Kivinjari kipi ni bora zaidi


Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,235
Likes
52
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,235 52 0
Kivinjari ni Programu ya Kompyuta inayotumika kwa ajili ya kutembelea wavuti kwenye tovuti mbalimbali ndani ya mitandao mbalimbali duniani kama hichi unachosoma wewe saa hizi programu uliyotumia ndio kivinjari kwa kiingereza ni browser .

Watu mbalimbali wamekuwa wakihoji kivinjari kipi zaidi ni bora kwa matumizi ya kila siku kwenye shuguli za mawasiliano ya mitandao kwenye tovuti na wavuti mbalimbali ?

Wengine huwa wanajiuliza ni kivinjari kipi kizuri kwa kutembelea aina Fulani ya tovuti pekee , ni ukweli ulio wazi kwamba kuna aina nyingi sana za vivinjari vingine ni vya zamani sana tokea miaka ya 90 na zingine zimeanza kuingia sokoni kwa siku za karibuni .

Mfano kwa mimi napenda kutumia kivinjari ambacho ni chepesi katika kufunguka kwanza , ambacho kinahifadhi kila tovuti ninayotembelea saa zote na iwe na uwezo wa kunionyesha vitu vya mwisho nilivyotembelea kama chochote kikitokea kwenye kompyuta hiyo kuna wakati kuna weza kutokea tatizo ikawa mshike mshike , kwa bahati nzuri kwa matoleo mapya ya Kivinjari cha Internet Explorer 7 na kuendelea hili limewezekana ina sehemu ya thumble ambayo inaweza kuhifadhi vile ulivyotembelea kama ukija tena kwenye kompyuta hiyo ingawa huduma hii inafaa zaidi kwa wale wenye komputa binafsi kama ni sehemu za internet café inaweza kuwa hatari kwa usalama wa mteja waliyetumia komputa hiyo .

Pia ningependa kutumia kivinjari ambacho kina ingiliana na baadhi ya programu zinazohusiana na usalama wa komputa yangu kama antivirus , firewall , antispyware na zingine nyingi , sasa kumetokea tatizo kidogo la watu kukimbilia baadhi ya vivinjari bila kuangalia vitu hivi mfano vivinjari vingi sana havitambuliki na aina nyingi ya antivirus au hata vikitambulika havina uwezo wa kufanya kazi na antivirus hizo kwa wakati mmoja .

Ingawa mashambulizi mengi kwa njia ya mtandao yanatokea kwenye internet explorer , kivinjari hichi kimeonyesha ukomavu na ushirikiano mzuri kati yake na programu zingine za kulinda komputa na mali zingine za mteja hata unapotembelea tovuti nyingi duniani unashauriwa uwe na internet explorer zaidi ya nyingine .

Kutokana na umuhimu wa habari na huduma zingine za kupata mawasiliano ningependa kuwa na kivinjari kilichokuwa na huduma za ziada kama hizo kwa bahati mbaya vivinjari vingi duniani havina huduma hizi lakini unaweza kupata huduma hizo kutokea kwenye tovuti ambazo zinamilikiwa na kampuni zinazotengeneza vivinjari hivyo kama kwa internet explorer ni rahisi kutumia msn au bing , kwa chrome ambayo ni google yenyewe itakupeleka kwenye google news na huduma zao zinginekwa urahisi na wepesi zaidi .

Kama unataka kivinjari ambacho huduma hizi ziko moja kwa moja unatakiwa ujaribu kama flock , programu hii haiko sokoni kwa muda mrefu lakini toka imeingia imekuwa ikifanya vizuri sana na mpaka sasa sijaona shambulio dhidi ya programu hii kwahiyo naweza kusema nyota yake ina ngaa kwa sasa hatuwezi kuongelea siku zijazo .

Kwa wale wanaopenda kushusha vitu kwenye mtandao downloading nao wangependa kuwa na browser ambayo ina weza kuingiliana na programu za kurahisisha ushushahi wa nyaraka na programu kwenye mtandao , internet explorer imekuwa ikifanya vizuri katika ulimwengu wa kudownload na kampuni nyingi za programu zimeshauri kabisa utumia internet net explorer .

Na mwisho ni kwenye ulimwengu wa blogu tumeona jinsi google inavyofanya vizuri kwenye huduma yao ya blogspot lakini imeshindwa kuunganisha huduma hiyo ifanye kazi vizuri na kivinjari chao kinachoitwa chrome kama wewe una blogu yako umewahi kuona shida inayokuwa unavyojaribu kufanya mabadiliko kwenye blogu yako na chrome ? , hata hivyo internet explorer imekuwa na shida nayo kwenye kuweka linki katika post kwa siku nyingi .

Mambo mengine ya kuangalia ni kama kupata programu ya kivinjari hicho ni bure , ina uwezo wa kuresume kurasa wakati wowote kama mtandao umekuwa unaenda taratibu , ni rahisi kuiunganisha na programu zingine na hata kama imetokea kuleta shida ni rahisi kuhamisha settings na baadhi ya vitu kutoka kwenye programu hiyo kwenda nyingine ambayo unaitumia kwa wakati huo yaani iwe na muingiliano na programu hizo .

Kwahiyo kuna mambo mengi sana ya kuangalia na kufikiria kabla ya kuamua kivinjari kipi zaidi ni bora kwa matumizi ya mtu , lakini pia ni kujua kama kivinjari hicho kama kina uwezo wa kutekeleza mahitaji yako mengi ya kimtandao kwa kila siku nakama kina uwezo wa kuingiliana na programu zingine unazotumia kwenye komputa yako bila tatizo lolote .

www.wanabidii.net www.naombakazi.com www.askmaro.blogspot.com
 

Forum statistics

Threads 1,250,864
Members 481,514
Posts 29,748,655