puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 940
- 1,847
Habari za muda huu wana Jf. Nimuda kidogo sijaandika chochote katika jukwaa hili zaidi ya kuwa msomaji na Mchangiaji mabandiko mbali mbali.
Mungu ni mwema ametupa nafasi ya kuona mwaka mwingine.
Tahadhali kwa nitakachokiandika hapa, hakina mahusiano na imani za kishirikina wala imani ya kidini kutoka upande wowote...zaidi ni vitu vinanitokea mithili ya ndoto ili hali inakuwa kama darasa kwangu na pengine kwa jamii nzima.
Silazimishi yoyote kuamini hili maana haupo ushahidi wa moja kwa moja zaidi ni mimi na nafsi yangu ndio imenifanya leo kuitoa siri hii nzito kuweka hapa jukwaani pengine inaweza kuwa msaada kwa watu wengine.
Mnamo tarehe 20 Jan 2022, majira ya saa 10 jioni, nilipata ajali mbaya sana ya pikipiki...nilikuwa naendesha mwenyewe nikiwa kwenye majukumu yangu ya kawaida.
Kiukweli ile ajali nilisababishiwa na coster ya abiria iliyokuwa inamkwepa n'gombe aliekuwa akikatiza barabarani ghafla. Hvy dereva wa coster akaacha njia nakuja kunivaa mimi.
Niseme wazi Mungu bado ananipenda kwa namna nilivyotoka mzima kwenye ile ajali kiukweli niliona kifo kinakuja mbele yangu kabla ya kunikalipia kikapotea. Kiufupi ndani ya dakika chache kama sio sekunde niliona giza Nene sana mithili ya kipofu (Sijawah kuwa mpofu ila hii ni nadharia tu) ghafla nikawa sisikii chochote toka nje ni kama mtu aliepooza na kiziwi ilibaki akilitu ya kunijulisha nini kinaendelea katika hali ya ghafla nikaanza kuona mwanga unakuja na kuongezeka ndipo nilipofungua macho na kuona rundo la watu wakiwa wamenizunguka nimelala kando ya barabara nikiwa nimepata majeraha kadhaa zaidi maumivu makali yalikuwa kwenye maeneo ya nyonga.
Nipo mkoa wa mwanza kwa miezi kadhaa sasa, nipo na kazi maalumu naifanya huku. Kama kuna mtu alipita kwenye page ya flora nitetee nafikiri ni kwenye Tiktok aliposti video ya n'gombe aliekuwa anatembea barabarani huku akiwa apishi magari...basi ng'ombe huyohuyo ndie alienisababishia mimi ajali maeneo ya National jirani na kituo cha polisi cha nyakato.
Namshukuru Mungu nilipelekwa hospital nikapata huduma na naendelea kuimarika siku hadi siku.
Kutokana na changamoto nilizowahi pitia huko nyuma ikiwemo na kile kisa cha jini nilichowah weka hapa jukwaani, imenifanya kuwa karìbu sana na Mungu....maombi yamekuwa mstari wa mbele katika maisha yangu kwa sasa.
Sasa usiku wa siku inayofuata baada ya ajali ambayo ilikuwa ni ijumaa...nikiwa katikati ya maombi mazidi ya kumshukuru Mungu kuniokoa na ile ajali mara ghafla nilipitiwa na usingi mzito ambao sikuweza kuhitisha maombi yale...jambo hili ndio limenufanya nirudi hapa leo.
Kiukweli nilikuwa nazungumza na mtu nisie muona ila jinsia atakuwa ni mwanaume kwa maana sauti yake ilikuwa ya kiume.
Ni kama alikuwa pembeni ya kitanda changu lakini nguvu za kufungua macho kumuangalia sikua nazo wakati huo ila nilikuwa namsikia vizuri anachoongea.
Ndugu zangu sio vifo vyote ni kudra za M/Mungu vingine ni hila za sisi binadamu. Kiufupi yule n'gombe sio wa kawaida kama watu wainavyo ni watu wanahitaji kafala zao hivyo ng'ombe ni kama sababu.. kilichotokea kwangu ni vita katika ulimwengu wa roho kati ya ushirikina na nguvu za Mungu.
Yote hayo niliambiwa na huyo mtu nisie muona sura, sasa kikubwa zaidi aliendelea kunieleza kama kifo kimemkuta mtu kwa ahadi za Mungu huwa kina dalili siku kadhaa kabla hakija tokea ambapo yeye alitafsiri kama kivuli cha kifo.
Ndugu zangu naomba nikomee hapa nutaendelea asubuhi maana issue ni ndefu kidogo...ila mkae mkijua kila mwanadamu anao uwezo wa kujua majira ya ukomo wa maisha yao (Kifo) Sio kwa siku halisi lkn ni kama unavyoona utoto/ujana/utuuzima na uzee.
Yapo mambo kadhaa ukiyafanya waweza kuona ukomo wa kivuli chako. Hivyo kama maisha yako yataishi ujanani itakuwa hivyo na haitobadilika hali kadhali na hayo makundi mengine ya rika.
Inahitaji kuwa jasiri katika hilo, hii ni zaidi ya majibu ya HIV, ni wachache sana hupata bahati ya kujua siri hii ila ndio uhalisia ulivyo.
Nikirudi nitaeleza vingi kuhusu hii issue na haikuwa ndoto ya siku moja maombi ndio yalikuwa ni kama call ya kumuita huyo bwana nisie mjua hata kwa kumuona zaidi ya kusikia sauti.
Natanguliza shukrani