Kivuko MV Kigamboni wanawatapeli watalii

Democracy999

JF-Expert Member
May 26, 2012
945
189
Nimeona jana Tarehe 9 Julai saa sita Mchana hivi. Watalii walijipiga picha wenyewe.

Baada ya hapo wakafuatwa na jimama mweusi na kijana mweupe kiasi, walilipa 50,000 Tsh kwa kila picha waliojipiga, wageni walijitetea kuwa hawajawapiga Watu wengine, walijibiwa kwa ukali kuwa ni eneo la Jeshi na Ikulu, Watalii walilaani sana japo hawakuwa na ujasiri wa kukubali kushtakiwa.

Watu chomboni walinung'unika kuwa mara kadhaa waliona matukio kama hayo.

Tunashauri mamlaka husika kuliangalia swala hilo.
 
It's very easy! Ni suala la kuweka tu vijitangazo "PHOTO SHOOTING STRICTLY NOT ALLOWED" badala ya kuviziana. Mtalii anayejua hapo pana Ikulu au Kambi ya Jeshi ni yupi kama sio kuwaonea tu.
 
Mbona ilani IPO ukiwa unaingia kukata ticket?
Kuna moja inakataza picha na nyingine inakataza kuvuta sigara
 
Baada ya hao watalii kutoa hiyo 50,000/= kama faini, je walipatiwa stakabadhi ya Serikali??
 
Kama mtu unayejiamini na unayeweza kutetea haki yako na ya wengine wewe uliwasaidiaje? Je walipewa risiti? Kama hapana nyie mliokuwepo mlihalalisha uhalifu. Vinginevyo mngesimama kutetea hilo ikiwa kweli mnajitambua. Hukutimiza wajibu wako alafu unataka eti maamlaka husika ambazo hazikuwepo eneo la tukio ndo ziangalie.
 
Ukimuuliza Faustine Ndugulile mbunge wetu anakaa kimya kama hakusikii hii ni kero na aibu kwa taifa.
 
Mbona watu kibao wanapiga picha wakiwa kwenye feri, na sijaona wakisumbuliwa, wau kwa sababu ni ngozi nyeupe.
 
Aisee Kumbe Pantoni sheria zake kali namna hiyo?

Hahaha,Sasa mbona Boat za kasi za Safari za kuja Zanzibar hakuna Masharti ya kupiga picha,na wakati na zenyewe zinapita ukanda huohuko wa maji wakati wa kuingia na kutoka,na mtu anaweza ku zoom na kupiga picha tena kwa ubora zaidi.
 
kila mtu anakula ofisini kwake na hao wazungu maboya tu mzungu gani anakubali kuburuzwa kiboya boya namna hiyo unapiga kiingereza cha kooni huyo Mmatumb.i lazima angeingia mitini bila kula huo mlungula
 
Hivi hiyo Ikulu na White House ya Obama ipi ina umuhimu? Mbona White House watu wanaenda tour, wanazunguka hadi kushika fensi... inakuwaje hilo gofu wanazingua
 
Back
Top Bottom