Kivuko Kigamboni chasababisha maafa


Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,386
Likes
38,563
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,386 38,563 280
WATU watatu wamepoteza maisha katika matukio tofauti jijini Dar es salaam, mmoja akikandamizwa na mlango wa kivuko akiwa ndani ya gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema kijana aliyetambuliwa kwa jina moja la Vincent, amefariki dunia kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Hiace maeneo ya Yombo Makangarawe jana saa 12:30 asubuhi.
Misime alisema polisi inaendelea na msako wa gari hilo ambalo linafanya safari zake kati ya Tandika na Yombo Buza.
Shuhuda wa ajali hiyo, Ally Ngwike, mkazi wa Yombo Makangarawe, alisema marehemu alikuwa na tatizo la akili na gari lililomgonga lilikuwa mwendokasi.

Katika tukio jingine, Misime alisema lilitokea maeneo ya feri baada ya gari aina ya Toyota pickup kugandamizwa na mlango wa kivuko cha Mv Magogoni na kusababisha kifo cha dereva wa gari hilo, Mohamed Nandumbe (58).
Dereva huyo alikuwa mkazi wa Magomeni na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni iliyopo Kigamboni. Mganga wa zamu wa hospitali hiyo, Dk Pili Mwera, alithibitisha kupokea mwili huo.

Wakati huohuo, Hassan Juma (25), mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, dereva wa pikipiki aina ya Chuma alikutwa amekufa maeneo ya Mbagala Nzasa.

Mtu wa karibu na Juma, Ibrahim Kagina, alisema mara ya mwisho waliachana saa 8:00 usiku.
 
TUKUTUKU

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Messages
11,841
Likes
49
Points
145
TUKUTUKU

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2010
11,841 49 145
Oh maskini mungu azilaze roho za marehemu peme peponi!bwana ametoa bwana ametwaa,jina la bwana lihimidiwe!!
 
M

Mike 1234

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Messages
1,634
Likes
4
Points
0
M

Mike 1234

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2009
1,634 4 0
poleni sana wote mliofikwa na msiba huu,ila zote zimesabishwa na uzembe
 

Forum statistics

Threads 1,235,092
Members 474,351
Posts 29,212,003