Kivuko cha Mv kivukoni na Mv magogoni acheni kufungia Maboya ya kujiokoa katika stoo kwa kufuli kubwa!

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Nimewahi kukitumia kivuko cha Mv Alina, Mv kigamboni na Mv magogoni,

Nimeshangaa kabisa maboya ya kujiokolea yako store yamefungiwa ndani ya kivuko kwa kufuli kubwa,

Nimerudi Tanzania mwezi wa 11 nimekuta hali ni Ile ile,

Maboya yamefungiwa mpaka kufuli lina kutu,

Tunaandaa nini??
 
Mkuu nilikua nawaza sana hicho kitu hata vivuko vyote vya Mwanza
Unakuta Vyumba vya maboya vimefungwa na kufuli kubwa tena Lina kutu kwakweli inashangaza

Ni vyema mamlaka husika.zitoe tamko ikiwezeka abiria anapoingia tu kwenye kivuko apewe boya
 
Wakati wa kupanda boti/meli tupewe life jackets, tuvae kabisa na wakati wa kuteremka tuwape wahusika. Mambo ya kusubiri ajali itokee ndo uvae, sidhani kama hata hilo jacket utaliona!
BBC
 
Mkuu nilikua nawaza sana hicho kitu hata vivuko vyote vya Mwanza
Unakuta Vyumba vya maboya vimefungwa na kufuli kubwa tena Lina kutu kwakweli inashangaza

Ni vyema mamlaka husika.zitoe tamko ikiwezeka abiria anapoingia tu kwenye kivuko apewe boya
Ndiyo
 
Kweli mkuu. Lazima serikali ifanye linalowezekana kuepuka na ajali za aina hii na zinapotokea walau tuwe tayari tumejiandaa kupunguza madhara. Hivi vyombo vya majini vibabeba watu wengi sana, msiba wake hua ni mkubwa.
 
Nimewahi kukitumia kivuko cha Mv Alina, Mv kigamboni na Mv magogoni,

Nimeshangaa kabisa maboya ya kujiokolea yako store yamefungiwa ndani ya kivuko kwa kufuli kubwa,

Nimerudi Tanzania mwezi wa 11 nimekuta hali ni Ile ile,

Maboya yamefungiwa mpaka kufuli lina kutu,

Tunaandaa nini??

Niliwahi kuandika hapa kuwa SUMATRA wapo likizo, nadhani mmoja ya wachangiaji hapa atakuwa mfanyakazi wa SUMATRA alikuja na povu balaa
 
Kuna siku nilipanda MV magogoni basi kabla ya kufika kigamboni ikakosa uelkeo kidogo aisee maboya yaliisha dk 2 tu na hayakutosha kuna haja capacity ya watu iendane na idadi ya life jackets kwenye vyombo vyetu ajali haipigi hodi rip ndugu zetu
 
Moderate Hii Thread Iwekwe Sticker Ikae Juu Kabisa Ya Jukwaa Tutakuwa Tunatoa Updates Kila Mtu Akipanda Kivuko Iwapo Life Jackets Zimefungwa Kwenye Vyumba Vyenye Kufuli

Nashauri iwe kwa vyombo vyote vya usafiri majini na nchi kavu, nasema hivyo kwasababu hata kwenye mabasi kuna madudu mengi yanayofumbiwa macho na askari wa usalama barabarani, moja ya sababu ikiwa ni rushwa pamoja na wao kumiliki vyombo hivyo.

Nadhani kuwepo kwa uzi wa kudumu kutasaidia wadau kupost picha za matukio halisi ili viongozi wa mamlaka za uteuzi waone yanayojiri kwingineko.

Hata hivyo basi tu, ukitazama kwa umakini, kwenye website ya polisi na SUMATRA walitakiwa kuwa na forums kwa ajili ya wadau kuweka maoni na kero wanazokutana nazo, lakini kwasababu wanazozijua wao mabo hayo wanayaona kama vile kazi isiyo na maslahi.
 
Wazingatie pia uwezo wa chombo kubeba abiria na mizigo... Isiwe watu mia ndio wana stahili kubebwa na kupewa life koti alafu wana jaza mia mbili... Hizi life jackets mia watazitoa wapi??

Pia waache kufanya kazi kwa mazoea... Wafanye kazi kwa weledi...

Pia kwanini meli ya MV bukoba INA karibia kutia nanga INA zama, MV nyerere na zingine... Hata magogoni hapo kuna muda magari yanatumbukia wakati kivuko ndio kina tia nanga... Hapa napo kuna kujifunza... Kuwa abiria tuache uswahili wa kukimbilia kushuka... Na kusababisha uzito kuegemea sehem Moja mwisho maafa
 
Sure
 
Back
Top Bottom