Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Siku moja baada ya kiwanda cha kusindika minofu ya samaki cha Kagera Fish kilichopo eneo la Kemondo mjini Bukoba kutozwa faini ya shilingi milioni kumi kutokana na kutiririsha majitaka ndani ya Ziwa Victoria, kiwanda kingine tena cha Kagera sugar mkoani humo nacho kimepigwa faini ya shilingi milioni 10 kwa kosa la kutiririsha maji taka kwenye mto Kagera.
Adhabu hiyo imetolewa na Naibu waziri wa nchi,Ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Mh. Luhaga Mpina, baada ya kiwanda hicho kukiuka sheria ya mazingira namba 20 ya mwaka 2004 na kanuni za ubora wa maji za mwaka 2007,kwa kutirisha maji yanayoingia kwenye mto Kagera yanayodaiwa kutokidhi viwango vya ubora, ambapo kimeagizwa kuchukua hatua za kuboresha mfumo wa ardhi oevu inayochuja maji hayo yanayotiririka.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera Godfrey Mheruka amesema faini ya shilingi milioni 10 dhidi ya kiwanda cha sukari Kagera ambacho kinatoa ajira kwa wananchi zaidi ya 5000 ni fundisho kwa viwanda vingine vinavyoendelea kukiuka sheria ya mazingira inayokataza uchafuzi wa mazingira nje ya viwango vilivyowekwa huku Meneja usafirishaji wa kiwanda hicho Vicent Mtaki akimueleza Naibu Waziri Mh. Mpina mchango wa kiwanda hicho kwa wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya hapa nchini katika kufanya majaribio.
Naibu waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira Mh. Luhaga Mpina amehitimisha ziara yake mkoani Kagera kwa kushiriki zoezi la usafi wa mazingira kwenye soko kuu la mjini Bukoba, kutembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha ammiminza, kuona shughuli za hifadhi ya mazingira katika msitu wa kupandwa wa rubale, kukagua mabwawa ya kutibu majitaka yaliyojengwa na mradi wa LVEMP awamu ya pili kwa ufadhili wa Benki ya dunia kwa gharama ya shilingi bilioni 2 katika kijiji cha Kyakairabwa pamoja na dampo la takataka la manispaa ya Bukoba lililopo kata ya Nyanga.
Chanzo: ITV