Kituo cha uwekezaji na Serikali ya mkoa wa Lindi waanzisha dawati la uwekezaji kushughulikia changamoto

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
258
500
Serikali Mkoani Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC wameanzisha Dawati maalum la uwekezaji ambapo masuala yote yanayohusu uwekezaji sasa yanashughulikiwa kupitia katika dawati hilo ambalo lengo lake ni kuwaweka karibu na kuwahudumia kwa upekee Wawekezaji wa Mkoa huo pamoja na kutangaza fursa zilizopo.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga amesema uamuzi wa Serikali wa kuanzisha dawati hilo Mkoani Lindi umekuja kufuatia kuwepo kwa fursa nyingi za Uwekezaji ambapo kwa kushirikiana na TIC wameweza kuzitangaza.

Mhe. Ndemanga aliyasema hayo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Dkt. Maduhu Kazi Mkoani Lindi, ambapo alisema kufuatia Kongamano la Uwekezaji lililofanyika mwaka jana waliweza kubaini masuala kadhaa ambayo yatasaidia kuongeza Wawekezaji.

“ Hapa Lindi tumeanzisha Dawati la Uwekezaji ambalo linatuweka karibu sisi na Wawekezaji wetu. Pia Ofisi ya TIC katika Kanda ya Kusini inafanya kazi nzuri ya kuhamasisha uwekezaji hivyo kwa kushirikiana nao tumepanga mambo makubwa na tutafanikiwa sana” alisema Mhe. Ndemanga.

Alisema Wawekezaji wengi wanafika Mkoani humo ambapo sasa kupitia dawati hilo wataweza kuwa karibu na kuwahudumia ipasavyo ambapo pia alizitaja baadhi ya Taasisi zilizoonesha nia ya kuwekeza ikiwepo Chuo Kikuu cha Dar es Salaama (UDSM) wanaotaka kujenga Chuo cha Utafiti wa Mazao, Chuo cha Usafirishaji na Chuo Kikuu cha Kiisilamu cha Morogoro; ambavyo vyote vimepata maeneo kwa ajili ya ujenzi wa vyuo husika.

TIC-310x165.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom