Kiwanda cha Chai Mufindi cha Unilever chasimamisha shughuli zake

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,338
Ni kufuatia kwa kifo cha mfanyakazi aliyepigwa na radi kiwandani hapo na kusababisha sintofahamu juu ya usalama wa wafanyakazi wa kiwanda hicho. Kifo cha mfanyakazi huyo kilisababishwa na mvua zilizonyesha kwa muda mfupi zilizoambatana na radi ambapo hakuwa maeneo salama ya kujikinga na radi ndipo alipopatwa na umauti.

Kufuatia tukio hilo kiwanda cha Mufindi na kile cha Njombe kimesimamisha shughuli zake kwa mda usiojulikana kupisha uchunguzi wa tukio hilo.

Katika hali nyingine wafanyakazi wa kiwanda hicho wamelalamikia kutokuwa na maslahi mazuri na mikataba ya kuridhisha, mmoja wa wafanyakazi hao alisema huchuma chai katika mazingira magumu na mshahara ni mdogo unaoanzia 100,000 na kuendelea huku ukijumuisha pesa ya kujikimu na ya kodi ambapo inawalazimu kulala katika mabanda wanayolipa kiasi cha Tsh 10,000 hadi 20,000 kwa mwezi.

Aidha ameongeza kuwepo kwa unyanyasaji kingono unaofanywa na viongozi wa juu wa kiwandani hapo kwa mda mrefu na wengine kukosa kazi ama kufukuzwa pale wanapokataa kutembea na mabosi hao.

Tunaamini serikali yetu sikivu itafuatilia masuala hayo.

Nakupenda nchi yangu Tanzania.
 
Back
Top Bottom