Kiwanda Cha Karatasi Mufindi Serikali Imekuza Kwa Nani

PENDING'ULA

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
268
46
Katika Tanzania ya leo ambamo Watanzania tumeanza kuzishitukia nyendo za uuzaji na umilikishaji wa rasilimali zetu kwa wageni limenijia wazo kutaka kujua mchakato mzima wa kukiuza kiwanda cha karatasi Mgololo. Je Serikali yetu imekiuza kwa nani!Je haiwezekani mambo ya Ki-Richmond kuwa yamefanyika pia hapa?
 
Nianze kwa kukupongeza PENDING’ULA kwa kuiibua hoja hii, ingawa naamini kuwa haitavuta hisia za watu wengi, kutokana na kiwanda hicho kutofahamika vizuri na kutogusa maisha ya wengi moja kwa moja, kama ilivyokuwa kwa TANESCO na RICHMOND; ukiondoa wale watu wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini kilipo kiwanda hicho na wale ambao ama hupita jirani wakiwa katika safari kwa treni ya TAZARA ama wamewahi kufanya kazi, au kutoka jasho wakati wa ujenzi wake, au kunufaika kwa namna moja au nyingine na huduma zitolewazo na kiwanda hicho.

Ili kuvuta hisia za wengi ufafanuzi wa kina unahitajika ili kuona jeuri ya kifisadi kama ilitumika katika kukiuza kiwanda hicho, au kama ulivyoita mwenyewe – URICHMOND kama upo.

Napenda kukupanua mawazo kwa kukupa baadhi ya taarifa ninazozijua kuhusiana na kiwanda hicho. Na kwa kifupi taarifa hizi pia zinachangia kuongeza shaka kwamba huenda kimeuzwa kifisadi au ni CHAO wakubwa Fulani!

Kwa mujibu wa CERTIFICATE OF INCENTIVES ambayo hutolewa kwa mujibu wa Ibara ya 17 ya sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 chini ya kanuni na masharti yaliyomo katika vifungu vya 14 na 15 vya sheria hiyo, iliyotolewa tarehe 19 Aprili 2004 na kupewa namba 040806, inatoa mchanganuo wa wenye hisa, utaifa na viwango vya hisa kama ifuatavyo:

SHAREHOLDERS NATIONALITY SHAREHOLDING
Angel Hurst Industries Ltd U. K 99.988%
Jaswant Singh Rai Kenyan 0.006%
Sabjit Singh Ra Kenyan 0.006%.

Kwa takwimu hizo ndugu wawili akina – Rai ambao ndio kwa sasa wanaitwa wenye kiwanda, wanamiliki jumla ya asilimia 0.12 tu, ya hisa zote za kiwanda. Aidha mwenye pande kubwa la 99.988% hajawahi kuonekana katika eneo la kiwanda wala mwakilishi wake wa kusimamia shughuli za kila siku za uendeshaji wa kiwanda licha ya kuwa na hisa kubwa namna hiyo, hali inayomfanya mwenye hisa kiduchu kuwa na maamuzi makubwa ya kiutendaji; na nathubutu kusema hakuna anayemjua hata miongoni mwa wafanyakazi, ingawa hao akina Rai wanafahamika vizuri kwao! Kwa dokezo hilo ni jukumu lako PENDING’ULA kumtafuta umjue Angel Hurst Industries Ltd ni kampuni ya namna gani, kweli ipo au ndio ki-Richmond – Richmond, staili ambayo ina umaarufu wa aina yake miongoni mwa mafisadi wa ki-TZ, kujichotea mabilioni ya walala hoi na waamka hoi wa nchi hii, kama ilivyothibitika katika sakata la ufisadi kwenye akaunti ya EPA, RICHMOND na pengine hata hii!

Nimalizie kwa kukuahidi takwimu zaidi juu ya thamani halisi ya kiwanda (Book Value) wakati wa mauziano, raslimali zilizokabidhiwa kwao na kiasi kinachodaiwa kulipwa kama gharama za uuzwaji ili uone kama kweli kuna uwiano au la, au pengine akina Mkapa, waumini wakubwa wa sera ya ubinafsishaji na ambao walisimamia kucha kuitekeleza, wamekitenga kwa ajili ya kujilipa “PENSHENI” kimtindo!
 
