Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Klabu ya Simba katika kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao 2022/2023 katika michezo ya Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa, leo Julai 13 2022 imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji (Attacking Midfielder) Augustine Okrah raia wa Ghana, kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Bechem United ya nchini Ghana.
"Mchezaji mkubwa mwenye hadhi ya kucheza timu kubwa kama Simba Augustine Okrah ni Mnyama". Imeeleza kwa ufupi taarifa kutoka klabu ya Simba.
Mghana huyu Okrah (28) ambaye alikuwa kwenye kiwango bora kabisa katika klabu ya Bechem United msimu wa 2021/22, ambapo cha kuvutia zaidi kwake ni uwezo wake mkubwa ndani ya dimba wa kutengeneza mabao na kufunga mabao akiwa amehusika mabao 18, huku akiwa amefanikiwa kufunga mabao 14, na akitoa pasi za mwisho za mabao 4 katika michezo 32 ya Ligi Kuu nchini Ghana.
Nyota huyu Okrah mwenye rekodi zake, ambaye anachezea timu ya Taifa ya nchini Ghana chini ya Kocha Otto Addo, amewahi pia kuzitumikia klabu kadhaa, zikiwepo RB Ghana, Al Merreikh, Asante Kotoko na Bechem United.
Hakika huu ni usajili wa kisomi ndani ya viunga vya Msimbazi, Augustine Okrah ni mchezaji ambaye namba zake hazidanganyi huko alikotoka ameweza kufanya vema kabisa, ambapo kwa msimu huu wa 2022/23, anaungana na Moses Phiri akitokea Zanaco FC na Victor Akpan raia wa Nigeria kwa wachezaji wa Kimataifa.
Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana