Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Nimemsikiliza na kumfuatilia Meya wa Kinondoni,Mstahiki Boniface Jacob. Tangu achaguliwe kuwa Meya,Mstahiki Jacob amekuwa akionyesha tofauti katika usemaji na utendaji wake. Kuanzia Stendi ya Mabasi Ubungo hadi soko la Simu 2000 pale Sinza,Meya Jacob ameonyesha dhamira na utayari wa kuleta maendeleo Kinondoni kama Manispaa. Akamaliza kuchambua kwa kina giza la Kiwanda cha Urafiki.
Nimemsikiliza tena leo kupitia Redio ya East Afrika kwenye kipindi cha Supermix. Ameelezea mambo mbalimbali katika manispaa yake. Hakika,anaeleza mambo akiwa ana uelewa mpana na taarifa za kutosha. Maswali yote ya mtangazaji Zembwela yamejibiwa kwa kiwango kikubwa na kutosheleza. Ameainisha mipango ya masoko, bomoabomoa ya kisheria na kadhalika.
Jambo kubwa la kufurahisha kwake ni kuelewana vya kutosha na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe. Salum Ally Hapi bila kujali vyama vyao na itikadi zao. Meya ni kutoka CHADEMA na Mkuu wa Wilaya anatokana na CCM. Hawa wanaweka utaifa mbele na kuwatumikia wanaKinondoni. Watafika mbali wawili hawa.
Kimsingi,Meya Boniface Jacob anastahili kuwa alipo. Kwa mwendo wake,atafika mbali kisiasa na kiutendaji.