Kiwanda cha dhahabu chaanza uzalishaji, Dubai yahamia Tanzania

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Kiwanda kikubwa Afrika ya mashariki na kati cha kuchenjua dhahabu kilichopo jijini Mwanza kimeanza udhalishaji rasmi kuifanya Dubai ihamie Tanzania rasmi kwenye suala zima la biashara ya dhahabu.

Kiwanda hicho kilichozinduliwa na rais Samia mnamo tarehe 13/06/ 2021 kimetajwa kuwa na manufaa makubwa kwa watanzania kwa kutoa ajira pia kuwarahisishia wafanyabiashara wa madini kutoka nchi mbalimbali kuja Tanzania badala ya kwenda Dubai kama ilivyokuwa zamani.

Ikumbukwe pia ujenzi wa kiwanda hiki ulipingwa sana na Tundu Lisu pale aliposema watanzania tukijaribu kuthibiti biashara ya madini tutashitakiwa MIGA.

Kinaajiri wangapi, operating costs ni kiasi gani na kinaingiza kiasi gani ?

Ni bora sisi kama wadau (wananchi tukajua hayo)..., sababu naona kushoto mnasema mambo poa kila kitu shwari pesa inaingia alafu kulia mambo magumu fungeni mkanda hivyo Tozo zinaongezeka...
 
Hongera Tanzania.
Hongera Hayati Joseph Magufuli kwa mradi wenye tija kiasi hicho.
Tanzania ni yetu sote tuisemee na kuiombea Mema daima.
Pale mpigania legacy anapojitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuliepuka jina la kiongozi fulani......eti kwa hoja ya uoga tu na wivu!!
 
Magufuli alie kijenga mbona hajapewa credit kwenye hii mada?, na anapewa mfunguaji tu. Ama kweli asie kuwepo na chake hakipo.

Lunatic
 
Tukiazima wazungu waje watawale hapo tutapiga hatua kimaendeleo, kwa viongozi waliopo wanaodeal na minor issues na kujimwambafy maendeleo hakuna,mnapiga hatua mbili mbele mnarudi hatua mia nyuma
 
Magufuli alie kijenga mbona hajapewa credit kwenye hii mada?, na anapewa mfunguaji tu. Ama kweli asie kuwepo na chake hakipo.

Lunatic
Kuna kazi alifanya JK,mbona magufuli alisemaga yeye ndiye amefanya,ALIYEPO MADARAKANI NDIYE MTENDAJI MWENYEWE HUYO NA NDIYE AMEFANYA YOTE.
 
Magufuli alie kijenga mbona hajapewa credit kwenye hii mada?, na anapewa mfunguaji tu. Ama kweli asie kuwepo na chake hakipo.

Lunatic
Yani kuna watu mpaka leo bado hamuamini kama Magufuli keshakufa?Hata daraja la mfugale,kijazi na daraja la kigamboni,STDG process zilianza na utawala uliopita lakini zikamaliziwa na cha roho mbaya,tatizo lipo wapi hiki kiwanda cha dhahabu ikawe nongwa credit kwenda kwa mama Samia?
 
Tulia dawa ikuingie nini
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom