Kivuli cha dude kubwa cha kutisha kinanisumbua usiku

Habari zenu wadau wote wa JF,

Nimepata tatizo ambalo silielewi, kwa muda mrefu nimekuwa nikiona kivuli cha mtu cheusi nikigeuka kinapotea ila hiyo hali haikunipa shida nilidharau halafu ilikuwaga ni home tu, Ila sasa hivi hata nikiwa kwengine.

Sasa kuna kivuli hicho kimenijia kwa mara ya tatu sasa hicho hakipotei kinakaa na huwa kwenye kuta za sitting room taa zikiwa zimezimwa usiku wa manane.

Leo hii ni mara ya tatu, huwa nakiona nikiwa macho yanaangalia pembeni nikigeuka nikiface kinapotea sasa leo nimemwita mama nikamwambia kile kivuli nachokwambia kiko ukutani vipi unakiona huku mimi nikiwa naangalia pembeni lakini nakiona mama akaniambia haoni kitu.

Sasa ndugu zangu wa JF mnisaidie hiki ni kitu gani maana nikiwaambiwa watu wengine wananiona kama nina wasiwasi au nimechanganyikiwa.

Kivuli chenyewe ni dude kubwa hivi halafu naona mkono wenye kucha ndefu ni cheusi.

Hii hali imenishangaza sana, mama ananiambiwa tunakuitia shehe akusomee.

Ila nimebaki na maswali, hiki kivuli kinataka nn kwangu kama kuna wadau wanafaham hali hii wanielezee.

Sitanii ndugu zangu nahitaji mawazo yenu
Uliwahi kuua?
 
Duuh, dunia ina mengi... Na usiku nao una mengi aisee.

Mtangulize MUNGU Kwa kila jambo ulifanyalo, Muombe MUNGU kabla ya kulala na baada ya kuamka kutoka usingizini .
 
Waswahili huwa na usemi wao
unaosema CHA MTU MAVI UKIKIONA
KITEME sasa bwana nikushauri jambo moja kama umewahi kuchukua kitu au mali ya mtu iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi fanya kurejesha hiyo mali au hicho kitu kwa mwenye nacho, hilo tatizo lako litakwisha kabisa...!!!!
Kama alimkojolea MKE wa mtu atautoaje huo mkojo?
 
Kila kitu kina formula zake... Na si kila mahali pana bahari ndugu
Mkuu mimi nina miezi kama miwili kuna tatizo limeanza kunitokea na sijui linasababishwa na nini. tatizo lipo hivi , kuna siku ulitokea moto chumbani na ukaunguza begi la mtoto wangu tu na nguo zake na inawezekana ulizima wenyewe maana mtoto yupo boarding na mimi nilikuwa kazini nilikuja kujua baada ya kurudi jioni, ikapita kama wiki asubuhi baada ya kujiandaa kwenda kazini wakati navaa viatu nikakuta kiatu ninachovaa kimekatwa kamba wakati usiku wakati naviandaa vilikuwa na kamba zake zikiwa nzima, sikuwaza nikabadirisha nikavaa vingine, hapa juzi nilienda south afrika niliondoka na nguo mbili tu za ziada kwa kuwa safari yangu ilikuwa ntakuwa kule kwa siku mbili tu nilivyofika kule wakati nipo hotel nimetoka kuoga nataka nibadilishe nguo nikakuta shat imekatwa kola haipo kabisa na surual imekatwa vipande vipande kama sambusa, mimi ni mtu wa kupuuza sana lakini kwa hili i think its to big for me , msaada wa ushaur na kwa uzoefu wako vipi kunaweza kuwa na mambo ya kiswahili katika haya yanayonitokea?
 
haya mambo naonaga sana ktk horror movies! fuata ushauri wa Mshana ikishindikana hama hilo eneo na ukishindwa kabisa basi fahamu utakuwa upo hollywood
 
Mkuu mimi nina miezi kama miwili kuna tatizo limeanza kunitokea na sijui linasababishwa na nini. tatizo lipo hivi , kuna siku ulitokea moto chumbani na ukaunguza begi la mtoto wangu tu na nguo zake na inawezekana ulizima wenyewe maana mtoto yupo boarding na mimi nilikuwa kazini nilikuja kujua baada ya kurudi jioni, ikapita kama wiki asubuhi baada ya kujiandaa kwenda kazini wakati navaa viatu nikakuta kiatu ninachovaa kimekatwa kamba wakati usiku wakati naviandaa vilikuwa na kamba zake zikiwa nzima, sikuwaza nikabadirisha nikavaa vingine, hapa juzi nilienda south afrika niliondoka na nguo mbili tu za ziada kwa kuwa safari yangu ilikuwa ntakuwa kule kwa siku mbili tu nilivyofika kule wakati nipo hotel nimetoka kuoga nataka nibadilishe nguo nikakuta shat imekatwa kola haipo kabisa na surual imekatwa vipande vipande kama sambusa, mimi ni mtu wa kupuuza sana lakini kwa hili i think its to big for me , msaada wa ushaur na kwa uzoefu wako vipi kunaweza kuwa na mambo ya kiswahili katika haya yanayonitokea?
duh, kuna viumbe watundu sana ktk ulimwengu huu! kaka ukipata suluhisho usisahau kuleta mrejesho
 
Kama kuna kikevi chochote unatumia Acha mara moja...
maana nna jamaa namfaham alikua anaanza kujifunza kuvuta BANGI/MARIJUANI Yeye alikua akiona kivuli cha ZIMWI/INSYUKA/GODIZILLA ama kiumbe cha ajabu kikimfata mda wote kumbe kwenye familia yao walikatazwa kutumia vitu hivi vya kilevi.
Hivyo nakushuri mkuu kama unatumia/unaonja/unajaribu kutumia kilevi chochote kile nakushauri Acha mara moja
Hahahhahahaaaaa et INSYUKA hii sinema ilinifanya nishindwe kukaa ndani peke yangu, pmbav zake yule insyuka kwa kunikosesha amani kipindi kile.
 
Inawezekana kuna jamaa yako anataka kukutoa kafara.

Omba.

Funga hata siku nzima usile kitu huku ukimwomba Mungu akuondolee hayo maruweruwe.

Na kama umedhulumu cha mtu urudishe!

Pole!
 
Mkuu mimi nina miezi kama miwili kuna tatizo limeanza kunitokea na sijui linasababishwa na nini. tatizo lipo hivi , kuna siku ulitokea moto chumbani na ukaunguza begi la mtoto wangu tu na nguo zake na inawezekana ulizima wenyewe maana mtoto yupo boarding na mimi nilikuwa kazini nilikuja kujua baada ya kurudi jioni, ikapita kama wiki asubuhi baada ya kujiandaa kwenda kazini wakati navaa viatu nikakuta kiatu ninachovaa kimekatwa kamba wakati usiku wakati naviandaa vilikuwa na kamba zake zikiwa nzima, sikuwaza nikabadirisha nikavaa vingine, hapa juzi nilienda south afrika niliondoka na nguo mbili tu za ziada kwa kuwa safari yangu ilikuwa ntakuwa kule kwa siku mbili tu nilivyofika kule wakati nipo hotel nimetoka kuoga nataka nibadilishe nguo nikakuta shat imekatwa kola haipo kabisa na surual imekatwa vipande vipande kama sambusa, mimi ni mtu wa kupuuza sana lakini kwa hili i think its to big for me , msaada wa ushaur na kwa uzoefu wako vipi kunaweza kuwa na mambo ya kiswahili katika haya yanayonitokea?
Bila shaka yoyote kuna "mambo ya kiswahili" kama unavyoyaita mwenyewe. Haijalishi jina gani unayaita, ninachosema ni kwamba kuna nguvu za giza zinatawala maisha yako na unapaswa kufanya kitu ili uwe huru.

Kwanza kabisa mimi sishangai kwamba unapatwa na mambo hayo kwani wewe mwenyewe unafanya kitu ambacho kinakaribisha hali ya kutawaliwa ama kuingiliwa na nguvu za giza. Utashangaa lakini ukweli ndio huo: KWANZA KABISA BADILISHA JINA UNALOTUMIA HAPA JF. "Kichaa Msafi"! Hili ni jina hatari kabisa! Fanya haraka kubadilisha na kwingineko, Whatsapp, Facebook, etc kama unatumia jina hili ama jingine lisilo zuri.

Huwezi kuamini kwamba mwanadamu hujiletea yote mwenyewe kwa matendo yake, iwe ni baraka au laana, ni wewe tu kwa hiari yako!

Baada ya hapo, tubu dhambi zako, acha ushirikina, tupa mbali (choma moto) chochote cha kishirikina; hirizi, bangili, mikufu, hereni, n.k.

Utahitaji msaada ya mtu wa kweli wa Mungu kwa ajili ya maombezi zaidi. Lakini anza sasa kujitakasa na kutubu, halafu tafuta mtu wa kweli wa Mungu kwa maombezi. Omba Mungu kwanza, usiende kwa mchungaji, nabii, mtume yeyote tu. Naposema mwombe Mungu, namaanisha mwombe Yesu Kristo wa Nazarethi. Usiseme Mungu naomba...., bali sema Bwana Yesu naomba....

Kama utapenda tutawasiliana zaidi. Bwana Yesu na akusaidie kutoka kwenye utumwa wa shetani sasa.
 
nashukuru kwa ushauri lakini nikuambie tu kwamba toka nimepata akili mpaka leo hii sijawahi kushiriki shirki ya aina yoyote ninavyosema shirki namaanisha sijawahi kwenda kwa mganga na sijawahi kumtegemea mwanadam zaidi ya Muumba wa Mbingu na Ardhi namaanisha Mungu, sijawahi kuingia mkataba wowote na nguvu za giza , hapa nilileta kama changamoto tu ninayopitia kwa sasa
 
Yawekana wazazi, angalia mienendo yao kuhusu masuala ya giza, je wapo vipi? Pia angalia yale unayopenda kuyafanya pengine ukifikiri hayana madhara, kama vile mavazi, unavyoangalia kwenye TV, n.k.
 
Tafuta sheikh akufanyie dua huo ni ushirikina ndugu MTU asikudanganye.
 
Fanya maombi sana (Dua) kila siku hakikisha kabla ya kulala unafanya dua ,hii dunia ina mengi ,inawezekana ni mauza uza yanakuandama ,muombe mungu mzaada katika hili naamini utavuka ,
Tunaamini Mungu anajua shida yako kabla hata hujawaza kumuomba kuna haja Gani mpaka utike jasho kwanza ndio akusaidie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom