Kiwanda cha kutengeza manukato bandia chakamatwa

Jongwe

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
1,040
662
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamegundua na kukifungia kiwanda bubu cha kutengenezea vipodozi bandia jamii ya manukato eneo la Tuangoma Kigamboni nyumbani kwa mtu na kumshikilia mmliki wa nyumba hiyo kwa mahojiano zaidi.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA Bw. Hiiti Silo pamoja na kuainisha bidhaa hizo kuwa hatari kwa afya za binadamu amesema hatua hiyo inafuatiwa kukamatwa kwa maduka ya mfanya biashara mmoja eneo la sinza jijini Dar es Salaam akiwa na shehena ya bidhaa hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja zikiwa na vifungashio vya kuzalishwa nchini uturuki.

Aidha katika heka heka za maofisa wa TFDA na Polisi kukamatwa kiwanda hicho mmiliki wa nyumba hiyo aligoma kuongea lolote kuhusu uzalishaji bidhaa hizo kabla ya kubebwa na kupelekwa polisi kwa mahojiano.
 
Kupitia channel ten taarifa ya saa moja usiku, wametangaza na kuonyesha kiwanda ambacho kimekuwa kikitengeneza manukato (perfume) bandia aina ya 'same' na kuziweka vibandiko vya kuwa bidhaa hiyo imetoka ufaransa na zingine uturuki. Kiwanda hicho kipo ineo la Toangoma wilaya ya Temeke
Chakamatwa??
 
Viwanda bandia viko vingi sana kwenye makazi ya watu!

Hakika..ila jamaa hawa wa TFDA muda mwingi wanafanya show off tu, kuna jamaa mtaani kwetu anatengeneza tomato sauce zisizo na kiwango , hawajamaa walikuja na waandishi wa habari ikarushwa huku na kule kujigamba wamefanikiwa kumnyaka huyu jamaa. Wakafunga mtambo wa huyo jamaa. . Wiki tu uzalishaji ukaanza kama kawaida.
 
Back
Top Bottom