Kiukweli, 'barua' ya Katibu wa Bunge kwa familia ya Lissu yaweza kupindua matokeo mapema sana. Spika Ndugai 'haijui' barua hiyo?

Kumbe mnajua alienda Amerika na mnajua alienda akitokea wapi na baada ya hapo akarudi wapi!!!!???

Kiukweli Jiwe ndio muasisi wa siasa za chuki na kuuana kwenye taifa hili!
Marekani alienda na akaongea na Raisi wa Tanzania aliyeko marekani balozi wa marekani Wilson Masilingi.Hawakukutana hospitali Bali mitaani Lisu akizurura mitaa ya marekani akila bata
 
Tutafika tu mnapopataka wala sio mbali!
Marekani alienda na akaongea na Raisi wa Tanzania aliyeko marekani balozi wa marekani Wilson Masilingi.Hawakukutana hospitali Bali mitaani Lisu akizurura mitaa ya marekani akila bata
 
Lipi jema kwenu?, basi asifungue shauri sasa, ujinga na uzwazwa mlionao ni kwamba mkishindwa Jambo lolote mahakamani hua mnadai ni maagizo toka juu, mkishinda haki imetendeka ,"pathetic "
PATHETIC ni kuamini kwamba kwa kuwa hakimu aliyeamua kesi hii ametenda haki, basi mahakimu wote na majaji wote wanatenda haki. Au kuamini kwamba kwa kuwa hakimu mmoja hakutenda haki, basi wote hawatendi haki.

PATHETIC Kuamini kwamba kwa kuwa Hitler alikuwa mjerumani na akawa mtawala katili, basi wajerumani wote ni wakatili. Kwamba kwa kuwa msukuma mmoja amekuwa rais wa nchi na uchumi umeparaganyika, basi wasukuma wote hawafai kuwa rais. PATHETIC
 
Kuna jambo la kujifunza ktk hili, kuna kitu kikubwa sana kinaitwa MUDA WA MAWASILIANO na kingine kikiwa ni ANUANI (kupitia kwa)

1. barua iliandikwa lini na mwaka gani? SAY 26 JUNE 2018 ama 26 june 2019
2. Barua iliandikwa kwa KAKA aliyepo TANZANIA na si kwa kaka aliyepo HOSPITALI ULAYA

Tunaweza tukapenda kumtetea kwa sababau za KIBINADAMU na KI-UTU kuwa mtu huyu ni mgonjwa, sababu hizo hizo haziondoi upande unaouma wa mgonjwa wetu akiomba kulipiwa KODI YA NYUMBA, CHAKULA na ADA ZA WATOTO kwa DIASPORA,
Naweza kusema hata NASSARI ALISEMA ATAENDA MAHAKAMANI baadaye tukashuhudia kuwa YOTE HAYA NI STAILI MPYA ZA KUUNGA MKONO JUHUDI
 
Unakumbuka kesi za Mbowe na Lema jinsi majaji walivyoshangaa wao kutopewa dhamana/kufutiwa dhamana?
Acha kuwa na akiliza za kijinga kisa unafaidika na huu utawala.
Mkuu unategemea zwazwa kama huyu anayenufaika na mfumo wa serikali hii aseme nini zaidi? Tumbo lake ndio linaloelekeza kichwa chake namna ya kufikiri,akili za sampuli hii niza kupuuzwa.
 
Yani awamu hii kila kona ni mtafaruku viongozi kusemana vibaya,majungu,fitina,kujipendekeza, ukatili.

ndugai vs makonda.
majaliwa vs makonda.
nape vs makonda.
magu vs lisu.
magu vs membe.
musiba vs makamba

mda si mrefu itakuwa Magu vs Magu.

mpaka ifike 2025 huyuu jamaa atakuwa ameshaharibu hii inchi sanaaaaa, yote hayaa yeye ndio chanzo.


Mungu wetu si kiziwi hivyo atupe hili donda ndugu kwa miaka mingine 5.
 
Nawiwa kukiri kufahamu kuwa jana limetolewa tangazo Bungeni kuwa Ubunge wa Tundu Antipas Lissu wa Singida Mashariki umekoma na jimbo lake liko wazi. Nimefahamu haya hapahapa JF kupitia bandiko la kaka na mtani wangu Pascal Mayalla.

