Kiukweli, nimeifurahia hukumu ya Lengai Ole Sabaya

Nawasalimu waungwana wa JF,

Jana ilisomwa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake. Sasa inajulikana kuwa wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Kila upande: wa mashtaka na ule wa utetezi una haki ya kukata rufaa ndani ya muda na taratibu zinazoainishwa na sheria.

Kiukweli, bila kujali kitakachotokea kwenye hatua ya rufaa, nimeifurahia hukumu ya akina Sabaya. Sifurahii mwenzangu Sabaya na yeyote yule kutumikia kifungo jela. Sifurahii mateso kwa mwenzangu yeyote yule. Jela si mahali pa kupafurahia.

Nilichokifurahia ni UJUMBE WA WAZI uliotumwa na Mahakama kupitia hukumu ile. Ujumbe wa kwamba kwenye jinai matendo ya mtu hutengwa na nafasi yake ya kiuongozi na kisiasa. Yaani,kiongozi anapotenda jinai hapaswi kujibanza kwenye nafasi yake ili kijinasua. Uongozi umetengwa mbali na matendo binafsi ya mtu aliyekuwa kiongozi. Ujumbe murua kabisa.

Hukumu ya Ole Sabaya inashabihiana na ile ya kwenye shauri la madai la Mchungaji Mtikila dhidi ya Mzee Augustino Mrema. Kwenye shauri tajwa, mahakama ilitenganisha matendo/maneno ya mtu binafsi na uwaziri wake(Mrema).

Hukumu ya Sabaya itufunze na kutukumbusha kutenda ya haki na halali pale tunapobarikiwa kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali. Hukumu hiyo itukumbushe pia kuwa uongozi hautaweza kuwa kichaka cha kujificha pale ambapo jinai au madai yatakapoletwa dhidi ya mhusika.

Jinai hufa na mhusika tu, haizeeki!
Sasa hapa umechambua nini kama Lawyer? Armed robbery ilifanyika au hizo ngonjera za kipuuzi.?
 
Back
Top Bottom