Kiwanda cha Mabomba cha PLASCO suluhisho la Maji nchini

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kampuni ya kutengeneza Mabomba ya Plastiki ya maji safi na maji taka ya PLASCO LTD ya jijini Dar es salaam, imejipanga kushirikiana na wadau wa sekta ya maji nchini kuhakikisha inatengeneza mabomba madhubuti yenye uwezo wa kuhifadhi na kupitisha maji na hivyo kuondoa dhana ya mabomba kuharibika kwa kutoboka kila wakati.

Afisa Mwendeshaji wa kiwanda hicho,Alimiya Osman alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikizalisha mabomba hayo ya maji yenye uwezo mkubwa duniani katika kuhimili aina yoyote ya udongo Ardhini, kuhifadhi na kupitisha maji kwa muda mrefu bila kuharibika kirahisi

Alisema teknolojia inayotumika kutengeneza mabomba hayo inatumika koteduniani hivyo kuwataka wadau wa maji nchini kuhakikisha wanashirikiana na wadau hao wa maji katika kukambiliana na changamoto za maji katika kuboresha huduma za maji nchini.

Alisema kuwa ili kufanikisha suala zima la utoaji huduma wanasisitiza serikali na wadau wa maji kuangalia matumizi ya fedha wanazopata kwa kununua bidhaa madhubuti za viwanda vya hapa nchini ili kuongeza wigo wa mapato na kupunguza tatizo la ajira.


Naibu katibu Mkuu wizara ya Fedha,Mhandisi, Antony Sanga imezitaka Mamlaka za Maji nchini, kuhakikisha zinatafuta fedha ikiwemo kukopa kwenye mabenki kwa riba nafuu ili kujenga miradi mbalimbali ya maji itakayowafikia wananchi kwa gharama nafuu.

Akiongea kwenye warsha ya siku tatu,inayofanyika jijini Arusha ,Mhañdisi Sanga amesema kuwa warsha hiyo imelenga kutafuta fedha ili kuendesha miradi mbambali ya maji mjini na vijijini

Katika hatua nyingine ,Mhandisi Sanga amesema kuwa serikali kupitia wizara ya maji inatekeleza miradi mikubwa ya maji ipatayo 1947 kupitia wakandarasi mbalimbali ambapo miradi hiyo ikikamilika kwa wakati itafanikisha adhima ya serikali ya kumtua mama ndoa ya maji kichwani

Ends..
 
Back
Top Bottom