Nimesoma na kusikia tangazo la Spika ambalo hasa limejikita kwenye mambo mawili: utoro wa Lissu Bungeni ( kutojulikana alipo na anachofanya) pamoja na kutojaza Fomu za Maadili ya Viongozi. Hayo ni mambo ya kisheria na kiutaratibu.

Niweke wazi kabisa hapa kuwa mimi ni muumini wa utii wa sheria na taratibu zilizowekwa. Kila Taasisi na jumuiya ya watu huwa na sheria na taratibu za kufuata, Bunge halikadhalika. Kufuata sheria na taratibu huponya,huepusha na kulinda. Kutofuata hutisha,huathiri na kuadhibu. Aliyoyasema Spika ni masuala ya kisheria na kiutaratibu.

Mkuu BAK amepandisha uzi wenye majibu ya Lissu kwa jambo lililojitokeza jana. Alikuwa akizungumza na BBC. Nimevutiwa na kupata mambo mawili. Mosi, Lissu analenga kufungua shauri Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa kukoma kwa Ubunge wake na jimbo lake kuwa wazi kwa sababu zilizotajwa. Pili, Lissu amesema kuwa kuna mawasiliano ya barua kati ya Ofisi ya Katibu wa Bunge na familia yake kuhusu maendeleo yake kiafya.

Barua husika aliandikiwa kaka wa Lissu, kwa niaba ya familia na Lissu mwenyewe. Ni Wakili Msomi Mwandamizi Alute Mughwai ndiye kaka wa Lissu. Kuandikiana barua humaanisha kufahamika mahali wahusika wa barua hizo walipo. Na kujua na kinachozungumziwa. Hakika,ni barua muhimu.

Kwangu binafsi, sababu ya utoro na kutojulikana alipo Lissu ni kuu kuliko iliyobaki. Ni kwakuwa inayofuata huweza kumalizwa nguvu na uamuzi juu ya hiyo. Yaani, ikithibitika kuwa Bunge lilijua lipokuwepo Lissu na alichokuwa akikifanya, ujazaji wa fomu za maadili unazungumzika. Kama alikuwa mgonjwa,angejazaje?(kwa mfano).

Ndiyo maana nasema kuwa kama kweli kulikuwa na barua kutoka Ofisi ya Katibu wa Bunge maana ya haraka ni kuwa Bunge lilifahamu alipokuwa Lissu na alichokuwa akikifanya. Kama barua hiyo ipo, Spika alipaswa kujua kabla ya tangazo lake.

Naamini, 'barua' ya Katibu wa Bunge kwa familia ya Lissu inaweza kupindua matokeo mapema sana baada tu ya mechi kuanzia kuchezwa Mahakama Kuu ya Tanzania. Tusubiri tuone!
Lawezekana sana kwenye nchi yenye kufuata utawala wa sheria.
Sifa ya Tanzania kwa sasa hivi ni utawala wa mtu mmoja. Asemalo ndiyo katiba na sheria za nchi.
We have gone to the dogs.
 
Acha uongo poyoyo ww , sheria inasema usipokuwepo kazini bila ya ruhusa/ taarifa au SABABU ZA MSINGI.
Huyo ni muongo hii ndiyo sheria yenyewe
Kazi na Kuugua
Likizo ya kuugua yenye malipo
Mwajiri anahitajika kumpa mfanyakazi livu ya ugonjwa ikiwa bodi ya matibabu imethibitisha kwamba mfanyakazi ni mgonjwa, amepata ajali, ameambukizwa maradhi yanayotokaka na au akiwa kazini na kwa hivyo hawezi kufanya kazi. Hata hivyo, sheria inatofautisha kati ya magonjwa/maradhi ya kawaida na maradhi ya kikazi (yanayotokana na au ukiwa kazini). Mfanyakazi ana haki ya kupata siku zifuatazo za ugonjwa ikiwa yeye ni mgonjwa kwa sababu ambazo hazihusiani na ajira: miezi miwili ya livu ya muda na malipo kamili; na livu ya ugonjwa ya miezi mitatu na malipo nusu (ikiwa bodi ya matibabu itahakikisha kwamba mfanyakazi hawezi bado kufanya kazi). Ikiwa baada ya miezi 05 kuisha, bado mfanyakazi haiwezi kufanya kazi, huenda mwajiri akakatiza mkataba wa ajira.

