Kituo cha watoto chafungwa kwa tuhuma za kunajisi wavulana

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Mahakama nchini Kenya imeamuru kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika Kaunti ya Machakos kifungwe mara moja, kufuatia tuhuma kuwa wavulana tisa walikuwa wakinajisiwa kwenye kituo hicho.

Idara inayoshughulikia watoto katika Kaunti hiyo ilipokea amri ya mahakama na kuifanyia kazi jana (Jumatano) ikisaidiwa na jeshi la polisi kufunga kituo hicho kilicho chini ya Kanisa Katoliki.

Wavulana hao tisa wanaodaiwa kuingiliwa na mpishi wa shule hiyo wamepelekwa katika kituo maalum na salama zaidi katika Kaunti hiyo kiitwacho Machakos Rescure Centre and Remand Home.

Kituo hicho cha watoto waishio kwenye mazingira magumu ambacho kina shule ya msingi, kinatunza jumla ya wavulana 39.

Tuhuma za wavulana kufanyiwa vitendo hivyo haramu ziliibuliwa Februari mwaka huu baada ya mvulana mmoja kutoa taarifa kuwa amekuwa akiingiliwa na mpishi ambaye amefanya kazi katika kituo hicho kwa miaka takribani kumi.

Mtoto huyo alieleza kuwa mpishi alikuwa akiwaita jikoni na kuwafanyia vitendo hivyo usiku na pia aliwatishia kuwa angewanyima chakula endapo wangemueleza mtu yeyote anachowafanyia.

Kwa mujibu wa Citizen, vipimo vya kitabibu vilivyofanywa katika Hospitali ya Machakos vimethibitisha kuwa mvulana huyo alikuwa akiingiliwa. Polisi wameanza kufanya uchunguzi zaidi kuhusu suala hilo wakimshikilia mpishi huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anawaingilia kinyume na maumbile/anawapiga magoli kama kagere/

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Kenya hamna sheria ya kunyongwa? Hawa watu kama kweli wanahusika hawahitajiki katika jamii.
 
Wafiraji kila kona ya nchi!! Kuna wengine wanawafira wake zao humu na wao watajifanya kusikitika! Astaghafirulah!
 
Nachoshangaaga eti hao polisi wanafanya uchunguzi wakati hadi daktari kathibitisha kuwa madogo wanalalwa na huyo njimbi,polisi emu zindukeni bana,kamata hiyo chalii,kata dudu yake,peleka gerezani maisha ikainamishwe
 
Idara inayoshughulikia watoto katika Kaunti hiyo ilipokea amri ya mahakama na kuifanyia kazi jana (Jumatano) ikisaidiwa na jeshi la polisi kufunga kituo hicho kilicho chini ya Kanisa Katoliki.
kwa nini Lakini? Hamukomi tu? Badilikeni
 
Daah! Inaumiza sana hii.

Achukuliwe hatua sababu huenda hao tisa ikawa idadi ndogo kutokana na muda aliokaa hapo kama mpishi.
 
Back
Top Bottom