johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,780
- 141,667
Pamoja na kwamba wakuu wengi wa mikoa ubunifu wao bado uko chini hali inayowafanya waachwe mbali kiutendaji na mkuu wa mkoa wa Dsm, mimi naona hata baadhi ya mawaziri wanalo la kujifunza kutoka kwa huyu kijana. Kwa mfano wakati Rais akihangaika kuziba mianya mbalimbali ya upotevu wa mapato ya serikali na kuitengenezea vyanzo vipya, Wizara ya maliasili na utalii imekuwa butu kabisa katika ubunifu. Nimshauri tu waziri wa maliasili analo la kujifunza ktk area ya ubunifu kwani tunaitazama wizara yake kama sehemu muhimu sana katika kuongeza pato la serikali. Wapo mawaziri wengine mfano Mazingira, Kilimo na hata yule wa biashara na uwekezaji tunahitaji kuwaona mkija na ubunifu na siyo vibaya mkapita katika ofisi ya RC Dsm kujichotea uzoefu. Kwakweli tukiweka chuki zetu za kisiasa pembeni na kujikita kwenye utendaji tutakubaliana kuwa kijana anapiga kazi. Wakuu haya mambo ya kusoma sana ni kukariri tu fikra za watu wengine na ndio maana Prof Lipumba Cuf iliyojengwa na kina Mapalala inamfia mikononi kama ilivyo kwa Prof Muhongo aliyechemka kwenye mambo aliyoyabobea! Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni hata kama hamumpendi!!!