SoC03 Kivuli cha mtoto wa kike kinavyoathiri malezi na ndoto za mtoto wa kiume

Stories of Change - 2023 Competition

nobility

New Member
Jun 3, 2023
1
1
Na Norberth Saimoni

hero-16415-exp-2022-10.jpg

Chanzo:NSPCC

Usawa wa kijinsia ni agenda ya nchi nyingi ulimwenguni ambayo inajumuisha hatua na jitihada mbalimbali zinazolenga kuhakikisha kunakuwa na ulinganifu baina ya mwanaume na mwanamke katika nyanja zote kijamii,kisiasa,kiuchumi na kitamaduni. Jitihada hizi zimekuwa zikifanywa na jamii kwa ujumla, asasi mbalimbali za kiraia na binafsi zinazolenga kumsaidia mtoto wa kike kukua katika malezi bora,kumlinda dhidi ya hatari zozote katika ukuaji wake ili kuzifikia ndoto zake. Jitihada hizi zimefanya mtoto wa kiume kutengwa, kusahaulika na kutokuwa karibu na watu ambao wangekuwa nae bega kwa bega katika makuzi yake hivyo kukutana na changamoto nyingi ambazo humuathiri katika ukuaji wake na kubadili hata kesho yake lakini anakosa msaada kwani siyo kipaumbele cha jamii na asasi mbalimbali zinazolinda na kusaidia haki na usalama wa watoto.

Jamii inamtazama mtoto wa kiume kama mwanaume, asiyekutana na changamoto au anaweza kuzikabili changamoto zozote peke yake bila kujali kuwa katika umri wake mdogo anakumbana na changamoto nyingi pia ambazo kama mtoto anahitaji msaada wa jamii katika kuzivuka na kufikia ndoto zake. Katika familia nyingi mtoto wa kiume anaaminishwa kuwa hatakiwi kulia hata kama anachangamoto, hiyo inafanya mtoto kukua akiamini kulia na kuonesha kuwa unakumbana na changamoto fulani ni kuonesha udhaifu hivyo hukaa kimya bila kuwa na mtu wa kumsimulia anayopitia na mwisho athari hasi ndizo huonekana akiwa mtoto au hata anapofikia utu uzima na athari hizi huonekana katika matukio mbalimbali ambayo hujumuisha kujiua au tatizo la afya ya akili kwani hukaa na changamoto nyingi bila kuwa na mtu wa kumsimulia au kumsaidia.

Mtizamo huu unafanya jamii kuwekeza na kuwa karibu na mtoto wa kike na changamoto zake anazokutana nazo katika jamaii,familia na katika masomo yake na ukimtelekeza mtoto wa kiume bila kuwa na mtu wa kumshika mkono na kumvusha katika changamoto anazokutana nazo ambazo hupelekea kuanguka na kutofikia ndoto zake.

CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO MTOTO WA KUUME NA ATHARI ZAKE.
Katika siku za hivi karibuni mtoto wa kiume kama ilivyo kwa mtoto wa kike amekuwa akikumbana na changamoto kubwa katika ukuaji wake ambayo ni unyanyasaji au ukatili wa kijinsia. Mtoto wa kiume amekuwa akikutana na unyanyasaji wa kijinsia katika mazingira tofauti tofauti,katika familia,shuleni na katika jamii pia,ndugu wa karibu wamekuwa hatari katika ukuaji wa mtoto wa kiume kwa kumfanyia mambo maovu na kumtisha asimwambie mtu na hukaa kimya kwakuwa jamii ipo mbali nae.

e6f16d8a-ab6a-46dd-a381-bd8380692159.png

Chanzo: Vikaspedia

Baadhi ya shule pia zimekuwa sehemu hatari kwa malezi ya mtoto wa kiume kwani zimekuwa ni sehemu ambazo mtoto hufundishwa mambo mengi mabaya na maovu pia kama kulawitiwa na mapenzi ya jinsia moja na imekuwa sababu kubwa hata wanapofikia utu uzima kujiingiza katika wimbi la mapenzi ya jinsia moja yote ni kutokana na kukutana na mazingira hayo wakati wa ukuaji wao lakini walikosa mtu wa kumsimulia na kumshika mkono kumuonesha njia sahihi.

watoto wa kiume wamekuwa wakianguka katika kuzifikia ndoto zao kielimu kutokana na mazingira magumu wanayowekewa na wazazi/walezi na jamii inayowazunguka kwani hatari zote huwakumba bila msaada. Mfano, kutembea umbali mrefu kuzifikia shule, kujihusisha katika shughuri za uzalishaji na kilimo badara ya kwenda shule, kutopata chakula wakiwa shule, pia kukosa vifaa muhimu kama daftari, peni na vitabu sambamba na sare za shule,hivyo wengi huishia kuingia mtaani ambapo huishia kujihusisha na makundi mabaya kama wizi, uporaji na matumizi ya madawa ya kulevya kwani usaidizi wa vifaa hivyo vya kielimu hutolewa kwa watoto wa kike tu na kumnyima fursa mtoto wa kiume bila kujali uhitaji wake wa huo usaidizi.

Pia athari za kisaikolojia kwa watoto wa kiume wanaokumbana na unyanhasaji wa kijinsia wanaokumbana nao wakati wa ukuaji wao zimekuwa zikiwakumba hata wanapokuwa watu wazima ambazo hupelekea kuwa na maamuzi yasiyo sahihi na tatizo la afya ya akili kutokana na kukua katika changamoto hizo. Mtoto wa kiume kuaminishwa kuwa hatakiwi kulia au kushirikisha watu changamoto anazopitia na jamii kutomjari anayopitia humuathiri hata anapokuwa mtu mzima wakati akipitia changamoto kubwa hubaki mpweke bila kuwa na mtu wa kumwelezea wala kuonesha kuwa kuna magumu anapitia kwani anaamini kuwa mwanaume kuinesha kuwa unapitia changamoto fulani ni udhaifu pia kukua bila kuona jamii ikimsaidia hufanya kuamini anatakiwa akabiliane nazo peke yake hivyo wengi huishia kujiua na wengine kupata changamoto ya afya ya kili pale mambo yanapo wazidia.

NINI KIFANYIKE KUMSAIDIA MTOTO WA KIUME NA CHANGAMOTO ZAKE?(SULUHISHO)

Jamii inapaswa kuwajari watoto n kuwalinda kwa kuzingatia taratibu nzuri za malezi na sheria zinazomlinda mtoto kufuatwa. Ni dhahiri kuwa katika mazingira ya sasa hatarishi kwa ukuaji na afya ya akili ya mtoto,jamii iwekeze nguvu pia katika kumtizama mtoto wa kiume ambaye amesahaulika na kumlinda dhidi ya hatari zotr zinazomzunguka na kujitokeza wakati wa ukuaji wake kwa kumsaidia kuzitatua changamoto zake na kumsaidia kuzifikia ndoto zake kama ilivyo kwa mtoto wa kiume ambao wote wapo katika umri mdogo hawajafikia uwezo wa kujitegemea katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Wazazi wanapaswa kujenga utamaduni wa kila siku wanaporudi majumbani kukaa na mtoto mmoja mmojakwa urafiki na kuongea nae kama kuna kitu au changamoto yoyote amekutana nayo katika siku husika, na kukumbusha ni zipi haki zake za msingi na upi wajibu wake katika jamii inayomzunguka kama mtoto wa kiume au kike,ni vitu gani hapaswi kuvifanya au kufanyiwa na mtu au mtoto mwenzake. Hii itamfanya mtoto kujua mipaka ya kimaadili kujua kipi hatakiwi kufanya au kumfanyia mwenzake na kipi hatakiwi kufanyiwa mtu mwingine,ambapo hurahisisha mtoto kutoa taarifa iwapo atapitia changamoto hivyo ni muhimu mzazi kujenga mazingira ya urafiki na mtoto na kawaida ya kukaa na kuongea nae ili iwe rahisi kuwekawazi changamoto anazokumbana nazo ili kumsaidia kukua katika maadili na usahihi kuzifikia ndoto zake.

istockphoto-1227501843-612x612.jpg

Chanzo: istockphoto

Jamii inapaswa kubadili mtizamo wa kimalezi na namna inavyomchora mtoto wa kiume na mtoto wa kike katika ukuaji wao.
Jamii itambue kuwa mtoto wa kiume anakutana na changamoto kubwa kama ilivyo kwa mtoto wa kike,hivyo inapaswa kuhakikisha inakuwa karibu nae kama ilivyo kwa mtoto wa kike katika ukuaji wao na kuwajengea mazingira wezeshi ili kukua vyema na kuzifikia ndoto zao,na hatimaye kujenga jamii yenye mtizamo chanya juu ya usawa wa kijinsia,malezi ya watoto,changamoto zao,na ukuaji wao.

Taasisi za kiserikali (kiraia) na taasisi binafsi zinazolinda na kutetea haki a watoto,ni wakati wa kutambua na kuzimulika kwa karibu changamoto
 
Back
Top Bottom