Asante sana Mpulikage kwa mchanganuo wako mzuri. Naomba kwa nafasi hii tena msaada wa kumtafuta Angel Hurst Ind. of U.K Naamini kwa utafiti wa majibu yako ya awali ambayo nathubutu kuyaita ya kina,hutashindwa kumpata huyo nae pia. Nawaomba pia wasomaji watakaoipitia habari hii wenye uwezo wa kunichangia uelewa wao ili mimi pamoja na wenzangu wakereketwa wa uporaji wa mali ya umma tupate hoja za kuwauliza wakubwa hawa.
 
Nianze kwa kukupongeza PENDING’ULA kwa kuiibua hoja hii, ingawa naamini kuwa haitavuta hisia za watu wengi, kutokana na kiwanda hicho kutofahamika vizuri na kutogusa maisha ya wengi moja kwa moja, kama ilivyokuwa kwa TANESCO na RICHMOND; ukiondoa wale watu wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini kilipo kiwanda hicho na wale ambao ama hupita jirani wakiwa katika safari kwa treni ya TAZARA ama wamewahi kufanya kazi, au kutoka jasho wakati wa ujenzi wake, au kunufaika kwa namna moja au nyingine na huduma zitolewazo na kiwanda hicho.

Ili kuvuta hisia za wengi ufafanuzi wa kina unahitajika ili kuona jeuri ya kifisadi kama ilitumika katika kukiuza kiwanda hicho, au kama ulivyoita mwenyewe – URICHMOND kama upo.

Napenda kukupanua mawazo kwa kukupa baadhi ya taarifa ninazozijua kuhusiana na kiwanda hicho. Na kwa kifupi taarifa hizi pia zinachangia kuongeza shaka kwamba huenda kimeuzwa kifisadi au ni CHAO wakubwa Fulani!

Kwa mujibu wa CERTIFICATE OF INCENTIVES ambayo hutolewa kwa mujibu wa Ibara ya 17 ya sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 chini ya kanuni na masharti yaliyomo katika vifungu vya 14 na 15 vya sheria hiyo, iliyotolewa tarehe 19 Aprili 2004 na kupewa namba 040806, inatoa mchanganuo wa wenye hisa, utaifa na viwango vya hisa kama ifuatavyo:

SHAREHOLDERS NATIONALITY SHAREHOLDING
Angel Hurst Industries Ltd U. K 99.988%
Jaswant Singh Rai Kenyan 0.006%
Sabjit Singh Ra Kenyan 0.006%.

Kwa takwimu hizo ndugu wawili akina – Rai ambao ndio kwa sasa wanaitwa wenye kiwanda, wanamiliki jumla ya asilimia 0.12 tu, ya hisa zote za kiwanda. Aidha mwenye pande kubwa la 99.988% hajawahi kuonekana katika eneo la kiwanda wala mwakilishi wake wa kusimamia shughuli za kila siku za uendeshaji wa kiwanda licha ya kuwa na hisa kubwa namna hiyo, hali inayomfanya mwenye hisa kiduchu kuwa na maamuzi makubwa ya kiutendaji; na nathubutu kusema hakuna anayemjua hata miongoni mwa wafanyakazi, ingawa hao akina Rai wanafahamika vizuri kwao! Kwa dokezo hilo ni jukumu lako PENDING’ULA kumtafuta umjue Angel Hurst Industries Ltd ni kampuni ya namna gani, kweli ipo au ndio ki-Richmond – Richmond, staili ambayo ina umaarufu wa aina yake miongoni mwa mafisadi wa ki-TZ, kujichotea mabilioni ya walala hoi na waamka hoi wa nchi hii, kama ilivyothibitika katika sakata la ufisadi kwenye akaunti ya EPA, RICHMOND na pengine hata hii!

Nimalizie kwa kukuahidi takwimu zaidi juu ya thamani halisi ya kiwanda (Book Value) wakati wa mauziano, raslimali zilizokabidhiwa kwao na kiasi kinachodaiwa kulipwa kama gharama za uuzwaji ili uone kama kweli kuna uwiano au la, au pengine akina Mkapa, waumini wakubwa wa sera ya ubinafsishaji na ambao walisimamia kucha kuitekeleza, wamekitenga kwa ajili ya kujilipa “PENSHENI” kimtindo!
Binafsi by any means nitapambana na hili jipu mpaka magufuli alitumbuwe
 
Hii nchi bwana. Kuna watu wanapaswa wauawe kwenye public, huku familia zao zikitazama.
 
mkuu, sheria bado hazjaweka hukumu ya kifo au kifungo cha maisha kwa mafisadi.

wabunge hawawezi kutunga sheria kali za ufisadi kwa sababu wao ndio vnara wa kutoa rushwa ktk uchaguzi na wapokeaji wazuri wa rushwa kutoka ktk taasisi zingne....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom