Kivuko cha MV. Temesa huipa Serikali hasara ya Milioni 10 kila Mwezi. Kilitengenezwa kwa bilioni 3

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Kivuko cha MV. Temesa, kinachotoa huduma ya usafiri wa abiria kati ya Luchelele Jijini Mwanza na Kijiji cha Ilunda, kata ya Ngoma'B' Wilayani Sengerema kilichojengwa na serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 3 kinadaiwa kujiendesha kwa hasara kutokana na kukosa abiria.

Hatua ya kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 75, kwa siku, mapato yake hayazidi Shilingi laki 2 wakati gharama za uendeshaji zikidaiwa kufikia Shilingi laki 5, kitendo ambacho kinatajwa kuisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 10 kila mwezi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe.Mwita Waitara akizungumza baada ya kusikiliza kero za wananchi na matatizo ya miundombinu maeneo ya vivuko na bandari, amemwagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Japhet Maselle kuyafanyiakazi malalamiko yaliyoelezewa.

ITV
 
Wahuni tu mbna kuna sehemu kuna uhaba wa hvo vivuko, hamisha chap
 
Hiyo sehemu kama hakuna abiria kivuko kinafanya nini?

Kivuko linaweza piga safari nyingine nyingi tu, na hao wa kiyo route wakapangiwa safari Mara Moja or mbili kwà siku.
 
Serikali ina wajibu wa kuwahudumia wananchi wake. Bila kivuko kama hicho, hao wananchi wangesafirije? Halafu itakuwaje kama baadae biashara na ukuaji wa shughuli za kiuchumi utaongezeka?
 
Tufanyeje
  1. Tuachane na kivuko tujenge daraja?
  2. Tuwahamishe wakazi wa hicho kijiji kwenda ng'ambo nyingine?
  3. Tuwanunulie kivuko kidogo na kilichopo kipelekwe kwingine?
  4. Tujiulize pia barabara zetu zote nchini zinarudisha gharama za ujenzi wake?
 
Kwa haya makato ya uzalendo aisee wawapeleke hata bure hii serikali isilete uhuni sasa
 
Eti think tank wa nchi ni Zungu. Wachumi wamejificha nao wanaaubiri uteuzi au ubunge
 
Back
Top Bottom