," alisema.
  Â
  Naye mbunge wa Maswa, John Shibuda alipendekeza kuundwa kwa chama cha wafugaji wa ng'ombe nchini kitakachokuwa na haki sawa na vyama vingine kama vya wafanyakazi au walimu, ili na wao waweze kupata sehemu ya kutolea shida na kero zao.   Awali akiwasilisha taarifa ya mifugo mkoani Shinyanga, mshauri wa mifugo wa sekretarieti ya mkoa, Chamatata B.A, alisema mkoa wa Shinyanga una ng'ombe zaidi ya milioni 2 na kwamba katika kipindi cha mwaka 2007/2008, wafugaji walipata zaidi ya shilingi 30 bilioni 30 baada ya kuuza mifugo yao kwenye minada 34. Â
  Tuma maoni kwa Mhariri
   
Loading...