Katika hali magonjwa ya kikazi au hatari za kikazi, haki za livu ya ugonjwa ni kama ifuatavyo: Miezi 06 ya livu na mshahara kamili; miezi 03 ya livu ya ugonjwa na mshahara nusu (ikiwa bodi ya matibabu itathibitisha kwamba mfanyakazi hawezi bado kufanya kazi). Ikiwa baada ya miezi 09 kuisha, bado mfanyakazi haiwezi kufanya kazi, huenda mwajiri akakatiza mkataba wa ajira.

Ikiwa mfanyakazi ni mgonjwa sana kufanya kazi kwa sababu ya HIV/Ukimwi, huenda mwajiri akakatiza kazi kwa sababu ya kutoweza kufanya kazi kama ilivyotolewa chini ya Sheria ya Ajira (kutoweza kufanya kazi ni moja ya misingi halali ya kusimamishwa kazi).

Ugonjwa wa mfanyakazi sio sababu nzuri ya kukatiza mkataba wa ajira na mfanyakazi haiwezi kusimamishwa kazi kwa sababu ya kutokuwepo kazini kwa sababu ya ugonjwa.

chanzo: § 60 & 69 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005

Huduma ya matibabu
Faida za matibabu zinapatikana kwa wafanyakazi wenye bima na zinajumuisha huduma ya kawaida ya matibabu, huduma ya mtaalamu, dawa, kulazwa, na usafiri.

Sheria ya Kuwafidia Wafanyakazi inamlazimisha mwajiri kugharimia gharama alizopata mfanyakazi ndani ya Zanzibari au kwa idhini ya Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu, nje ya Zanzibari kama matokeo ya ajali inayotokana na kazi, gharama hizi zinahusiana na dawa, upasuaji na matibabu ya hospitali, huduma ya wauguzi wataalamu na utoaji wa dawa; utoaji wa udumishaji, ukaratabati na ubadilishaji wa viungo na vifaa bandia.

Usalama wa kazi wakati wa kuugua
Ajira ya mfanyakazi ni dhabiti wakati wa ugonjwa na maradhi/ugonjwa hauwezi kivyake kuwa msingi wa kusimamishwa kazi. Katika hali ya ugonjwa wa kawaida, sheria inatoa kwamba ajira ya mfanyakazi iwe dhabiti kwa miezi 05 ya kwanza ya ugonjwa na katika hali ya maradhi ya kikazi, ajira iwe dhabiti wakati wa miezi 09 ya kwanza ya ugonjwa. Matoleo haya sio ya mwisho na makubaliano ya pamoja yanaweza kutoa vipindi virefu zaidi wakati ajira ya mfanyakazi mgonjwa nio dhabiti.

Mfanyakazi ambaye amekuwa akimfanyia kazi mwajiri kwa kipindi cha miezi sita anastahiki livu ya ugonjwa.

chanzo: § 69 ya Sheria ya Ajira Nambari 11 ya 2005
 
Naamini, 'barua' ya Katibu wa Bunge kwa familia ya Lissu inaweza kupindua matokeo mapema sana baada tu ya mechi kuanzia kuchezwa Mahakama Kuu ya Tanzania. Tusubiri tuone
Nyie watu mnajichanganya
Kuna uzi hapa,huyo kaka anadai wMeandika barua 11,haijajibiwa hata mija
Usanii wenu utajulikana mkienda mahakamani
 
Nyie watu mnajichanganya
Kuna uzi hapa,huyo kaka anadai wMeandika barua 11,haijajibiwa hata mija
Usanii wenu utajulikana mkienda mahakamani
Uwe unasikiliza vizuri. Barua zilijibiwa na kulikuwa na ahadi ya kutuma madaktari bingwa Nairobi na hata Ubelgiji. Pathetic!
 
Dreamliner sasa linaenda chato moja kwa moja, air hostels sijui walikuwa wangapi?????? Hii ni aibu kubwa baada ya Mobutu mfalme mpya mzalendo na mbana matumizi.
 
Chuki inamaliza maarifa
Hii ni Afrika na watu wana nguvu kuliko taasisi/mahakama. Usishangae ikatoka amri toka juu kwamba hiyo kesi iendeshwe mpaka jiwe anapotoka madarakani awamu yake ya pili. Kama huamini watu wana nguvu kuliko taasisi angalia sheria nyingi zilizotungwa awamu hii ya jiwe, nguvu zinatolewa kwenye taasisi na kupewa mtu (msajili), yeye ndio anaamua kila kitu! Na hapa kwetu Jaji mkuu ndio huyo hana meno.
 
Back
Top Bottom