Kiwanda cha miwa cha Mkulazi ni kilio kwa wananchi

kimbilioletu

Member
Jun 9, 2020
12
22
Habari!

Hiki ni kiwanda cha miwa cha mkulazi(Mbigili).

Hapa kiwandani baadhi ya miwa imekomaa lakini kiwanda haifahamiki kitaanza lini usindikaji.

Ni kiwanda ambacho kipo wilaya ya Kilosa, ujenzi wake unasuasua sana.

Miwa mikubwa.jpg

Baadhi ya miwa ikiwa tayari kuvunwa lakini kiwanda hakieleweki.

Rais Magufuli aliiagiza benki ya Azania kuwapa mikopo wakulima wa nje(outgrowers) kupitia vyama vyao vya ushirika(AMCOS). Azania benki ilitoa pesa hapo awali lakini sasa imegoma kuendelea kutoa pesa kwa vile kiwanda hakieleweki.

Mbaya zaidi wakandarasi waliotoa huduma ya kulima, kusambaza mbolea, madawa na mahitaji mengine hawajalipwa mpaka sasa.

"Maisha yamekuwa magumu sana, pesa zetu hatulipwi na mimi nilikopa benki baadhi ya mtaji wangu".......alisikikaa mmoja kati ya wakandarasi.

"Nilitoa shamba langu kwa ajili ya kulima miwa, tuliambiwa ina faida sana kuliko mpunga, mpaka leo miwa inadumaa tukiwafuata Amcos wanatuambia Azania hawataki kutoa pesa mpaka kiwanda kikamilike".........alisikika mmoja kati ya wakulima wadogo wadogo.

Baadhi ya wakandarasi wamejaribu kuonana na waziri Jesta Muagama bila mafanikio.

Ndugu yangu hawa wanasiasa wa serikali hii ni hatari sana kwa maisha yetu, wanakuja hapa wanatuambia limeni tu kiwanda kitaanza kazi punde, tunawapa kazi makampuni ya kulima tukienda benki wanasema hatutoi pesa mpaka kiwanda kikamilike"......alisikika mmoja kati ya viongozi wa Mbigiri-Amcos.
Kimsingi hali ni mbaya sana hapa ila watu wanaogopa kupaza sauti. Kila mmoja akiambia iki ni kiwanda cha rais Magufuli anaogopa kupaza sauti kwa hofu ya kuambiwa anamchonganisha Rais na wananchi.

"Tuliambiwa rais Magufuli angekuja mwezi wa Januari mwaka huu ili kukifungua kiwanda, mpaka leo mwezi wa sita kimya. Hali ni mbaya kwelikweli umasikini unazidi kutujaa ni bora tungelima mpunga tu"........mkulima alilalamika lakini alihofu kutaja jina lake.

Chanzo chetu cha habari kilijaribu kuuona uongozi wa Azania benki na majibu yao yalikuwa yaleyale....HAWATOI PESA MPAKA KIWANDA KIKAMILIKE.

"Rais anapaswa kuingila kati ili atuokoe sisi wakandarasi maana toka mwezi wa 12 mwaka jana hatujalipwa pesa zetu na benki na taasisi tulizokopa pesa wanaanza kuuza dhamana zetu tulizoweka".....mmoja kati ya wakandarasi alizidi lalamika.
 
Hii investment ilikuwa ya NSSF na washirika wake I.e pension Funds ambazo ndiyo wamiliki au shareholders wa Azania Bank. Changamoto ipo hasa hizi merging za Pension Funds bado mambo hayajatengamaa. . Poleni wakulima.
Kuna baadhi ya wakulima waliacha kulima mpunga wakalima miwa, muda huu hali zao ni mbaya sana, hawana hata chakula.
 
Hii investment ilikuwa ya NSSF na washirika wake I.e pension Funds ambazo ndiyo wamiliki au shareholders wa Azania Bank. Changamoto ipo hasa hizi merging za Pension Funds bado mambo hayajatengamaa. . Poleni wakulima.
Pensions funds waache siasa waende kwenye actions ,watafute an EPC company ajenge awakabidhi. Tatizo hapo unaweza ukakuta kujengwa kwa kiwanda kunacheleweshwa na watu wachache wanaotala percent fulani. Let us wake up, watu tufanye kazi kwa kujitoa bila kuangalia hizo faida binafsi ila tuweke uzalendo mbele kwanza
 
Management ilisavunjwa ikawekwa nyingine, but up to know nothing is going on.
 
Pensions funds waache siasa waende kwenye actions ,watafute an EPC company ajenge awakabidhi. Tatizo hapo unaweza ukakuta kujengwa kwa kiwanda kunacheleweshwa na watu wachache wanaotala percent fulani. Let us wake up, watu tufanye kazi kwa kujitoa bila kuangalia hizo faida binafsi ila tuweke uzalendo mbele kwanza
Well said. Ila pia kuna kasumba kwa viongozi wanapobadilishwa huwa viongozi wapya wa kiitanzania hawatii kipaumbele miradi waliyoikuta. Yaani mingi hufa. NSSF sasa yuko William Erio ambaye alichukua kijiti kwa Prof. Godius Kahyarara ambaye ni mchumi na alikuwa ontop ya project ya Mkulazi Sugar industrykupitia Mkulazi Holding Company. Sasa William Erio Mwanasheria sijajua idara yake ya investments. Lakini pia hizipension funds ziko hoi kabisa financially na sasa kwa private sector COVID imeshusha sana mapato maana retrenchment na nusu mishahara imetembea sana.
 
Back
Top Bottom